CCM Mwisho wake kuwepo kama chama tawala ni 2020

Naona upinzani safari hii watashinda uchaguzi kwa kupigiwa kura na wamarekani. Mimi nashangaa hivi wamarekani nyinyi mnawaona watu sana eeh? Pole sana wale hawanaga marafiki huwaga wazee wa masilahi basi. Mjitathimini
Ni wazee wa maslahi,Ina maana mi macho alienda kuwabebembeleza awape na kuwaongezea migodi ya uranium kule Namtumbo ili wasishinikize jamaa kutoka madarakani kutokana na kuonesha kubariki uchafu wote unaotendeka nchini kwa kukaa kimya bila hata kuwakemea wanaofanya hivo?.
Nilikuwa nawaza tu
 
Tatizo hata vyama vya upinzani vifurukute vipi haviwezi kuachiwa na washika dola kukua na hata kushinda. Mbona washika dola wenyewe washasema!

Na hii siyo mara ya kwanza kutamkwa, sio Tanzania pekee, ni hata katika nchi nyingine za Afrika.

Hata hivyo binadamu ni viumbe wanaoishi kwa kubadilika kifikra. Itachukua muda lakini CCM haiwezi kudumu milele kama wenyewe wanavyo tangaza.

Na kwamba hiyo haitakuwa maajabu ya dunia. Dunia imesha shuhudia mengi yakitokea, mengine hata hayakupata kufikiriwa.

Inapendeza kupata chama mbadala kutawala, lakini kwa mazingira yaliyopo ni vigumu. Na kwamba hakuna chama kitakachopewa hiyo lulu katika kisahani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Rubawa, Kamandoo hata mimi nilizungumza nae, ni kweli alipanga kujiongezea au kumuweka mtu wake naomba nimuhifadhi, CCM bara ikafanya mambo, Karume akasimamishwa na kwenye matokeo, kiukweli naomba nisiseme ila wote wanajua kilichotokea.
Komandoo aliadhibiwa kiaina kama Aboud Jumbe.
P
 
Ni kujidanganya tu... Hakuna chama cha kuitoa ccm madarakani kwa sasa.
 
Mkuu Rubawa, hayo unayoyasema mimi pia nayapitia, baada ya lile swali la Ikulu, kuna watu wanafanya mambo ya kiajabu ajubu as if wametumwa na yeye, kwasababu wanajua huwezi kupata access kuuliza, lakini through circumnavigating, nimeweza kubaini hao watu hawajatumwa na Magufuli, tena usikute hata Magufuli mwenyewe hajui nini watu wake wanawafanyia dhulma kubwa watu in his name!.

Kwenye wateule wake, unaweza kukuta sii kweli
Mh rais Magufuli amewapa wateule wake madaraka makubwa ya kudhurumu na kunyanyasa kwa kisingizio cha kutumwa na rais, hivyo wewe kudhani ni kweli wametumwa na rais Magufuli hivyo kudhania kuwa Mh rais Magufuli anajua dhuluma zote juu yako, kumbe in reality rais Magufuli hajamtuma yoyote kufanya dhulma zozote na hivyo hajui chochote kuwa huku chini kuna watu wana nyanyasika.

The best way kuujua ukweli ni kufanya cross checking kwa kutumia njia inayoitwa circumnavigating ikishindikana, then unatumia direct.

Kuna mambo mengi mabaya wanamhisi ni rais Magufuli, lakini ukweli sio yeye na wala hajui kitu.

Mfano kuna watu wanadhani lile tukio la zile pyu pyu pale Dodoma ni yeye, kumbe sio yeye wala hakujua kitu, ila...

Mambo mengine ni too sensitive tuyaache yapite ila yote yana mwisho haya.
Pole kwa yote.
P
 
Wewe ndiye unaota
Ndoto unazoota baada ya kunywa kvant ipo siku utaenda kumshika makalio mamako mkwe, ndugu hizo pombe zimekushinda ziache, ni hivyo tyu. La maaskofu wenu limekuchachia umerukia jengine.

In God we Trust
 
Huo ndiyo ukweli kuwa ccm inafikia kikomo mwezi October
In God we Trust
 
Sijawah kusikia taarifa ya USA kuhusu democrasia ya China... Tumejirahisisha sana
Na US hajawahi kuwanunulia China vyandalua vya malaria au msaada wa ARV.
Unapokuwa masikini na unalelewa hata vitu vidogo vidogo lazima ukubali hata mipango yako ya maisha anayekulea ana ihakiki.
Ni kama mtoto wako nyumbani, waweza kumsimamia hata ratiba ya kuoga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itawatawala milele nyinyi mazuzu msiyo na faida kwa taifa
In God we Trust
 
Unajua kwamba katika kipindi cha miaka minne iliyopita hakuna siasa za upinzani zilizo fanyika nchini kote zaidi ya kesi za polisi na mahakama kwa wapinzani? Unajua kwamba viongozi wengi wa upinzani walidhoofishwa kisha kulazimika kuikubali CCM hadharani ikiwa ni mbinu ya kuipaisha CCM?
Kama wewe ni National Sales Manager basi naipa pole hiyo kampuni unayofanyia kazi, kwani kama umekosa uwezo wa kuligundua hili uwezo wako utakuwa chini mno.
Hivi unajua kwa nini vijijini Waalimu walitumika sana kuijengea sifa CCM? Ndio wanaoaminika na ndio kundi la wasomi walio karibu nao. Jee mahusiano ya walimu na serikali ya CCM awamu ya tano unayajua kwa sasa?
Watumishi wengine jee? Nenda kwa wafanyabiashara ambao wanafunga biashara zao kila siku utawaambia nini na Magufuli? Usidanganyike na sifa za usoni ni kwa vile wanao mchalenji wanakiona cha mtema kuni kimya kimya.
Tumehuru na wapinzani kupata majukwaa ya kusemea nyongo zao ndio utajua kuwa CCM maisha yake yamekamatiwa na Uzi mdogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal nimefurahi sana kuona muono wangu tupo wengi hasa kwa yeyote ambae kutafiti kidogo. Kwa hali inavyo endelea tutaruhusu vyama vya upinzani kukosa nguvu kabisa kama hatuta weka nguvu ya kutosha kubalisha hii hali.

Kwa hiyo kila tuandikapo kuhusu kufa kwa CCM naomba ukweli huu mchungu tuwe tukiujuwa. Kutembelea wananchi vijijini na miji midogo utajifunza mengi sana. Asilimia karibu 80% ya Watanzania vijijini na Miji midogo wanaamini Magufulu ni mtuu wao. Kila kilicho fanya vizuri na Halimashauri, Mikoa, Vijiji utasikia Viongozi wanasema kazi ya Mkulu na wananchi imeanza kuwaingia kuwa kila kizuri nchi hii kinafanya na Mkulu pekee au maelekezo yake.

Viongozi wengine wote wanaonekana ni wasumbufu tuu, Upinzani tusi zembee kuna kazi kubwa ya kufanya na kwa hali ilivyo kama uchaguzi unafanyika leo tutasumbuka na matokeo kwa kuwa hatuto amini. MAENDELEO HAYANA CHAMA.
 
Utabiri kutoka MAREKANI!!!
 
Hivi kuna mkakati gani unaoeleweka utakaoitoa CCM madarakani kwa huo muda unaosema? Watu Wa hivi huwa naamini wakati wanaandika haya walikuwa wamelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…