CCM mmeteua au mmepinduana?

Wallah nakuapia kuanzia Leo utaona ID mpya sana zikiwa Team Mama na Team Magu! Kuna ID zilizokua ProMagu zitampinga ProSSH.

Mtawatambua kwa maandishi yao na miandiko yao
Sijui MZEE MGAYA atakuwa upande upi!!!?
 
Huyu Dogo ndio kawa DC? Huyu alitakiwa apandishwe kizimbani na yule jambazi mwenzie
Kawa DC Ubungo. Style yake ya kuongea na kuhutubia kama ya Mjomba wake. Hua anatukana na kudhalilisha watumishi wa Halmashauri tena hata watu wazima. Anamaneno ya shobo saaana sana
 
Reactions: BAK
Hawa wahuni na wauaji wamejawa na kiburi utadhani wana hati miliki ya Tanzania kufanya lolote lile watakalo kwa sababu wako juu ya sheria.

Kawa DC Ubungo. Style yake ya kuongea na kuhutubia kama ya Mjomba wake. Hua anatukana na kudhalilisha watumishi wa Halmashauri tena hata watu wazima. Anamaneno ya shobo saaana sana
 
MaCCM yamekaa kujali matumbo yao tu. Mwenyekiti kaamua kufanya mabadiliko anaanza kutishwa! Kwani huo ukatibu mliambiwa ni kazi ya kudumu?

Mwingine roho imemuuma mpaka kaanzisha Uongozi Institute isiyo rasmi.
 
Haya mambo aliyaanzisha Hayati, yani alikifanya chamakama cha kwake akaanza kuteua watu wake wengine hata hawakuwa wanachama wazoefu. Wazee wa CCM wakawa hawana chao sasa umegeuka utaratibu. Yani mtu ambaye hajawahi kuwa na uzoefu na uongozi wa chama anaweza kula shavu akaachwa mkongwe. Sasa hivi steve nyerere ana maana kuliko hata Nape.
 
Miongoni mwa viongozi walioandaliwa ni jambazi Sabaya
 
Uteuzi uliofanyika ni mzuri sana! CCM halisi imerudi kazini, CCM MPYA ya Magufuli na akina Bashiru, Polepole n.k imekufa rasmi!
 
Wenye chama tulisha jikatia tamaa, karibu viongozi wote chamani ni toka serikalini.
Chingolo, Shaka wako kiserikali zaidi.
Kauli mbiu hakuna, zaidi ya kazi iendelee, yaani living in the shadows ofMagufuli.

Itachukua muda kupata viongozi wa chama.
 
Nani alikuambia CCM wanaogopa kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge? hata wakifukuza viongozi wote kuanzia wenyeviti wa matawi mpaka mwenyekiti wa Taifa watashinda jwa kiwango wanachotaka.

Kwa kifupi uchaguzi mkuu uko kwenye kurasa za katiba s kwenye uhalisia na matendo. Ilimradi polisi wapo na wakurugenzi CCM itashindwaje kubeba masanduku ya kura na kutokomea nayo na kisha kuyajaza kura zao kwa viwango watakavyo kisha wakajitangaza washindi.

Wanachofanya CCM kwa sasa si uteuzi ila ni kutengenezeana utaratibu wa kugawana ulaji kichama.
 
Wallah nakuapia kuanzia Leo utaona ID mpya sana zikiwa Team Mama na Team Magu! Kuna ID zilizokua ProMagu zitampinga ProSSH.

Mtawatambua kwa maandishi yao na miandiko yao
Ina maana hawajui kuandika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…