CCM: Mpuuzeni Butiku! Zuio la CHADEMA kutokufanya siasa linatoka Mahakamani, sio Serikalini

CCM: Mpuuzeni Butiku! Zuio la CHADEMA kutokufanya siasa linatoka Mahakamani, sio Serikalini

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefafanua kuwa kuzuiwa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli zake za kisiasa hakutokani na uamuzi wa CCM wala Serikali, bali ni maagizo ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Januari 21, 2026, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi amesema kuwa zuio hilo linatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu katika shauri la maombi madogo namba 8960 la mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shauri hilo lilifunguliwa na wanachama wa CHADEMA akiwemo Said Issa Mohammed, Ahmed Rashid Khamis maarufu “Ana Komu”, wakiiomba Mahakama iamuru chama hicho kisifanye shughuli zozote za kisiasa wala kutumia mali za chama hadi pale mgogoro wa ndani unaoendelea utakapopatiwa ufumbuzi wa kisheria.

Kihongosi amesema Mahakama Kuu ilisikiliza maombi hayo na kutoa zuio la muda hadi shauri la msingi namba 8323 la mwaka 2025 litakapomalizika kusikilizwa na kuamuliwa.

Amesisitiza kuwa CCM haina mamlaka wala sababu ya kuzuia shughuli za CHADEMA, akibainisha kuwa masuala yote yanayohusu zuio hilo yako mikononi mwa Mahakama, na kwamba chama chake kinaheshimu misingi ya utawala wa sheria na maamuzi ya mhimili wa Mahakama.

Katika wito wake kwa Watanzania, Kihongosi amewataka wananchi na wadau wa siasa kuacha kutoa tafsiri potofu au lawama zisizo na msingi, na badala yake waheshimu maamuzi ya Mahakama kama chombo halali cha kutoa haki nchini.

Pia Soma: Butiku amshukia mwenezi CCM: 'Ziara ya hovyo', Agusia sakata la CHADEMA
1768990883422.png


1768990904823.png
 

Attachments

  • 1768989206535.png
    1768989206535.png
    915.6 KB · Views: 55
Mifumo yote nchi hii kuna mstari mwembamba sana kuitenganisha na ccm
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefafanua kuwa kuzuiwa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli zake za kisiasa hakutokani na uamuzi wa CCM wala Serikali, bali ni maagizo ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Januari 21, 2026, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi amesema kuwa zuio hilo linatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu katika shauri la maombi madogo namba 8960 la mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shauri hilo lilifunguliwa na wanachama wa CHADEMA akiwemo Said Issa Mohammed, Ahmed Rashid Khamis maarufu “Ana Komu”, wakiiomba Mahakama iamuru chama hicho kisifanye shughuli zozote za kisiasa wala kutumia mali za chama hadi pale mgogoro wa ndani unaoendelea utakapopatiwa ufumbuzi wa kisheria.

Kihongosi amesema Mahakama Kuu ilisikiliza maombi hayo na kutoa zuio la muda hadi shauri la msingi namba 8323 la mwaka 2025 litakapomalizika kusikilizwa na kuamuliwa.

Amesisitiza kuwa CCM haina mamlaka wala sababu ya kuzuia shughuli za CHADEMA, akibainisha kuwa masuala yote yanayohusu zuio hilo yako mikononi mwa Mahakama, na kwamba chama chake kinaheshimu misingi ya utawala wa sheria na maamuzi ya mhimili wa Mahakama.

Katika wito wake kwa Watanzania, Kihongosi amewataka wananchi na wadau wa siasa kuacha kutoa tafsiri potofu au lawama zisizo na msingi, na badala yake waheshimu maamuzi ya Mahakama kama chombo halali cha kutoa haki nchini.
 
Kama ndivyo mnahangaika kusaka maridhiano ya nini na nani? Kwanini msiachane na upuuzi huo unaoitwa 'maridhiano" ili kuipa Mahakama nafasi na uhuru wa kuamua shauri lile?

Kesi ya ugaidi ya Mh Mbowe iliyokuwa ikiendelea Mahakamani iliamuliwa Mahakamani au Ikulu??

CCM ijitafakari kwa nafasi zake za uongozi kwani wakati mwingine wanapewa watu nafasi ambozo hawana uwezo nazo.

Angalia suala la Mh Jaji Warioba aliyeshiriki kuasisiwa kwa CCM eti anakwenda kufundishwa miiko ya CCM na mtu ambae amezisoma na kuzikariri vibaya miiko ile.

Ifike mahali kama Siasa za Vyama vingi vimekuwa mzigo kwa CCM isiyoweza ushindani wa kisera, basi pelekeni Hoja Bungeni kuirejesha nchi kwenye mfumo wa chama kimoja cha Siasa. Acheni kuwapotezea watu muda huku mkiwaona ni maadui kwenye taifa lao, kisa kutimiza wajibu wao wa shughuli za kisiasa ambazo zipo kisheria.
 
Huyu Kikaragosi ni bogus kabisa!! Yaani anadhani watu wana akili ndogo kama ya kwake. Watu wana habari za ndani ya CCM, ndani ya Tume mchongo ya uchaguzi, ndani ya ofisi mchongo ya msajili wa vyama, Serikali na mahakama mchongo, jinsi kwa pamoja walivyotekeleza huo uharamia.

