CCM Mwisho wake kuwepo kama chama tawala ni 2020

CCM itashinda hata kwa goli la mkono-Nape Nnauye 2015
Mtoa mada ukishiba ugali ni bora uhesabu nywele zako kuliko kuota ndoto kama hizi.

Nzi wa kijani itachukua miaka mingi sana kutoka madarakani hasa upinzani huu wa Lipumba na wale ambao walimfukuza Zitto Kabwe kisha wakampokea Lowassa.
 
Sasa ndugu uliyeleta uzi, mtu akikwambia corona imeshambulia fahamu zako atakuwa amekosea?

Hapa kwa sasa Mungu ndiye mwamuzi wa haki.

Inawezekana hata ninyi nia yenu si nzuri na huenda kuna watu wabaya sana miongoni mwenu ndio maana tukiomba Mungu anawapa ccm ushindi hata kama ni kwa kuiba kura.
Kipindi Mungu aliamua kuwapa,wasimamizi wa uchaguzi waliingiwa hofu na kutangaza matokeo halisi.

Mungu akiamua bhana hata wafanyeje,watashindwa tu.Unless wewe ni nabii tutakuelewa maana kwa sasa hata dalili tu hakuna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina wasi wasi sana kama ulicho andika umekifanyia utafiti, au ni kujaza maandiko kwenye hii JF ? Mwenye kuelewa siasa za Tanzania kwa ukweli na kwa utafiti unamfanya aanze kujenga wasi wasi na maandiko mengi utakayo shusha hapa hapo baadaye. Jitahidi usimshirikishe mungu kwa maandiko ambayo hujafanya utafiti wa kutosha.
 
Mwambie aliyekutuma kuwa CCM
bado wananchi tunaikubali, Tz 200% ni CCM.
 

..hiyo ni kauli ya Mwalimu akiwalinganisha wagombea Uraisi wa mwaka 1995.

..na leading candidates walikuwa toka upinzani ,Augustino Mrema, ambaye alikuwa hajui KIINGEREZA vs Ben Mkapa, au Jakaya Kikwete, au Cleopa Msuya.

..kwa kuzingatia hali hiyo Mwalimu aliona mgombea bora ni kati ya wale 3 ambao walikuwa CCM.

NB.

..katika uchaguzi huo Mwalimu alisema Tz imepoteza heshima kimataifa hivyo ilihitaji Raisi atakayeweza kutuondoa ktk aibu hiyo.
 
kuna tetesi kwamba Polepole kishanunua nyumba Kigali kishajipanga kukimbilia huko
 
Tundu Lissu 2020 ili tuondokane na utawala huu wa kikabila
 

..swali ni kwanini ccm inatumia mabavu na ukatili kupambana na vyama vya upinzani?

..You would think rekodi ya utekeleza ya ccm itawafanya wajiamini, lakini badala yake wanaogopa wapinzani kuwafikia wananchi kwa namna yoyote ile.
 

Mkuu nimetoka kapa. Tutafuteni suluhu la Corona kwanza wandugu siasa baadaye.

Kuwepo kwetu hai kwanza mengine baadaye.
 
Sijawah kusikia taarifa ya USA kuhusu democrasia ya China... Tumejirahisisha sana
 
Mkuu Gerald Magembe, kwanza asante kwa mchango huu, kama kuna Chadema wenye akili na wamekusoma hapa, wata copy na kuwatumia viongozi wao

Hakuna kitu kigumu na kinachotumia fedha kama research, hapa umewafanyia Chadema research ya bure, wangepaswa wakulipe. Michango kama hii yenye ukweli mchungu ndio itawasaidia wapinzani wa kweli. Numbers don't lie, CCM ina wajumbe wa shina, wale wajumbe wa nyumba kumi, huko ndio grassroots level, baada ya wajumbe wa mashina, wana mashina ya wakereketwa karibu vijiwe vyote ni CCM, wanakuja matawi, wanakua vijiji, kata, wilaya, jimbo, mkoa. Ndani ya ofisi zote za CCM kuna Jumuiya zao tatu za wanawake, vijana na wazazi, wakati kwenye vyama vya upinzani kuna maeneo hakuna hata ofisi moja ya chama chochote cha upinzani wilaya nzima.

