Mchambuzi,
Hali ya kisiasa nchini imebadilika sana. Kwa mtazamo nilio nao uchaguzi ujao utategemea sana matumizi ya katiba kuliko uzoeefu tu wa chama fulani ndicho kimeshinda. Nina maana kama Rais atatoka CCM kwa mujibu wako basi bunge litamilikiwa na wapinzani. Uwezekano wa upinzani kutoa Rais kwasasa siyo probability tena ni kitu kilichowazi. Itategemea sana utangamano ndani ya vyama vya upinzani.
lmani kuwa CCM imedumisha amani na utulivu sasa haipo. Sidhani matokeo yanayoitikisa nchi na ambayo wananchi wanajua wazi ni serikali ya CCM ima inayafanya au inayalinda watakubaliana kuwa kuna amani na utlivu.
Amani na utulivu si kukokekana kwa vita tu bali kukosekana kwa amani ndani ya mtu binafsi.
Utakubaliana nami kuwa hali ya maisha ni ngumu sana kiasi cha wananchi wanakata tamaa. Kupokelewa kwa upinzani katika kasi iliyopo ni sehemu ya wananchi kuonyesha hasira na pengine kutafuta ujani wa kujizuia wasisombwe na maji.
Makundi ya wagombea:
Kundi la kwanza ulilosema linapambana na ufiasdi sina uhakika kama kundi hilo lipo tena. Nadhani ingekuwa vema kusema kundi lililokuwa linapambana na ufisadi. Kundi hili la vijana wa mwalimu halipo ndani ya chama na nakuhakikishia aliyebaki ni Peter Kisumo baada ya wengine kuenguliwa kimtindo na kwa chuki binafsi.
Kwa mtazamo wangu, makundi mengine ninaweza kuyaweka kama ifuatavyo
Kundi la pili na tatu yanatokana na kuvunjika kwa kundi la mtandao. Wapo wanaotaka kuendeleza ufalme na wengine wanajihisi kuwa nje baada ya kumenyeka. Makundi haya ndiyo yanayoiumiza CCM kwa sasa.
Kundi la nne ni lile linalodhani uwepo wa kundi la pili na la tatu ndio unaua chama.
Kundi la tano la 'darasa' la mwalimu tayari limeshapoteza umiliki na wamebaki nje ya ulingo wa kisiasa. Ili kuendelea kulitenga katiba ya CCM inawaundia kitu kinachoitwa baraza la ushauri.
Kushindwa kurudisha heshima ya chama ni dalili za kundi hiki kukosa nguvu ya kisiasa kabisa.
Nini kitatokea;
Chama kitaparaganyika. Kutatokea hujuma za wenyewe kwa wenye zitakazonufaisha upinzani kama utasimama imara.
Kuparaganyika haimaanishi CCM kufa, bali ni CCM kupoteza nguvu ya kisiasa.
Ndiyo maana nasisitiza kuwa utawala ujao utakuwa na mtawala anayemiliki serikali na mwingine bunge au kinyume chake.
Kilichodhahiri ni kuwa muda wa chama kushika hatamu umefika tamati.
Vigezo vya kiongozi
Naongezea tu miongoni mwa yale uliyoainisha. Kwanza ni lazima tuhakikishe kuwa vyombo vya habari vinachukua misimamo ya kisiasa ili kutoa nafasi ya wananchi kuelewa na kuweka hoja kwa mizania.
Hali ya sasa ya kujificha kwa kutumia hoja ya uandishi usiofungamana ni kujidanganya. Hili lispoangaliwa linaweza kutumika vibaya sana kama lilivyotumika huko nyuma kuwachafua au kuwapamba viongozi. Njia moja rahisi ni kujua kuwa gazeti au televisheni ipi inasimamia wapi. Tuache wafanye endorsement za wazi ili kila habari ichujwe kwa uzito wake.
Pili, kwa kukosekana takwimu za upigaji kura mahali kama bungeni, ni vigumu sana kujua msimamo wa kiongozi.
Mchambuzi, nikupe mfano. Leo watu wanaongelea Bernad Membe kama potential candidate. Jambo baya ni kuwa hatujui huyu mtu ana misimamo gani kuhusu masuala ya taifa kwasababu amejificha katika uvungu wa serikali.
