Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mchambuzi,
Labda nizirejee hoja zako kadri zilivyonigusa na bila mpangilio.
Kuhusu 'majority takes all' kwa maana ya mshindi wa 50.1 anakuwa ameshinda hakika hili lilitengenezwa makusudi kabisa kutokana na hali ya ZNZ na CCM kujifunza kutoka hapo.
Utaratibu huu sikubaliani nao kabisa kwasababu tunaweza kupata kiongozi aliyechaguliwa na asilimia 30 ya wapiga kura.
Pili, ni utaratibu unaoweza kujenga mazingira ya rushwa na si ushindani. Rushwa ninayoiongelea ni ya kuunga mkono vyama vidogo vidogo ili viweze kugawa kura kutoka vyama viikubwa.
Hapa ndipo nasema Chadema walikosea sana kumkabidhi JK hoja ya katiba. Sidhani kuwa akina warioba ambao ni CCM wataweza kufanya tofauti na ilivyo. Sina imani hiyo na hakika Chadema ambao walipewa dhamana wameshindwa mtihani huu wa mwanzo.
Kuhusu Peter Kisumo, sina maana kuwa yeye ni msafi lakini tofauti ya vijana wa mwalimu na hawa wa sasa ipo sehemu moja tu, kuwa wakati ule wazee walisikiliza wananchi wanasema nini na wali act kufuatana na matakwa ya wananchi hata kama si 100%. Uongozi wa sasa kuanzia BWM na JK naweza kusema kwa dhati kabisa hausikilizi hoja na manung'uniko ya wananchi. Kwahiyo Kisumo namweka katika kundi la vijana wa mwalimu kwa mtazamo huo.
Mara nyingi amesema jamani tunapokwenda sipo, lakini nani amsikilize.
Kuhusu Chadema kutokuwa na mworabaini wa matatizo ya Maradhi, umasikini na ujinga nakubaliana nawe kuwa nchi hii haiwezi kubadilika kwa siku moja. Tutakuwa wazembe kama basi hatutafikiria kizazi kijacho kwa kuamini 'status quo'. Ni lazima tuwe na mahali pa kuanzia na pa kuanzia ni hapa.
Lakini pia ukumbuke kuwa kinachowatia wananchi maudhi si umasikini, maradhi na ujinga tu. Hasira zaidi ni pale ambapo hakuna jitihada za kuwasadia zinazoonekana na kinachoonekana ni kila mtu abebe alichojaliwa.
Hivi unadhani mwananchi anajisikiaje akisikia hakuna dawa wakati huo huo kuna mwenzake mtumishi wa umma ana pesa ambazo mkulima wa kawaida hawezi kuziweka katika tarakimu.
Wananchi wanajiuliza endapo hali ni mbaya iweje watu 27 wahodhi mapesa zaidi ya bajeti za maeneo yao. Wanajiuliza, kama hakuna mwarobani iweje ubadhirifu umekithiri na wizi wa kodi zao umekuwa kama fashion.
Hasira zao ni pale wale wenye dhamana ima wameungana na wahalifu au hawataki kuwachukulia hatua wahalifu. Hapo ndipo wanaona basi wakati umefika tujaribu kitu kingine kama walivyofanya Kenya, Zambia, Malawi n.k.
Ni kutokana na hayo ile hali ya kutegemea kura za vijijini kwasasa haipo. Nakuhakikishia kuwa huko vijijini kuna mwamko mkubwa kuliko mijini tulikozoea. Angalia uchaguzi wa wabunge mwaka 2010 na 2005. Utashangaa kuwa jiji kama la Dar es Salaam limebaki nyuma kukumbatia mtazamo tofauti. Inakuwaje huko mikoani watoe wabunge wengi kuliko Dar?
Tumeshudhudia hata vijiji vikihama kwa makundi dalili mbaya sana kwa CCM.
Na mwisho, tusiangalie privitization, marketization na Liberization kama chanzo cha matatizo. Vitu hivi havikuanza leo vikuwepo. Vitu hivi vimepata nguvu kutokana na udhaifu wa mifumo na uongozi wetu.
Mdudu mbu yupo siku zote katika mazingira yetu, ni hadi pale tutakapokuwa dhaifu kujilinda tutaugua malaria. Tatizo si malaria ni udhaifu wetu unao mpa mbu nafasi kueneza malaria.