Elections 2010 CCM na siku tatu za mwisho za uchaguzi

akashube

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2009
Posts
401
Reaction score
23
A. Kinana ameonyesha umahiri mkubwa kwa wakubwa wake ndani ya CCM kwa kuandaa mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa siku tatu za mwisho za kampeni, tarehe 28,29 na 30 Oktoba CCM inafanya 'suprise' kwa kutoa pigo kali kabisa dhidi ya CHADEMA na CUF ili kuwavuruga kabisa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa upepo kwa wapiga kura.

Akimnukuu R. Odinga waziri mkuu wa Kenya kuhusu umuhimu wa saa 24 za mwisho kabla ya siku ya uchaguzi A. Kinana ameuelezea mpango huo kwa wakubwa wa chama chake kama mkakati ambao ni 'feasible'.

WITO

CHADEMA na CUF jiandaeni na siku hizo tatu za mwisho na hayo masaa 24 ya mwisho.......something dirty is cooking.
 
nimesoma the Guardian na kutambua kuwa ule uchochezi kupitia ujumbe wa simu unauhusiano mkubwa na mtandao wa Chama tawala. Nakuhakikishia kuwa Watz wa leo hawadanganyiki kirahisi. Kinana anajisumbua bure kwani wapiga kura wameshafanya uamuzi tayari. Wanataka MABADILIKO baada ya miaka 50 ya taabu na mahangaiko ndani ya ufukara uliokithiri.
 
Ndugu yangu ni kweli kwamba watanzania hawa danganyiki tena kirahisi lakini u never know watawapata wangapi cha msingi ni kujipanga kama mtoa hoja alivyo sema tusipuuze kila kitu....
 
Mh!kweli hili Chadema inabidi wawe makini nalo sana!
 
Kwa kadiri ya uwezo wao hao mafisadi na watu wasiokuwa na utu na hesihima kwa watu waliowaweka madarakani (hao viongozi wa ccm
) amabo hawatujali wanafikiria kutumia uwizi na kuwachafua wengine kama walifavyomfanyia mrema na cuf 2005 na sasa Chadema, hizo mbinu zote tumeshajua na hizo hila na mbinu zote, watanzania tumwombe Mungu maaanana aanenda kutupa maendeleo makubwa na kutupa rais ambaye anapendezwa naye.
A. Kinana ameonyesha umahiri mkubwa kwa wakubwa wake ndani ya CCM kwa kuandaa mkakati maalumu wa kuhakikisha kuwa siku tatu za mwisho za kampeni, tarehe 28,29 na 30 Oktoba CCM inafanya 'suprise' kwa kutoa pigo kali kabisa dhidi ya CHADEMA na CUF ili kuwavuruga kabisa na kubadilisha kabisa mwelekeo wa upepo kwa wapiga kura.

Akimnukuu R. Odinga waziri mkuu wa Kenya kuhusu umuhimu wa saa 24 za mwisho kabla ya siku ya uchaguzi A. Kinana ameuelezea mpango huo kwa wakubwa wa chama chake kama mkakati ambao ni 'feasible'.

WITO

CHADEMA na CUF jiandaeni na siku hizo tatu za mwisho na hayo masaa 24 ya mwisho.......something dirty is cooking.
 
duh,hii ni balaaa nahisi hata mabomu yaliyo kamatwa huko lindi ndio moja kati ya mipango yao
 
Ndugu yangu ni kweli kwamba watanzania hawa danganyiki tena kirahisi lakini u never know watawapata wangapi cha msingi ni kujipanga kama mtoa hoja alivyo sema tusipuuze kila kitu....

Jamani watanzania tunapopata habari kutoka jikoni tuhabarishane mapema, hii ndio namna pekee ya kukaba mpaka mate, wakitema tunafukia.

Chochote watakachokipanga tutakiweka hadharani. JK akitaka iwe siri ahakikishe hata mijusi wa Ikulu hawajui....lakini vikao!!!!?
 
Tunaanza kuyaona haya taratibu, mara kuchokoza CHADEMA kwa makusudi kisha ' murder case' halafu msg kuwa CHADEMA wamwaga damu, haya tena 'coverage' za TV ni CCM tu, CHADEMA wanapewa kwa ufinyu mno isipokuwa TV ya mlimani tu, haya wanachama kutoka mkoa mwingine( Arusha) kubebwa kwa mabasi hadi mkoa mwingine( Manyara) ili tu JK aonekane kajaza mkutano, msgs za kutisha wanataaluma, vitisho kwa wanavijiji kama huko Iguguno Singida ambao wana CCM wamewatishia kuwa wakichagua CHADEMA nchi itaingia vitani, haya kuweka ndani wagombea wa CHADEMA.

Jamani tuwaangalie hawa kwa makini.
 
Jamani watanzania tunapopata habari kutoka jikoni tuhabarishane mapema, hii ndio namna pekee ya kukaba mpaka mate, wakitema tunafukia.

Chochote watakachokipanga tutakiweka hadharani. JK akitaka iwe siri ahakikishe hata mijusi wa Ikulu hawajui....lakini vikao!!!!?

Teh teh teh, Nimeipenda hii ya kukaba hadi mate.
 
Wanatapatapa.....ni sawa na timu beki hazikabi
 
Back
Top Bottom