Uchaguzi 2020 CCM na NEC mtanzikoni

Uchaguzi 2020 CCM na NEC mtanzikoni

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wagombea wa Udiwani wa Kata za Mukendo na Kwangwa, Manispaa ya Musoma Mjini, wameshindwa kuchukua fomu zao za kugombea udiwani katika kata hizo, baada ya watu waliojitambulisha kuwa wagombea wa CCM kuchukua fomu hizo na kutokomea nazo!

Chanzo cha habari hizi kinaeleza kwamba hadi sasa Mgombea wa Kata ya Mukendo kupitia Chama cha CCM hajapewa fomu na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Mukendo!

Ni wazi sasa kwa hicho kilichotokea Musoma, katika kata za Mukendo na Kwangwa, kinawaweka CCM na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwenye mtanziko mkubwa sana.

Kwa takriban wiki nzima sasa na usheee hivi, kumekuwepo na taarifa za Wasimamizi wa Uchaguzi katika majimbo fulani fulani kuwapatia fomu za Chadema wagombea ambao hawajapitishwa na Chadema na wala chama hicho hakiwatambui lakini Wasimamizi wa Uchaguzi wamewapatia fomu na kuwanyima fomu hizo wagombea sahihi walioteuliwa na Chadema.

Mifano ya haraka na mizuri ni katika majimbo ya Kilombero na Kibamba. Huko Kilombero Msimamizi aliamua kumpatia fomu kijana mmoja ambaye Wanachadema wenyewe wanajiuliza ametokea wapi, lakini Msimamizi akampatia fomu huku akiwa hana utambulisho wa kutoka mamlaka rasmi zinazohusika na itifaki ya mawasiliano kati ya Chadema na Msimamizi wa Uchaguzi kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi, ambapo Katibu wa Jimbo huwasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi na si vinginevyo.

Huko Kibamba ndiko ambako bila shaka itakuwa patashika na nguo zitachanikia uwanjani. Watu wanaodaiwa kuwa ni CCM au washirika wa mfumo na CCM au wote kwa pamoja, ukiwa ni ushirika wa kihalifu, kwa mara nyingine wameionesha Ofisi ya Mkurugenzi wa Ubungo inapaswa kupigwa MITAMA mikali sana kama Mbasha. Watu ambao Msimamizi wa Uchaguzi amegoma kuwataja, wameandika barua na kumtambulisha mtu mwingine, ambaye pia Msimamizi amegoma kumtaja, amechukua fomu za kugombea nafasi hiyo ya ubunge kupitia Chadema.

Ni kwamba Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibamba, imeandikiwa barua feki, nayo ikawasiliana na mtu feki, kisha ikatekeleza kwa kuzingatia barua feki na kumpatia mgombea feki fomu. Maana yake hata fomu hiyo ni feki kwa sababu mchakato mzima huo umekuwa feki na hila. Wamempatia fomu mtu ambaye hajulikani (wao wanamjua), hajawahi kushiriki hata mchakato wa ndani wa Chadema, wala si mwanachama wa Chadema na hakuna mtu anamjua, lakini wanalazimisha kuwa fomu za Chadema zimechukuliwa.

Tangu matukio ya kihalifu ya Kilombero na Kibamba yatokee wiki iliyopita, NEC wamepatwa kigugumizi sana kuchukua hatua na maamuzi kwa masuala ambayo yako wazi kabisa kuwa ni njama na hila za CCM. Kuendelea kuyakalia kimya inamaanisha kuwa NEC inajua mkakati huo mpya wa kupora fomu kupitia kuwapatia watu wengine. Kisha inawaambia Chadema wakawatafute watu hao kupata fomu zao.

Kwa hicho kilichofanyika Musoma kwenye hizo kata mbili, itabidi CCM na NEC yao watokea tu tunduni walikojificha wakishirikiana kwa siri. Je nako huko pia watawaambia CCM wakawatafute hao waliochukua fomu?

Tunasubiri kuona na kusikia. Je, Msimamizi ataendelea kusimamia anachokiamini (wanachofanya kwa Chadema wakiamini ndiyo sahihi) au atabadili msimamo kwa kuwa tu wagombea hao ni wa CCM!?

Ngoma inogile sasa wakunyumba mbombo ngafu
 
CHADEMA waiombe NEC i address hili suala maana wakisema waingie kwenye umafia wa aina hii wataumia sana. Wajue CCM ndio wameshika mpini. Wasimamizi wa chaguzi za madiwani ni Wakurugenzi wa Halmashauri. Kitendo cha Mkurugenzi kutamka tu "Fomu imeshachukuliwa na mtu kutoka chama chenu", habari inakua imeishia hapo!!!
 
Haya mbona tulikuwa tunafanyiwa upinzani? Naona jini limekata kamba
Hawa sio wa kuwaamini, inawezekana wanatengeneza justification kuwa hata majimbo kama Kibamba sio michezo yao.

Eti kwao kata ndio fomu zimetolewa then kwa Chadema ni fomu ya jimbo, hawa jamaa ni kenge sana wanaharibu nchi then pakinuka waonekane wapinzani ndio shida.
 
Maigizo ya ccm hayo ili na wenyewe waonekane wameathiriwa na huo ujinga but hiyo haipo.
 
Policcm wameanza kampeni zao za ushindi..wapinzani wakae kitalaam wataliwa vichwa mapema tu
 
kuna shida gani watu au kwa mtu yeyote kupewa form? maana yake NEC wanahalalisha wagombea binafsi... si waseme tu kwamba wagombea binafsi sasa ruksa... ya nini figusu? kama ni kwa chama, tutawaona wakati wa campagn wanao jimwambafai kwamba ni wawakilishi wa CDM/CCM ili hali sio... NEC haiwezi kuwa na au ku-print form moja pekee.. ni kujiabisha tu humu ulimwenguni bilasababu yeyote ya msingi...
@Judge Kaijage- tafadhari- simamia haki- wewe ni ulikuwa judge na weledi wako ndio sasa utakuwa unaangaliwa...
 
Kama tume wameanza kulea ujinga mapema hivi wataweza vipi kuusimamia uchaguzi kwa haki
 
Kwanini awa wanaodani wanalinda amani ndio wanakuwa chanzo cha uvunjifu wa amani?
Unawezaje ukawa msimamizi wa uchaguzi alafu ukatoa fomu kwa mgombea feki ali ukijua taratibu zote na namna gani ufanye na mgombea anapaswa awe na vielelezo gani kutoka kwenye chama chake? Maajabu haya...........
 
Kwanini awa wanaodani wanalinda amani ndio wanakuwa chanzo cha uvunjifu wa amani?
Unawezaje ukawa msimamizi wa uchaguzi alafu ukatoa fomu kwa mgombea feki ali ukijua taratibu zote na namna gani ufanye na mgombea anapaswa awe na vielelezo gani kutoka kwenye chama chake? Maajabu haya...........
Unaamini kua hawajui au ni bahati mbaya mkuu? Yajayo yanafikirisha
 
Mjinga tu ndio ataamini Mambo ya kijinga kutoka kwa wajinga. Kama waliweza kutumia SSIT kutuganya anauza mahindi watashindwa Hili ili kusawazisha Mambo!!
 
Back
Top Bottom