Mfano wa pili, Lowasa sasa anazungumzia ajira, kilimo kwanza, elimu n.k. Lakini alikuwa katika serikali miaka mingi tu na hatujui misiamamo yake juu ya masuala hayo.Huyu utamhukumu vipi ikiwa hatujui misimamo yake mingine zaidi ya ile tunayoijua.
Tunatakiwa tujue uadilifu wao. Napo pana kikwazo kwasababu rekodi za uadilifu wao wameziwekea kinga ya kutosomwa au kujulikana. Tutabaki kulumbana huyu ana mali Uingereza
Nadhani kigezo muhimu sana kiwe utendaji wa mtu akiwa popote, mafanikio na kushindwa kwake.
Uadilifu usiishie kuangalia thamani zake, uadilifu ni pamoja na hekima ya mtu, tabia zake akiwa mwenyewe au na wenzake na hulka ya mtu miongo michache iliyopita.
Kama wapinzani wataacha kuiga siasa za CCM basi wanaweza kufanikiwa kumlete mgombea mwenye kukidhi vigezo. Nasema hivi kwa kuangalia huko nyuma waliwezaje kufanikiwa hata kama hawakupata walichokusudia. Mfano, Chadema waliweza kumpa mgombea kwa utaratibu tu na si kufuata nani mwenyekiti n.k.
Tatizo linalowakbaili linatokana na kuiga CCM, kuogopana na kuacha kukijenga chama kama taasisi. Hapa nina wasi wasi kama wanaweza kuleta mgombea atakayekidhi vigezo.
Kwa upande unaoushauri wewe wa chama chako, ningeshauri watumie utaratibu wa udikteta. Fulani awe mgombea, period. Kwa kutimia vigezo vyako na vingine tusivyovijua au tulivyoviacha au kuvisahau CCM itamalizika kabla ya kuingia katika uchaguzi. Hakuna mtu anayeweza kusimama na kujenga hoja kwa uhalali na haki akaachwa kupelekwa mabwePande.
Utamaduni wa majaribio ya kutoana nafsi ulioasisiwa na CCM utatumika kwa yoyote yule awaye, mgombea au mpambe. Utawezaje kupata mtu mwenye vigezo kwa utaratibu huo?
CCM wakitumia vigezo unavyopendekeza kama mwanachama wao, huo ndio utakuwa umehitimisha miaka 50 ya utawala. Nakuhakikishia na naomba uninukuu vema, kabla ya mwaka Dec mwaka huu utaona mvurugano na hadi 2014 unaweza kusikia baadhi ya watu wametoweka katika mazingira tatanishi.
Mwalimu Nyerere alisema ukianza kula nyama ya mtu hutaishia hapo utakula zaidi.
Nadhani wakati umekwisha wa kumfundisha mbwa mzee ujanja mpya 'teach the old dog new tricks'
Wakati umefika tutengeneze kitu na tuachane na utaratibu wa recycling.
Ikidibi kuwa na recycling basi yatumike material nje ya yale yaliyomo katika gabbage bin.
Nguruvi3,
Asante sana kwa mchango, kwa kweli umetoa hoja nyingi nzuri sana, na zina amsha tena huu mjadala, ambao ulianza kulega lega, huku umuhimu wa mada kama hizi ukizidi kuongezeka kwa jinsi tunavyozidi kukaribia 2015. Kimsingi, nakubaliana na mawazo yako mengi. Nitajaribu kujadili hoja zako kadhaa ambazo aidha tunapishana kidogo au zinazohitaji ufafanuzi zaidi.
Kwanza, ni ufafanuzi. Msingi wa hoja yangu haikuwa kuzungumzia vigezo vinavyotumika kumpata mgombea wa ngazi ya Urais (CCM) au ubora wa vigezo hivyo, bali kuzungumzia aina ya wagombea watakaojitokeza, hasa kwa mwendo wa makundi. Vinginevyo nakubaliana na wewe mia kwa mia kwamba vigezo na utaratibu wa sasa kwa ujumla wake, ni mbovu na hauzai viongozi wazuri. Kama tunavyofahamu, kamati kuu itachuja majina na kubakisha matano kwa vigezo ambavyo huwa havijadiliwi sana, aliyekuwa anavijadili ni Mwalimu Nyerere, hata wakati tulipokuwa tunaelekea uchaguzi wa 1995. Ukitazama kwa makini vigezo ambavyo Mwalimu alitueleza vinatumika na kamati kuu katika kupendekeza majina matano kati ya jumla ya wana ccm wote waliojaza fomu, kwa kweli leo hii ni majina machache sana ya wanasiasa wanaotajwa tajwa yanakidhi vigezo vile.
