CCM mpya mwacheni Rais Samia afanye yake, huyu ni Rais wa nchi sio wa CCM. Mlivyolivuruga Taifa inatosha, ni muda wa nchi kufufuka

CCM mpya mwacheni Rais Samia afanye yake, huyu ni Rais wa nchi sio wa CCM. Mlivyolivuruga Taifa inatosha, ni muda wa nchi kufufuka

Vugu-Vugu

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
1,430
Reaction score
1,637
Wanajamvi Salaam,

Tangu mama Samia apokee Kijiti cha kuwa Rais wa JMT.

Binafsi sijawahi kuandika chochote humu ama kumpongeza ama kumkosoa Ila kwa yanayoendelea sasa,Sisi Wazalendo halisia kamwe hatuwezi kukaa kimya tena Lazima tuwajibu hawa waliojiita eti Wazalendo kwa kutafuna nchi.

Leo naanza kwa kutoa ushauri kwa Wana-CCM waliokosa vyeo/wenye hofu ya kukosa vyeo na wote wanaomshambulia mama kwenye Mitandao ya Kijamii kila Uchapo waache maramoja Kwani anachokifanya Samia dunia imemwelewa na Sisi Wazalendo asilia tumemwelewa Sana na 2025 ni "Tano tena " kwake.

Kwanza, Hebu mnijibu maswali yafuatayo kabla ya kumlaumu Mama Samia:-

1. Nimemsikia mama akiwaonya TRA kuacha maramoja kutumia mtindo wa presumptive Tax assessment na mitutu ya bunduki katika kudai kodi badala yake ifanyike grooming ya wafanyabiashara wapya ili tutoke kwenye walipakodi 2.7M walau tufike walipakodi 4M.

Je, hili ndilo linawafanya mumshambulie mama yetu kila uchapo au furaha yenu ni watu kufunga biashara na kutimkia nchi za jirani? Au ndio hivyo mlizoea kuwatisha kisha kuwanyang'anya pesa zao!


2. Nimemsikia mama anataka kukutana na Wapinzani wote ili kumaliza tofauti zilizoasisiwa na mtangulizi wake ili tuwe na Taifa lenye "Amani na Utulivu wa kweli " hivi kweli hili ndilo linawafanya mumnyanyase mama kiasi hiki?

Kwanini mmerithi moyo wa kikatili kiasi hiki? Nikweli ninyi mnafurahia namna bunge letu lilivyo leo? Yaani hakuna hata mtu wa kumuuliza Waziri mkuu maswali as if shida za watanzania zimekwisha,Kweli hiki ndicho kinachowavutia ninyi kiasi cha kukereka na mama?

Nitaendelea baadae na mada hii
 
Tatizo ni Jiwe kuweka ukoo wake kwenye ngazi kubwakubwa za taifa. Wanamhujumu mama chinichini
 
Mkuu kwa mwandiko huu, bila shaka ulisomea chini ya muembe
 
Mama pia ampe Januari Makamba Uwaziri Mkuu ili awasafishe wale wote ambao bado wanaUmagufuli kwenye Serikali ya Nchi yetu Tukufu
Majaliwa hana shida na wala hajawai kuwa na shida yeyote yeye ufanya kutokana na maagizo anayopewa. January kiburi kingi sana ingawa ni kiongozi mzuri.
 
Wanajamvi Salaam,

Tangu mama Samia apokee Kijiti cha kuwa Rais wa JMT, Sijawahi kuandika chochote humu kumpongeza ama kumkosoa Ila kwa sasa hatuwezi kukaa kimya tena kwa namna anavyoshambuliwa kila kona na Wana-CCM wenzake ,Eti kisa ni yeye kuwa na hofu ya kweli kwa Mungu kwa kutenda yale tu yampasayo Mungu na Wanadamu.

Leo naanza kwa kutoa ushauri kwa Wana-CCM waliokosa vyeo/wenye hofu ya kukosa vyeo na wote wanaomshambulia mama kwenye Mitandao ya Kijamii kila Uchapo.

Kwanza, Hebu mnijibu maswali yafuatayo kabla ya kumlaumu Mama Samia :-

1. Nimemsikia mama akiwaonya TRA kuacha maramoja kutumia mtindo wa presumptive Tax assessment na mitutu ya bunduki katika kudai kodi badala yake ifanyike grooming ya wafanyabiashara wapya ili tutoke kwenye walipakodi 2.7M walau tufike walipakodi 4M.
Je hili ndilo linawafanya mumshambulie mama yetu kila uchapo au furaha yenu ni watu kufunga biashara na kutimkia nchi za jirani ?au ndio hivyo mlizoea kuwatisha kisha kuwanyang'anya pesa zao!!.


2. Nimemsikia mama anataka kukutana na Wapinzani wote ili kumaliza tofauti zilizoasisiwa na mtangulizi wake ili tuwe na Taifa lenye "Amani na Utulivu wa kweli " hivi kweli hili ndilo linawafanya mumnyanyase mama kiasi hiki?! Kwanini mmerithi moyo wa kikatili kiasi hiki? Nikweli ninyi mnafurahia namna bunge letu lilivyo leo? Yaani hakuna hata mtu wa kumuuliza Waziri mkuu maswali as if shida za watanzania zimekwisha,Kweli hiki ndicho kinachowavutia ninyi kiasi cha kukereka na mama?!!

Nitaendelea baadae na mada hii,
Crap
 
Sisiemu ni ileile tu, ndiyo maana kila anayekuja anafanya yaleyale na kumlaumu aliyepita, hata Sa100 akiondoka atalaumiwa tu
 
Mama Samia kunguni na viroboto wapo hadi hapo Lumumba, safisha safisha mama nyumba iwe safi.
 
Back
Top Bottom