Nikawashauri Chadema as the main opposition party, they should invest on people, kwa kutumia modern ways of mass mobilization through mass communications. Fedha zilizotumika kununua yale mandinga makubwa ya M4C zingetosha kabisa kuanzisha redio yake, tv yake, gazeti lake na interactive online forum ili to reach the masses wa grassroot level, wao wameng'ang'ania siasa za kiharakati za mikutano ya siasa na maandamano.

Utamwambia nini mtu anayesomeshewa bure watoto wake, kapatiwa maji, barabara, hospitali na huduma muhimu za jamii?.

Kila ukiwaambia ukweli huu wa 2020 Chadema wanakarika na kutukana hovyo humu mitandaoni.

Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums

Ile 2015 Chadema ilikuwa ichukue nchi, ika bugi tuu step

Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...! - JamiiForums

Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... - JamiiForums

P.
 
Naunga mkono hoja atuna wapinzani tunawachumia tumbo na hizi kelele za tume Uhuru sijui kwenda kuonana Mh Rais ni kwenda kuomba kwenye maigizo ya uchaguzi wa mwaka huu nao wapewe majimbo kadhaa kwa Ajiri matumbo yao...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rubawa, kwanza ni kweli miongoni mwa wapinzani, kuna wapinzani wa kweli, wachumia tumbo na wasaka fursa, baada ya Bunge kuvunjwa wachumia tumbo na wasaka fursa, wote watajitimkia zao, watabaki wapinzani wa kweli tuu, swali linakuja kwa political dynamics za sasa na the political landscape ya Mafulification, jee watatoboa au ndio tunarudishwa mfumo wa chama kimoja?.
P
 
Kwangu ni kheri chama kimoja kuliko huu usanii na maigizo haya tulio nayo mfano mdogo Kuna kauli mbili toka kwa mtu mmoja ndani ya wiki moja Angalia Mahojiano ya Maalim Seif wakt katoka Ikulu kuomba kupewa japo Umakamo wa kwanza Rais Znz mwaka huu hlf siku mbili mbele amefanya mahojiano Global TV angalia tna amesema nn khs Magufuli na serikali yke...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rubawa, kama ni Maalim Seif, please huyo mwache kwasababu uchaguzi wa 2020 kwake ni do or die, hivyo katika maandalizi ya mpambano wa mwisho, atakuwa tayari kwa lolote. Baada ya kuonja ving'ora ile 2010-2015, halafu akavikosa 2015-2020
amejutia makosa yake, hivyo sasa kwa 2020 hawezi kufanya tena makosa, yuko tayari kusema chochote, kufanya chochote ali mradi 2020-2025 ni ving'ora tena.
P
 
Sio yy tu wanasiasa wetu wote ngoja nikupe mfano mwaka fulani nilikuwa Ikulu ya Zanzibar kwenye maongezi na Komandoo akaniuliza hv una fikiria Ukarume unaweza kurudi tna znz siku jibu kitu mwenyewe akasema ilo aliwezekani ila baada muda nasikia alitaka kujiongezea muda madarakani isiwe miaka 10 tna...
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiacha watu wachache ambao kwa sababu zake mwenyewe Mh Magufuli amekubari kuwapa madaraka makubwa kudhurumu kunyanyasa sie wote tunao jaribu kuonyesha mapungufu machache ili km Taifa twende Pamoja. Ila yupo Sawa kwenye mengi Nasimama Nae Mh Magufuli Pamoja Dhuruma zote juu yngu na baadhi unazijua vzuri...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pombe ikizidi haya ndo matokeo take,
Unajiapiza kwa mungu gani?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…