CCM msituletee tena viongozi kama Awamu ya Tano

CCM msituletee tena viongozi kama Awamu ya Tano

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Aina ya uongozi kama ule wa Awamu ya Tano ulikuwa balaa kwa mustakabali wa umoja wa nchi yetu.

Sina haja ya kurudia madhambi mabaya ya Awamu ya Tano maana kila mtu yalimgusa.

Kiini cha hayo matatizo ni kinyang'anyiro cha urais wa 2015 ambapo walijitokeza wagombea zaidi ya 40.

Naona hili linajirudia mbio za Uspika.

CCM waliboronga vibaya mwaka 2015, na matokeo tuliyaona.

Sasa hivi CCM iwe makini na waache umavikundi, mitandao, na "gangs" za kimasilahi binafsi.
 
Makundi huko CCM yaliasisiwa tangu enzi za Kikwete, wanaofuata wanaendeleza tu hiyo tabia, na pale ambapo viongozi wanajua wanachaguliwa ili wakale kwa urefu wa kamba zao lazima wachague kundi lenye nguvu ili wakatimize malengo yao.
 
Wengi wao walipewa teuzi na vyeo kama fadhila ya uchawa ulilipa Sana awamu ile ilikuhitaji dakika 5 kumsifia jiwe Ili kesho uletewe v8 na barua ya uteuzi Bashe, Mwigulu, Mollel, Waitara, Chalamila, Hapi, Kihongosi, Gambo, Sabaya, Ndugai, Tulia, Mnyeti, Mtatiro, Kange, Byakanwa, nk wote hawa hawakupewa nafasi sababu ya weledi wao bali ni kucheza na media wakimtukuza jiwe.

Ilikuwa ukimsifia au ukitishia kumuua, kudhalilisha, kuwafunga wapinzani teuzi cheo umepata hapa tumeona mahakimu wengi sana wamelamba ujaji kwa kuwafunga tu wapinzani inatakiwa wavuliwe ujaji awamu awajaupata kwa uweledi basi kwa kuukandamiza upinzani, tuliona mapolice wakiwa bize kuwakamata na kuwafurumushia mabomu wapinzani bila weledi Ili tu kumfurahisha jiwe wapewe vyeo.

Lakini Mungu ajatuacha yatima.
 
Makundi huko CCM yaliasisiwa tangu enzi za Kikwete, wanaofuata wanaendeleza tu hiyo tabia, na pale ambapo viongozi wanajua wanachaguliwa ili wakale kwa urefu wa kamba zao lazima wachague kundi lenye nguvu ili wakatimize malengo yao.

Na kwakuwa baadhi ya watendaji wa Kikwete bado wapo mpaka awamu hii, basi nategemea makundi yaendelee kuwepo ili wajitengenezee njia ya kula kuelekea 2025.
Turudi katika kuasisi sera zinazo waondolea wananchi matatizo yao ikiwa ni pamoja na maendeleo.

Kikwete anabeba lawama zake kwa kuanzisha umakundi ya maslahi, mtandao, ndani ya chama.

Matokeo yake tumeyaona.
Mwalimu alsema TUJISAHIHISHE.
 
CCM inabidi muangalie upya mfumo wenu wa kupata viongozi kosa mlilotufanyia 2015 linaweza jirudia Tena .Inaonekana kwenye kiti Cha spika Kuna linyang'au jingine kama jiwe linaenda kuuokota uspika .
Na huo ndo wasi wasi wangu pia.
Maslahi mapana ya nchi, CCM lazima iyazingatie.
 
Back
Top Bottom