Mkuu Gerald Magembe, kwanza asante kwa mchango huu, kama kuna Chadema wenye akili na wamekusoma hapa, wata copy na kuwatumia viongozi wao
Hakuna kitu kigumu na kinachotumia fedha kama research, hapa umewafanyia Chadema research ya bure, wangepaswa wakulipe. Michango kama hii yenye ukweli mchungu ndio itawasaidia wapinzani wa kweli. Numbers don't lie, CCM ina wajumbe wa shina, wale wajumbe wa nyumba kumi, huko ndio grassroots level, baada ya wajumbe wa mashina, wana mashina ya wakereketwa karibu vijiwe vyote ni CCM, wanakuja matawi, wanakua vijiji, kata, wilaya, jimbo, mkoa. Ndani ya ofisi zote za CCM kuna Jumuiya zao tatu za wanawake, vijana na wazazi, wakati kwenye vyama vya upinzani kuna maeneo hakuna hata ofisi moja ya chama chochote cha upinzani wilaya nzima.
Nikawashauri Chadema as the main opposition party, they should invest on people, kwa kutumia modern ways of mass mobilization through mass communications. Fedha zilizotumika kununua yale mandinga makubwa ya M4C zingetosha kabisa kuanzisha redio yake, tv yake, gazeti lake na interactive online forum ili to reach the masses wa grassroot level, wao wameng'ang'ania siasa za kiharakati za mikutano ya siasa na maandamano.
Utamwambia nini mtu anayesomeshewa bure watoto wake, kapatiwa maji, barabara, hospitali na huduma muhimu za jamii?.
Kila ukiwaambia ukweli huu wa 2020 Chadema wanakarika na kutukana hovyo humu mitandaoni.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums
Ile 2015 Chadema ilikuwa ichukue nchi, ika bugi tuu step
Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...! - JamiiForums
Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... - JamiiForums
P.