02 February 2023
Tunduma, Tanzania
CCM WAWASHA MITAMBO, WARUSHA "MAKOMBORA' KWA WALICHOKIITA CHAMA CHA UPANDE WA PILI
Wanachama wa CCM jimbo la Momba wamejitokeza kwa wingi barabarani kufanya shughuli za kisiasa kujibu walichoita mapigo upande wa pili walioanza mikutano ya hadhara.
Baada ya Kikao cha ndani wameenda kufanya kikao cha nje kuadhimisha miaka 46 toka kuzaliwa CCM tarehe 5 February 1977 na kujadili mafanikio waliyoita makubwa ingawa upande wa pili ambao hawajautaja hawaamini kuwa yapo.
Walipopanda jukwaani Viongozi wa CCM wazungumzia hotuba za chama kimoja ambacho hawajakitaja jina kilichofanya mikutano yao kanda za ziwa mikoa ya Mwanza, Simiyu na Mara wakiongozwa na kiongozi mmoja mkuu na mwingine aliyerudi kutoa nje ya nchi.
Viongozi wa CCM wakihutubia wanachama na wapenzi wa CCM Tunduma kwamba upande pili wanaona mazuri na makubwa lakini wanabeza tu na hawakubaliani na mengi lukuki mazuri yanayoonekana.
Viongozi hao wa CCM wasema nchi ni ya raha mustarehe na kushangaa watu kukimbilia kukipenda na kukishabikia chama cha upande wa pili kisicho kuwa na serikali.
Source : Jay TV Tanzania