Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mungu si mwanasiasa bali wanasiasa wana miungu. Shetani si mwanasiasa bali wanasiasa wana vishetani vyao.
Siasa ni imani lakini siasa sio dini. Siasa ina wafuasi na dini pia ina wafuasi, lakini si lazima mfuasi wa dini awe mfuasi wa siasa na kinyume chake.
Ni muhimu think tank ya CCM ielimishwe sasa kwakuwa ikizidisha hii michanganyo mwisho itachanganyikiwa, na ikichanganyikiwa inaweza kufanya mambo bila ufahamu kamili. Sijui ni hofu ama ni nini, lakini dalili zinaonesha wazi CCM imejawa hofu.
Hofu huleta woga
Hofu huondoa ujasiri
Hofu huleta taharuki
Hofu huondoa ufahamu
Kila jambo ni mchakato na kila mchakato una formula zake, wabobezi wa kemia wanalijua hili vema. Ukikosea formula huwezi kupata matokeo tarajiwa.
Usijaribu kumchanganya Mungu na shetani ..hizi ni falme mbili kinzani..japo ufalme wa Mungu ni mkubwa kuliko ufalme wa shetani. Kuna namna ya kuenenda na shetani na kuna namna ya kuenenda na Mungu; hupaswi kuzichanganya hizi falme mbili kwenye jambo moja.
Ndani ya wiki moja CCM imezichanganya falme mbili, matokeo yamekuwa hasi. Lilianza kitu kinachoitwa 'tamasha la wasanii' wasiopungua 200, wote tulishuhudia ufalme wa giza ulivyosujudiwa pale. Shetani alipewa airtime ya kutosha kabisa.
Siku chache baadae likaja kitu kinaitwa 'kongamano la amani' wahusika walikuwa ni viongozi wa dini mbalimbali walionona kweli kweli, wakajaribu kuusimika ufalme wa Mungu pale.
Mwaka uliopita lilijitokeza kundi la watu mia moja taslimu waliojiita waganga wa kienyeji mashuhuri Tanzania, wakatoa onyo na kupiga mikwara yao.
Think tank ama kitengo cha propaganda, kilitakiwa kufanya nini ili kisiharibu taswira ya chama mbele ya wananchi?
Wale watu mia moja taslimu hawakupaswa kupewa jina la WAGANGA WA KIENYEJI, walau basi wangeitwa wazee wa mila. Lakini je, ni kweli kabisa uganga wa kienyeji unafanya kazi kwa jinsi ile? Jibu ni HAPANA. Kwahiyo basi kule kulikuwa ndiyo mwanzo wa kuchanganyikiwa.
Hiki kilichokuja kuitwa TAMASHA LA WASANII kingetakiwa kufanya nini?
Ili kuonesha UTU na kujali pamoja na nyimbo zao zile wangetawanywa na kwenda kutoa huduma za kijamii kwa wahitaji na wasiojiweza, wangetawanywa kwenye mahospitali, nyumba za watoto yatima na zile za kulelea wazee wasiojiweza. Ssehemu ya pesa iliyotumika kuwalipa wasanii ingetumika kuwahudumia hawa wahitaji.
Hiki kilichoitwa jana KONGAMANO LA AMANI, badala ya kujikusanya pale kwenye ukumbi wa gharama na kula vinono kwenye AC, walitakiwa wakusanyike sehemu kama uwanja wa taifa na kufanya ibada ya kuliombea Taifa na watu wake wote. Kuombea:
Hivi inaleta picha gani kwa wagonjwa waliolala pale Ocean rd na Muhimbili wakidaiwa pesa za matibabu ambazo hawana uwezo nazo wanakufa wanajiona huku viongozi wao wa kidini kwa sura zilizong'aa na nyuso zilizonona wakikaribishwa kwenye hafla ya kusifu na kuabudu? Badala ya kupendwa ndio kwanza wataanza kutengeneza chuki.
Chama kilifadhili kusanyiko la waganga wa kienyeji 100
Chama kikafadhili tamasha la wasanii 200
Chama kimefadhili kongamano la amani Tanzania la viongozi wa dini- sina idadi yao
Ni jambo jema kwakuwa chama kina miradi mbalimbali, lakini je, hayo ndio matumizi sahihi ya mapato?
Think tank ya CCM inapaswa kujitafakari upya. Maamuzi ya kukurupuka kwa ajili ya hofu yanaweza kuliweka taifa kwenye mtanziko mkubwa.

- Amani ya Taifa
- Mshikamano
- Upendo
- Umoja
- Msamaha na kusameheana
- Ustawi wa Taifa na watu wake n.k, n.k