Na kuhusu umuhimu wa udikteta katika kupata kiongozi mzuri, nakubaliana na wewe, nah ii ndio njia Mwalimu aliitumia na kuweza kutupatia viongozi wazuri, hasa 1995 kwani 1985 siasa za zamu ya upande huu au ule ndio zilitawala. Sina maana kwamba rais wa awamu ya pili hakuwa mzuri, hoja yangu ya msingi ni kwamba vigezo alivyozungumza Mwalimu 1995 vilitumika na tukapata rais mzuri sana – B.W. Mkapa. Lakini tukumbuke pia kwamba, hata Mkapa 2005 na yeye alitumia udikteta kutupatia kiongozi wa kumrithi. Akiwa bado Mwenyekiti wa CCM taifa, Mkapa alifuta utaratibu wa 'Kura Tatu' ukumbini mkutano mkuu 2005 na kuagiza utaratibu wa ‘Kura Moja' ufuatwe, na ndio ukasaidia kupatikana na Rais wa sasa. Kwahiyo hili la udikteta linawezekana, ila suala linalofuatia hapo ni je, utaratibu kama huu ni kwa manufaa ya nani: Chama? Taifa? Kundi fulani? Huu ni mjadala tofauti na nisingependa kuingia huko kwa sasa.
Hoja ya pili ambayo ningependa kuijadili ni ile ya wapambanaji ufisadi. Sikuelewa vizuri sana hoja yako kuhusu Mzee Kisumo, je maana yako ni kwamba yeye ndiye mpambanaji wa kweli dhidi ya ufisadi aliyebakia? Vinginevyo nakubaliana na wewe kimsingi kwamba wapambanaji wa dhati ni wachache, au hawapo tena, na kama wapo, basi ni wachache sana amabo ni miongoni mwa hawa tunaowasikia kila siku. Nadhani wapambanaji wengi wa kweli hawapo madarakani, lakini muhimu zaidi ni kwamba walikuwa na rekodi hiyo hata walipokuwa madarakani, na hata ukiangalia maisha yao ya leo ni ya kawaida sana ukilinganisha na nafasi zao walizowahi kushika. Kwa mfano, mimi nina amini kabisa watu kama Mzee Kaduma ni wapambanaji wa kweli, na career zao zilipata misukosuko throughout kutokana na msimamo huo. Tukirudi kwenye hoja yangu ya msingi, whether wapambanaji wengi wa leo ni genuine or not, bado nina amini kwamba kuna kundi ambalo litajaribu kupitisha mgombea wao kupitia brand ya mapambano dhidi ya ufisadi.
Hoja ya tatu ambayo ningependa kuijadili ni ile kwamba Upo uwezekano mkubwa wa Rais 2015 akatokea upinzani. Kwa hili tupo pamoja, ila naomba kuhimiza kwamba - msingi wa mada yangu haikuwa kujadili kwamba Rais 2015 atatokea CCM, bali mchakato utakaotoa mgombea urais CCM 2015. Lakini tukiwa bado katika hoja hii, ningependa kusikia maoni yako kuhusu suala ambalo huwa ninalijadili sana humu lakini kwa bahati mbaya huwa sipati a good response, na suala lenyewe linahusu KANUNI YA USHINDI kwamba mshindi ni mshindi. Chini ya kanuni ya sasa, iwapo kwa mfano mgombea Urais kupitia CCM 2015 atapata 50.1% ya kura, na wa Chadema 49.9%, mshindi atakuwa CCM! Kwa mtazamo wangu, iwapo kanuni hii itaendelea kutumika 2015, itakuwa ni vigumu sana kwa mgombea wa Chadema kushinda kwani CCM bado ina nguvu sana, hasa vijijini, na sioni CCM kushindwa kupata 50.1% mwaka 2015. Kwa mantiki hii, ushindi wa Chadema 2015 sana sana itakuwa uundwaji wa serikali ya pamoja baina ya CCM na Chadema kutokana na kura kutopishana sana. Swali linalofuatia ni je, Chadema watakubali? Kwani tayari Chadema wameonyesha kutokubaliana na utaratibu huo kwa kuwaita CUF CCM ‘B' kutokana na chama hiki kushiriki na CCM katika kuunda serikali ya umoja Zanzibar. Sababu ya msingi ya Chadema kupingana na hili inaeleweka, lakini iwapo itatokea kama ya Zanzibar, Je Chadema wamejiandaa juu ya hili? watasusia matokeo 2015? Ni muhimu walifanyie kazi sasa.
