A
Anonymous
Guest
Naandika hii taarifa kwa niaba ya wafanyakazi wa Uhuru Publications Limited ambao wapo na wale ambao walishaondoka hata waliokufa pia, pamoja na wastaafu.
Kampuni hiyo yenye gazeti la Uhuru na Mzalendo inadaiwa mamilioni ya fedha za malipo ya mafao pamoja na michango ya wafanyakazi tena ni ile ya kisheria ya NSSF ambayo kwa miaka mingi haikuwahi kuipeleka NSSF licha ya kwamba iliwakata kwenye mishahahara yao.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba, katika siku za hivi karibuni baadhi ya viongozi wamekemea taasisi na kampuni ambazo hazipeleki michango ya wafanyakazi NSSF, lakini kampuni ya chama chao haitaki kupeleka haki hizo za wafanyakazi.
Hivi inachukuliaje watu hawa? Kuna waliostaafu zamani, waliohamia sehemu zingine kufanya kazi, waliokufa na hata waliopo ambao ni wafanyakazi wa miaka mingi sana.
Kuna taarifa ambazo waliwahi kuambiwa kwamba mambo yatakuwa mazuri, tena na ule utawala ambao uliondolewa madarakani kwamba watalipwa kila dai la mtu, lakini iliishia kuwa hadithi.
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari tarehe 22/1/2022 alipokuwa kwenye shughuli kuaga miili ya waandishi wa habari waliokufa katika ajali ya gari kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw Robert Gabriel pale Nyamagana alikemea kampuni za habari ambazo haziwalipi waandishi na wafanyakazi wake na akasema ataanza kufuatilia.
Lakini sisi wafanyakazi tunaiona kwa sasa hiyo ni sawa na kauli za wanasiasa kuwalaghai watu ili waonekane kwamba wanawatetea, kumbe sivyo. Tunajiuliza Nape alimaanisha nini kusema vile wakati kampuni ya chama chake haitaki kulipa haki za watu walioifanyia kazi kwa uaminifu wakiwa wanakitetea chama hicho kupitia vyombo vyake.
Jambo jingine linalosikitisha zaidi kwa Nape ni pale alipokemea kwa nguvu suala lile pale Nyamagana, lakini anasahau kwamba wapo wafanyakazi wa Uhuru ambao wameshatangulia mbele za haki muda mrefu, lakini haki zao zimepigwa danadana muda mrefu.
Naandika hili nikimkumbuka mwenzetu Dunia Mzobora ambaye aliwahi kuwa mhariri tena mkubwa tu pale Uhuru, lakini familia yake imesota sana kufuatilia haki zake wakati alifariki dunia muda mchache tu baada ya kutoka kazini (Uhuru).
Yupo pia Hayati Rashid Zahoro ambaye amefariki duniani, lakini pia kuna wastaafu wengi tu ambao wengine baadhi yao waliamua kugoma kuondoka kazini kwa sababu hawajalipa mafao wala hawana uhakika NSSF zao watalipwa lini.
Sio hao tu, bali kuna kundi la wafanyakazi wa zamani ambao waliacha madai yao ya NSSF zao, ila zipo taarifa za uhakika kwamba hazijalipwa mpaka sasa na walishahama siku nyingi wengine miaka zaidi ya minane ila hakuna kinachoendelea kuhusu haki zao.
Napoandika haya nasikitika kwamba CCM chama ambacho kinatamba ni cha kutetea haki za Watanzania bado hakifanyi hivyo kwa watu wanaokitumikia na waliotoa jasho ili kibaki madarakani kupitia uandishi, lakini wana madai ambao yana miaka mingi sana hayajalipwa.
Naamini kwamba Rais Samia Suluhu Hassan, mwenyekiti wa CCM Taifa atalishughulikia hili kama vile ambavyo amekuwa akiwapigania Watanzania katika maisha yao. Na hii nasema kwa ushahidi, na kama hawatalipa basi tuko tayari kuanza kuchapisha mitandaoni madai yetu na nyaraka tulizonazo ili haki zetu zilipwe maana huu ni unyonyaji na unyanyasaji kisaikolojia kwa watu waliokitumikia chama hicho.
USHAURI: Mama anatakiwa asimamie hili. Alipiganie. Akusanye nyaraka zote za maslahi ya wafanyakazi wa chombo hiki waliopo na waliopita kisha afanyie kazi hili. Hakika tumechoka kusubiri haki zetu ambazo ni za kisheria kama NSSF.