D2050
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 1,958
- 1,190
Leo 13/10/2020 nilikuwa crdb banki, wakati tupo kwenye foleni ndani ya hii banki niliwakuta watumishi watatu wa serikali
1) Alikuwa ni mwanamke ambaye ni mwalimu,huyu mama alikuwa analalamika kuwa serikali ndani ya miaka 5 haijawaongezea mshahara hata kidogo,kutokana na ufinyu wa mshahara wake amekuja kukopa crdb akamlipie ada mtoto wake wa chuo.huyu mama kwa sumu aliyokuwa nayo mdomoni pake,kama anaitwa kwa wanawake wenzake wa kazini kwake na anapoishi,hakika CCM mnakazi na hawa watumishi wenu
2) Alikuwa mzee ambaye amestaafu kazi mwaka huu mwezi wa 3 hadi leo analalamika hajapewa pesa yake,huyu mzee anaongea kwa uchungu sana.anasema amelazimika kuja kukopa banki ili ampeleke mwanae chuo. na anawatoto wawili ambao wamemaliza masomo yao ya chuo toka mwaka 2017 hadi leo hawana ajira wapo tu nyumbani.huyu mzee ukimsikiliza vizuri utamwonea huruma.CCM mpo wapi kuwasemea hawa wafanyakazi wa serikali?
3) Alikuwa ni mfanyakazi bado yupo kazini ambaye ni polisi.huyu bwana alikuwa analalamikia mshahara wao mdogo na wao hawajapandishiwa.ila wao hawana uwezo wa kuongea kwa wakubwa wao.
CCM;haya malalamiko ya watu yamekuwa mengi sana,jiangalieni sana