Bila kupepesa macho, ni dhahiri kuwa kadiri muda unavyokwenda idadi ya wapinzani wa CCM inaongezeka. Si rahisi wahusika kukubali hili lakini kuukataa ukweli ni kujitoa ufahamu.
Baba wa taifa alionao ujio wa vyama vingi, wana CCM walitaka kung'ang'ania eti kibaki chama kimoja. Busara za mwalimu zikanusuru bomu lililokwisha anza kujiunda la akina Mabere Marando, Prince Bagenda, Mapalala na wengine la madai ya uwepo wa vyama vingi.
Bahati mbaya ya wakati huu, pamoja na CCM kuona wimbi la watu kutaka mabadiliko ya utawala, iwe kwa kutumia katiba mpya au chama kingine, na wanaona dhahiri kuwa idadi yao inapungua wakati ya wapinzani inapanda hakuna anayethubutu kukubali hayo. Habari hii hawataki kuisikia. Wanajikita kwenye maigizo. Kusoma watu usiku kucha kwenda kwenye mikutano ya kampeni. Wanasema wana takwimu sahihi za wanachama wao, kuwa sasa wamefika milioni 16.
Wanategemea wasanii kuvuta watu kwenye mikutano mithili ya sumaku ya kuvuta chembechembe za vyuma bila kujali waliokuja hapo wanataka nini. Wamekalia propaganda kama za Tariq Aziz wa Iraq aliyekuwa akitoa taarifa za vita ya operation desert Storm. Oooohhh tumemkomesha mmarekani, tumewauwa wote, wakati nchi yake inaendelea kutekwa na miundombinu kuharibiwa.
Ushauri wangu kwa CCM, tuvue miwani ya mbao, tuvae miwani ya darubini inayoona mbali, sijui mnaita binoculars, sijui kiona mbali.
1) Tukubaliane kuwa utawala wa milele kwa CCM haupo!
2). Tukubaliane kuwa katiba hii ya sasa haitufai!
3). Tukubali kusimamia au kuratibu mabadiliko ya katiba na kuweka utaratibu wa kistaarabu na wa kisasa wa kupokezana madaraka kutoka chama kimoja kwenda kingine wakati nchi ikiwa bado ina amani, ni tulivu, ikiwa watu bado wana kauvumilivu ambako kwangu mimi naona kanazidi kuishiria.
4). Tukubaliane kuwa tukitaka tuendelee kwa utaratibu uleule wa kumaliza uchaguzi, kwa kuchaguliwa au kulazimisha ushindi, tujue kuwa tukizuia tena shughuli za vyama tunazidi kuunda bomu la nyuklia. Watanzania wanakuwa wakimya lakini wana lao jambo. Vijana watazidi kujidhatiti, nguvu yao ya 2025 itakuwa kubwa zaidi. Tukitaka kuwadhibiti kuanzia 2020 hadi 2025 itabidi tutumie nguvu zaidi ya tuliyotumia kuwadhibiti kuanzia 2016. Lakini tujue kwa sasa dunia inatumulika. Je tutaweza kuwaziba midomo kama tulivyofanya hapo nyuma?
Tukisema tuwaache waendelee na siasa zao wakati kuna walioenguliwa kwa mizengwe, kuna ambao walishinda lakini hawakutangazwa, mahakama zimejaa kesi za uchaguzi. Huko Zanzibar nako sijui mambo yako sawa kiasi gani, hayo maendeleo tunayoahidi kuwapa wananchi na miradi mikubwa tuanayoendelea nayo tutaweza? Zingatia kuwa uchaguzi ukiwa na kasoro, huenda wahisani wakazuia mikopo, au misaada yao. Elimu bure itaendelea? Vitambulisho ndio hivyo vimepigwa pini na Lisu, wafanyabishara tumeishawakamua vya kutosha.
Tufanye nini sasa?
Baadhi ya majibu:
1). Hoja za zomea zomea, vijembe, kejeli baada ya uchaguzi hasa CCM dhidi ya wapinzani zikome kabisaa!
2). Mahakama ziachwe huru zifanye kazi zake
3). Kuwepo Baraza maalum la maridhiano lenye lengo la kurudisha umoja wa kitaifa. Baraza kuhusishwa viongozi wa dini, viongozi wastaafu desig ya Warioba siyo akina Makamba, Wanasheria waadilifu, viongozi wa vyama vya siasa, NGOs, ili kuweka utaratibu wa kujenga daraja la serikali na vyama vya siasa. Kufuta uhasama unaoanza kuota mapembe.
4). Bunge kama chombo cha wananchi tukiache kifanye kazi yake. Bunge liwe live kama awali.
5). Ishinde CCM au Chama kingine CUF, CHADEMA, ACT Tukubaliane kuwa rasimu ya katiba mpya ya jaji Warioba iwekwe mezani. Tusameheane kwa yaliyopita. HIYOHIYO RASIMU YA KATIBA IPIGIWE KURA, maana tukisema tuanze kuijadili tutarudi kulekule ee kwa akina Avemalia Semakafu na akina Amon Mpanju. Sasa sijui tutasubiri hija tena ili mahujaji wapigekura wakiwa wanarushiana mawe kumpiga shetani? Bahati mbaya mtaalamu wa kura za hivyo hatunaye tena, Mzee Sita (Mungu amuweke anapostahili).
6). Ikishinda CCM, JPM punguza ugumu wa misimamo yako dhidi ya wapinzani. Hii habari ya maendeleo hayana vyama huku Polepole wanaonunua wa vyama vingine ni siasa za kitoto, hazina impact yeyote katika kushawishi au kuvuta wanachama. Ikiwezekana wapoze wapinzani wapate nafasi katika baraza la mawaziri na usiwashawishi wahame vyama vyao, jaribu kujenga umoja.
KWELI KABISA NAWAAMBIA CCM MKISUBIRI WAPINZANI WAFIKE IDADI MNAYOTAKA MTAKUWA MMEISHA CHELEWA, waingereza wanasema THINGS WILL BE BEYOND YOUR CONTROL! Hapo mtalazimika kutumia nguvu ya ajabu kuzima wimbi, maana mikono haitaweza. Na hapo huenda mkatafuta mashimo ya panya kujificha kama ilivyokuwa kwa Gadaffi!
Nawasilisha!