Uchaguzi 2020 CCM mtapata kura za watumishi wa TRA na BOT na familia zao tu, ambao mliwapandishia mishahara kwa zaidi ya 300%

Walimu ni zaidi ya 70% ya watumishi wote, wanafuata watu wa afya zaidi ya 20%. Hawa wote waalimu, madaktari, wauguzi, manesi, hawana umuhimu kwa Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5 ya wanyonge, TRA na BOT tu ndio wa muhimu. Watampigia kura.
Lakini tra ni wa muhimu sana,wao ndo wanakusanya hela,
Bot wao ndo wanatunza hela,ni watu muhimu sana hawa,ba polisi pia na wanajeshi
 
Dogo,

Nina ndugu yangu yuko TRA. Ni kweli walipandishwa mishahara kiasi chake lakini uhalisia dogo TRA walikuwa hawajapandishwa mishahara karibu miaka 6.

Na hii imechelewa sana lakini walitakiwa kupandishwa level hii ya leo miaka 12 iliyopita. Najua hujui ila nakupa tu hii taarifa.
Halafu dogo tukienda na uhalisia TRA wanastahili kupewa zaidi ya wanachopata sasa. Linganisha mshahara wa afisa wa Tanzania Revenue Authority (TRA) na Kenya Revenue Authority (KRA) na allowances zao utaniambia. Ni kama wanaishi dunia mbili tofauti wakati ni nchi jirani tu.

Tena ungejua TRA walivyokanyagwa kwa muda mrefu kwenye mishahara usingewaandika hapa. Anyway, labda huna information na sikulaumu kwa hilo.
 
Toka serikali ya awamu ya 5 imengia watumishi wa umma zaidi ya laki 5 hawakuwahi kupandishiwa mishahara wala madaraja lakini kuna kundi la watumishi wachache sana nchi hii wameneemeka na serikali ya awamu ya 5, watumishi hao ni wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania.

Serikali ya awamu ya 5 kwa sababu zisizoeleweka ikaamua kuwapandishia mishahara watumishi wa TRA na BOT kwa zaidi ya 300% huku ikiacha zaidi ya 98% ya watumishi wengine wa umma kwenye lindi la ufukara na njaa kwa mishahara midogo waliyoipata miaka 6 iliyopita.

Serikali ya awamu ya 5 imewagawa watumishi wa umma, kuna wegine wanaonekana wa muhimu na wengine hawana umuhimu. Kwa mtazamo wa serikali ya wamyonge watumishi wa TRA na BOT ndio wa muhimu lakini watumishi wengine wote sio wa muhimu.

Mtumishi wa elimu ngazi ya stashahada wa TRA analipwa mara 2 ya mtumishi mwenye shahada 2 wizarani ama kwenye taasisi nyingine za umma.

CCM waombeni wafanyakazi wa TRA na BOT wawapigie kura, hawa wengine ambao mmeona sio wa muhimu watampigia Lissu ambae ameahidi kuwapandishia mishahara muda mfupi baada ya kuapishwa.

Mnasema hii nchi ni tajiri halafu mnashindwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi? Ngoja wanaojua utajiri wa hii nchi waingie waboreshe maisha ya watanzania ambao mmewafukarisha kwa miaka 60.
UMENENA KWELI MKUU.MIMI KAJAMBA NANI KURA YANGU KWA LISSU
 
TRA hata kama utawanyima mshahara kwa mwaka mzima basi hawato miss kwenda kazini.
 
Toka serikali ya awamu ya 5 imengia watumishi wa umma zaidi ya laki 5 hawakuwahi kupandishiwa mishahara wala madaraja lakini kuna kundi la watumishi wachache sana nchi hii wameneemeka na serikali ya awamu ya 5, watumishi hao ni wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania.

Serikali ya awamu ya 5 kwa sababu zisizoeleweka ikaamua kuwapandishia mishahara watumishi wa TRA na BOT kwa zaidi ya 300% huku ikiacha zaidi ya 98% ya watumishi wengine wa umma kwenye lindi la ufukara na njaa kwa mishahara midogo waliyoipata miaka 6 iliyopita.

Serikali ya awamu ya 5 imewagawa watumishi wa umma, kuna wegine wanaonekana wa muhimu na wengine hawana umuhimu. Kwa mtazamo wa serikali ya wamyonge watumishi wa TRA na BOT ndio wa muhimu lakini watumishi wengine wote sio wa muhimu.

Mtumishi wa elimu ngazi ya stashahada wa TRA analipwa mara 2 ya mtumishi mwenye shahada 2 wizarani ama kwenye taasisi nyingine za umma.

CCM waombeni wafanyakazi wa TRA na BOT wawapigie kura, hawa wengine ambao mmeona sio wa muhimu watampigia Lissu ambae ameahidi kuwapandishia mishahara muda mfupi baada ya kuapishwa.

Mnasema hii nchi ni tajiri halafu mnashindwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi? Ngoja wanaojua utajiri wa hii nchi waingie waboreshe maisha ya watanzania ambao mmewafukarisha kwa miaka 60.
Nashindwa kusaidia nyumbani maana hali tete naishi kwa salary advance kila mwezi mwaka wa 7 sijapanda daraja
 
Back
Top Bottom