Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimezindua rasmi kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, ikiwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi huu muhimu. Uzinduzi wa kampeni hizi umefanyika katika kijiji cha Dutwa, Wilaya ya Bariadi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Shamsa Mohammed, alisema kuwa kampeni za uchaguzi zitafanyika kwa njia ya kistarabu, ambapo chama kitawaeleza wananchi kazi ambazo kimefanya na mafanikio yaliopatikana chini ya uongozi wa CCM. Alisisitiza kuwa: "Tunaamini katika uwazi na ufanisi, na kama hatutosema, Miti itasema. Tumetekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo, na wananchi wanapaswa kuona na kuthamini kazi tunayofanya."
Aidha, Ndg. Shamsa Mohammed alieleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kimejizatiti kuhakikisha kuwa uchaguzi huu unakuwa wa amani, haki na umoja, huku lengo kuu likiwa ni kuendeleza maendeleo ya wananchi na kuhakikisha huduma bora kwa kila mkoa, wilaya na kijiji.