Uchaguzi 2020 CCM mtapata kura za watumishi wa TRA na BOT na familia zao tu, ambao mliwapandishia mishahara kwa zaidi ya 300%

Walimu ni zaidi ya 70% ya watumishi wote, wanafuata watu wa afya zaidi ya 20%. Hawa wote waalimu, madaktari, wauguzi, manesi, hawana umuhimu kwa Magufuli na serikali yake ya awamu ya 5 ya wanyonge, TRA na BOT tu ndio wa muhimu. Watampigia kura.
Lakini tra ni wa muhimu sana,wao ndo wanakusanya hela,
Bot wao ndo wanatunza hela,ni watu muhimu sana hawa,ba polisi pia na wanajeshi
 
Dogo,

Nina ndugu yangu yuko TRA. Ni kweli walipandishwa mishahara kiasi chake lakini uhalisia dogo TRA walikuwa hawajapandishwa mishahara karibu miaka 6.

Na hii imechelewa sana lakini walitakiwa kupandishwa level hii ya leo miaka 12 iliyopita. Najua hujui ila nakupa tu hii taarifa.
Halafu dogo tukienda na uhalisia TRA wanastahili kupewa zaidi ya wanachopata sasa. Linganisha mshahara wa afisa wa Tanzania Revenue Authority (TRA) na Kenya Revenue Authority (KRA) na allowances zao utaniambia. Ni kama wanaishi dunia mbili tofauti wakati ni nchi jirani tu.

Tena ungejua TRA walivyokanyagwa kwa muda mrefu kwenye mishahara usingewaandika hapa. Anyway, labda huna information na sikulaumu kwa hilo.
 
UMENENA KWELI MKUU.MIMI KAJAMBA NANI KURA YANGU KWA LISSU
 
TRA hata kama utawanyima mshahara kwa mwaka mzima basi hawato miss kwenda kazini.
 
Nashindwa kusaidia nyumbani maana hali tete naishi kwa salary advance kila mwezi mwaka wa 7 sijapanda daraja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…