CCM iliitaka Serikali itafute kila mbinu ya kuizuia CHADEMA isishiriki uchaguzi. Jukumu hilo la kwanza ilipewa ile tume mchongo ya uchaguzi. Wakakubaliana watengeneze mazingira ambayo CHADEMA haitakubali kushiriki uchaguzi kwa mazingira hayo. Cha kwanza walichokifanya ni kutengeneza kanuni mbaya kuliko kipindi chochote. Wakaamua ule utaratibu wa mawakala kupewa nakala ya matokeo wafutwe, na watu wasiruhusiwe hata kupiga picha ile karatasi ya majumuisho ya kura kwenye kituo. Kama walivyopanga, CHADEMA wakagomea kusaini hizo kanuni za kishetani. Baada ya kutokusaini, tume ile ovu ya uchaguzi, haraka ikatangaza kuwa CHADEMA haitashiriki uchaguzi. Wakajua wamemaliza kazi. CHADEMA walipoendelea kufanya mikutano ya NRNE, CCM wakalalamika baada ya kuona mwitikio mkubwa wa wananchi. CCM na Samyua wao wakaagiza Lisu akamatwe mpaka uchaguzi upite, wakijua bila Lisu, mikutano hiyo haitakuwa na nguvu. Wakamkamata Lisu. Lisu akiwa ndani, mikutano ikaendelea ikiwa na uungwaji mkono mkubwa wa wananchi. Ndipo CCM ikamwagiza msajili wa vyama ahakikishe CHADEMA haiendelei na mikutano. Msajili akatoa tamko kuwa kamati kuu yote ya CHADEMA ni batili, katibu mkuu na wasaidizi wake ni batili, akijua kuwa Heche pekee asingeweza kuendelea na mikutano. Ilipoonekana mbinu hiyo haijafanikiwa, ndipo wakaamua kutumia pesa na mahakama kupitia majaji mchongo. Wakapatikana waroho wa pesa kutoka kundi lililowekwa pembeni kwenye uongozi wa CHADEMA. Awali ilikuwa kundi hilo lijiunge na CHAUMMA, lakini baadaye wakaelekezwa wasiondoke ili watumiwe katika kufungua kesi bandia ambayo jaji mchongo tayari alikuwa ameandaliwa, na hukumu imeandaliwa.

Kwa ujumla yote yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa dhidi ya CHADEMA, ni matakwa ya CCM na Samuya na genge lake la waovu, waporaji wa rasilimali za Tanganyika. Halafu hivi vikaragosi, kama Kohngos, vinatumika kwa sababu ya uchu wa pesa. Lakini huko mbeleni vikaragosi kama hivi vitakuja kujuta kwa kushirikiana na waovu dhidi ya Tanganyika yao, maana hakuna atakayetamani kuwasikia wala kuwaona.
 
Alimsikiliza Jaji Mkuu? Mahakama haipo huru sababu watendaji wake hawana mishahara minono!
 
Kwamba hajui kuwa Butiku anajua nani anaagiza mahakama iwakomoe cdm? Anadhani hayo ni mambo mapya kufanywa na ccm, hivyo hajui kuna wanaccm wengi wanajua kipi kinafanyika nyuma ya pazia?
 
Hiki chama Cha CCM kinazidi kudidimiza taifa shimoni. Nani mwenye akili timamu asiyetambua mchoro mzima hadi uamuzi wa mahakama una baraka zote za CCM!

Kihongosi is such useless individual
 
Huyu mpumbavu anadhani Watanzania sie ni wapumbavu kama walivyo huko ccm?

Nani hajui kuwa Mahakama hizi za kipumbavu haziko huru tena na zinafanya kazi kwa kuangalia maslahi ya ccm na wanaccm badala ya Haki na Taifa?
 
Kama ndivyo mnahangaika kusaka maridhiano ya nini na nani? Kwanini msiachane na upuuzi huo unaoitwa 'maridhiano" ili kuipa Mahakama nafasi na uhuru wa kuamua shauri lile?

Kesi ya ugaidi ya Mh Mbowe iliyokuwa ikiendelea Mahakamani iliamuliwa Mahakamani au Ikulu??

CCM ijitafakari kwa nafasi zake za uongozi kwani wakati mwingine wanapewa watu nafasi ambozo hawana uwezo nazo.

Angalia suala la Mh Jaji Warioba aliyeshiriki kuasisiwa kwa CCM eti anakwenda kufundishwa miiko ya CCM na mtu ambae amezisoma na kuzikariri vibaya miiko ile.

Ifike mahali kama Siasa za Vyama vingi vimekuwa mzigo kwa CCM isiyoweza ushindani wa kisera, basi pelekeni Hoja Bungeni kuirejesha nchi kwenye mfumo wa chama kimoja cha Siasa. Acheni kuwapotezea watu muda huku mkiwaona ni maadui kwenye taifa lao, kisa kutimiza wajibu wao wa shughuli za kisiasa ambazo zipo kisheria.
Yaani nacheka Mimi BABU yenu, aliyeandika Katiba na Asiyeijuwa wala kuisoma katiba ya CCM.
 
Back
Top Bottom