CCM na Serikali Watanzania Wamewakosea Nini Hadi Kuamua Haya?.

CCM na Serikali Watanzania Wamewakosea Nini Hadi Kuamua Haya?.

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Ulimnofu.
Asalaam alykhum.
Bwana Yesu asifiwe.

Kule DRC poleni kwa kuwakosa ndg waliofariki maji ziwa Kivu.

Nisipoteze muda.
Adani Group inaonekana ni kampuni imeundwa maalum si kutoa huduma ipasavyo nje ya nchi zawa kwao huko India.

Nje ya India kampuni hilo halina tija na ufanisi kwenye factors muhimu.

Baada ya kufuatilia kwa kiasi kidogo tu nimegundua hao jamaa adani group wanatumika katika baadhi ya nchi barani afrika na baadhi ya nchi za ulaya kama ni special robbery company.

Wazungu huko wameitimua hii kampuni, juzi hapo Kenya wananchi wameishtukia hii robbery company na kuliamsha kuwa wasipewe uwanja wao.

Baada ya kuona wakenya wameshtuka serikali ya Kenya ikapiga maktaimu na sidhani kama itawapa JKIA.

Kuna mkenya ambaye aliibua sakata la hiyo robbery company to afrika akasakwa na serikali ili wambane pumbu jamaa akatoweka now yupo ugaibuni.

Hatimaye Adani imetua Tanganyika (shamba la bibi) Tanesco inaenda kugawanywa vipande vipande ili tu wahindi hao wapate ulaji wa kukusanya Tshs na kuzipelekakuwa dollar zitakazopelekwa India.

Viongozi wa serikali na CCM hamuoni aibu kuifanya hii nchi shamba la bibi?.

Najua mnakumbuka mfano, wale wahindi mliowapa TRC je, walifanya nini cha ziada ambacho leo kinafaida kwa nchi?.

CCM na viongozi wa Serikali Watanzania Wamewakosea Nini?

Mnajua kwa sasa hatuna shida na umeme mara baada ya bwawa la Mwl. Nyerere kuanza kuzalisha umeme wa kutosha na mwingine unaenda kuuzwa nje ya mipaka ya Tanganyika.

Kuna nini au nani anatakiwa kuiibia fedha nchi kwa kipindi hiki?.

Hebu tuone aibu, japo hamna uchungu na nchi hii ila oneni haibu aseee, mnatuona hatuandamani na tunaandamana kwenye mitandao ila the day has come.

Je,tumewanyia nini watanzania nyie watu?.
 
Watanzania ni MAZUZU. Lile tatizo la UJINGA alilolisema nyerere bado linaitafuna nchi.

Acha washikaji waendelee kula nchi na vizazi vyao hadi pale wananchi tutakapojitambua.

Lawama hazina msaada wowote kwa sasa na hatupaswi kuonewa huruma.

Mtu isipomfaa akili yake, basi utamdhuru ujinga wake.
 
Tunatafuta Pesa kwa ajili ya uchaguzi mshipa wa aibu tumeukata kwa sasa
 
Ndio mambo mnayoweza watanzania haya. Wewe katika uzi wote hujaona point isipokuwa hiyo typo
Sikutaka kumgusa maana humu JF kuna panya na panya buku.
 
Hawa viongozi wetu kama wameshindwa kutumia Rasilimali zetu kutuondoa katika umaskini, na kuishia kuwapa wageni kila kitu , wasitufanye wote tuonekane wajinga na vizazi vya badae.

Waachie ngazi,

Hivi kwani ni lazima watuongoze?? Inashangaza mno kuna watanzania lukuki ndani na nje ya nchi wenye uwezo mkubwa tu ila kila siku inafanyika recycling ya viongozi.

Mjipime kama kweli mnafaa kuendelea kutuongoza.
 
Back
Top Bottom