Hoja ya nne ambayo ningependa kuijadili ni kuhusu hali ngumu ya maisha miongoni mwa wananchi walio wengi inayopelekea CCM kuzidi kupoteza mvuto, hivyo kuwepo na uwezekano wa upinzani kushinda 2015. Kwa hili nakubaliana na wewe, lakini tukubali pia kwamba Chadema hawataweza kuja na mwarubaini wa matatizo ya msingi yanayokabili wananchi wengi, hasa vijijini ambayo ni yale yale kwa miaka zaidi ya 50 sasa – Umaskini, Ujinga na Maradhi. Hii ni kwa sababu, ndani ya matatizo haya, CCM na Chadema sera zao zinalea hili tatizo kwani wote wana mahaba makubwa sana na
Privatization, Marketization and Liberalization, na tunajua wazi kwamba hawa mapacha watatu kamwe hawataiva chungu kimoja na Maadui zetu watatu wa Maendeleo –
Umaskini, Ujinga na Maradhi. Vinginevyo iwapo una mawazo tofauti juu ya hili, naomba unielimishe.
Hoja ya tano ya kuijadili ni ile kwamba 2015, upinzani lazima uondoke na ushindi aidha wa ngazi ya urais au wingi wa viti bungeni. Uwezekano ni Uwezekano, hivyo kwa dhana ya Uwezekano, hilo linawezekana. Kwahiyo suala la possibility, tupo pamoja, lakini ningependa kujadili suala la impossibility - binafsi sidhani kama Chadema wataweza kupata majority seats bungeni 2015, ila watapata viti vingi sana, hasa kutokana na zoezi lao la M4C, lakini nadhani mwisho wa siku, CCM itazoea at least 60% ya majimbo 2015. Kuna sababu nyingi kwanini nadhania hivyo, kwa mfano, kwanza ukitazama majimbo mengi ambayo CCM ilishinda 2010, ilikuwa ni ushindi wanasiasa wanaita ‘ushindi wa manyoya', yani ‘sweeping victory', na hili litajirudia sehemu nyingi huko vijijini. Pili, wapiga kura wetu wengi wana tabia za kustaajabisha kidogo – unakuta kuna sehemu wanapigia kura mtu na sio chama, ili mradi mtu huyo na yeye awe na msimamo wa kuchukia yale yanayowatesa na kuyasema wazi, hasa kuikabili serikali bungeni; tatu, kuna majimbo mengi ambayo 2010 kura za urais wananchi walikipigia kura CCM kwa wingi sana, lakini ubunge upinzani (Chadema); inastaajabisha sana kwamba Jimbo la Freeman Mbowe na la Zitto Kabwe ni sehemu ya majimbo ambayo Kikwete alimshinda Dr. Slaa kwa kura nyingi sana (over 60% of the votes went to Kikwete Kigoma kaskazini na Hai). Mbowe na Zitto didn't deliver for Slaa!!. Ni mambo kama haya ambayo yananifanya niamini kwamba, pamoja na ipact itakayojitokeza baada ya zoezi la M4C, bado masuala niliyojadili will will work to the advantage ya CCM huko majimboni 2015.
Kwa kumalizia, nimependa sana hoja yako umuhimu wa kuchagua viongozi kutokana na misimamo yao on 'issues' mbalimbali, na misimamo hii kuwa wazi kwa wananchi. Upo sahihi kabisa, na niliwahi kujadili hili kwenye mada yangu kuhusu vyama vya siasa na ombwe la itikadi. Vile vile nimefurahisha sana na hoja yako kuhusu role ya Media kwenye siasa za nchi. Mimi nadhani sisi bado wachanga sana katika hili, hasa ikizingatiwa kwamba, kwanza media nyingi ni media maslahi, tofauti na nchi za wenzetu ambako media organization zinaundwa ki-itikadi, hivyo kazi zao zote kuwa na mrengo maalum.