CCM nambari wani

Watu watataka mabaliliko wakiyakosa ndani ya ccm watayatafuta nche ya ccm
 
Erythrocyte karibu CCM najua kuna siku utakamata kadi yako safi uingie ktk safina aliyotuachia ml Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Kuna mpuuzi mmoja wa Lumumba amkuja na porojo zake eti amegundua kuwa wafuasi wa CDM ni watu waliokata tamaa... hapa atapata majibu ya kina ...
 
Erythrocyte karibu CCM najua kuna siku utakamata kadi yako safi uingie ktk safina aliyotuachia ml Nyerere
Utasubiri hadi miguu ikuingie tumboni , ujana wenu mlikuwa na nani , mmekongoroka ndio mnataka mimi nije huko ! Nendeni chalinze .
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tpaul itakuwa vizuri sana kama ukituongezea na picha za hospitali ya taifa .
 
Type kama hizi kuthaminiwa wakati wa Uchaguzi tu. too sad.

 
Type kama hizi kuthaminiwa wakati wa Uchaguzi tu. too sad.


nyinyi mkishasoma mnawakimbia wazazi wenu kule kijijin mnawaacha wanapigika au mnataka chama cha mapinduzi kiwasomeshe halafu kiwasaidie kuwatunza wazazi wenu.
 
Hao wazazi wamezaliwa ktk nchi yenye utajiri mwingi wa asili ambao mmeamua kuwa malaya wa kugawa kwa mataifa ya nje!!! ... Just to name few of them: Tuna Mt Kilimanjaro, Mt Meru, Lake Victoria, Lake Tanganyika, Lake Rukwa, Lake Nyasa, Jipe, Natron, Manyara... Mungu akatupatia ardhi yenye Tanzanite, Gold, Uranium, Diamond, Nickel, Copper, Ruby, Greenite, Quartz, Gypsum, Iron, Coal, Gas, Oil, Magadi, Chumvi...Tuna Mabonde mazuri yenye kutiririsha mito ndani yake ikiwemo Malagarasi, Ruvuma, Ruvu, Rufiji... Mungu akatupendelea Bahari yenye JOdari watamu wenye kuzaliana Tanzania na kusambaa Duniani kote! ...Tunakila kitu na Utajiri wa kuwalipa na kuwatunza wazee wetu kama wafanyavyo nchi nyingine zisizokuwa na Rasilimali kama za kwetu! Ila CCM kwalaana kubwa mliyokuwa nayo mnawadhalilisha sana Watanzania huku mkiendelea kutembeza bakuli la kinafiq kuomba msaada!!! Grrrrrrrrrrrrrr
nyinyi mkishasoma mnawakimbia wazazi wenu kule kijijin mnawaacha wanapigika au mnataka chama cha mapinduzi kiwasomeshe halafu kiwasaidie kuwatunza wazazi wenu.
 
Mkuu, bado uliyotaja ni machache; ukitafakari sana utalia machozi, ila kila lenye mwanzo lina mwisho!
 
Tatizo kubwa letu watanzania tunaamini juhudi binafsi ndiyo itakayokufanya ufanikiwe si kweli kama nchi isipokuwa na Sera nzuri za maendeleo ,Maendeleo hayawezi yakaja mpaka sasa tunatumia development policy ya 1996 hii nchi inamalengo kweli hata useme unajikwamua kiuchumi siasa safi na Sera za nchi zinaplay great party katika Maendeleo yetu asilimia kubwa ya watanzania hatupigi kura ukiuliza wanajibu mm chama cha siasa kitaniletea ugali Nyumbani kuipuuza siasa na kutojali ndo hapa ilipotufikisha.imefika hatua watu wanaamisha pesa benki kuu kama M-pesa.
 
AMA KWELI wewe ni sampuli ya akina "Kikwete aliyesema Msongamano wa Magari Dar es Salaam ndio maendeleo" Wakati wajomba zake hapo Msoga wanashindia uji wa mtama na maji ya kwenye Rambo la kunyweshea Wanyama".. Yaani wauza cocaine wanaofugwa na CCM ndio unachukulia sample ya kujustify maendeleo ya Mtanzania?!!!!!..Hii nci inahitaji Mapinduzi si bure.. !!
 
Huku Serikali ikidaiwa matrilioni, CCM yapanga hila kushinda uchaguzi 2015!

Na Sylivester Hanga

Toleo la 378
5 Nov 2014

KAMA ingekuwa nchi inaendeshwa kwa itikadi za kidini, ningethubutu kusema kuwa angalau siku hizi Mbunge wa Iramba (CCM) na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, "ameokoka".

Kauli yake ya wiki iliyopita kukiri kuwa Serikali inadaiwa na kuwa italipa zaidi ya shilingi trilioni 4 na ile ya mwanzo kuwa angetamani Bunge Maalumu la Katiba lisimame ili kuokoa fedha, zinamfanya aonekane anabadilika japo katika siasa watu hubadilika kila uchao.

Mwigulu alikuwa akizungumzia madeni lukuki yanayoikabili Serikali kiasi cha kufifisha huduma za afya na sekta nyingine za kijamii. Tatizo lake hasemi ni nini hasa kimekwamisha ulipaji wa madeni hayo, na jinsi fedha za makusanyo ya kodi zilivyotumiwa na zinavyotumiwa na watawala.

Tatizo sio kukopa kwenye mabenki ya kibiashara na mifuko ya jamii – japo hilo nalo ni kasoro kubwa kwa serikali inayojigamba kuwa uchumi unakua; bali tatizo ni namna fedha zilizokopwa zilivyotumika na zinavyotumika. Katika hili, Serikali imefeli; maana ufisadi umepamba moto kila kona, na kote zinazolengwa kuchotwa ni fedha za umma za makusanyo ya kodi.

Na tunavyoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka kesho, hali itakuwa mbaya zaidi. Kwa mambo yanavyokwenda hivi sasa serikalini, wananchi watarajie kupanda zaidi kwa ugumu wa maisha kuelekea mwaka wa uchaguzi wa 2015.
Kwa nini? Kwa sababu ni kawaida kwa wanasiasa wanaoutaka urais kutumia kila hila na ghiliba kuchota mapesa ya umma kwa ajili ya kuwania ubunge na urais; hata kama wanajua kuwa baada ya miaka 9 kupita ndani ya Ikulu watasema; "nimechoka natamani siku ziende upesi" (rejea kauli ya Kikwete ya hivi karibuni).

Huku kukiwa na mahitaji ya zaidi ya shilingi bilioni 270 kwa ajili ya kuboresha daftari la wapiga kura, uendeshaji wa kura ya maoni kuhusu Katiba Pendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ufisadi ndani ya serikali ndiyo kwanza umepamba moto.

Ukiacha kashfa ya hivi karibuni ya Bunge kutumia vibaya fedha za umma kwa malipo yanayotia shaka, kashfa nyingine za ufisadi bado zinalitafuna taifa na kuzidi kuwachanganya wananchi.
Hivi karibuni, Zitto Kabwe na kamati yake ya Bunge anayoiongoza alimtaka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutoa taarifa kuhusu zilivyochotwa zaidi ya Sh. bilioni 200 kupitia akaunti ya Tegeta Escrow ya IPTL.


Hivi sasa Watanzania wanasubiri kwa hamu kuona kama TAKUKURU na CAG wataitoa ripoti hiyo kwa wakati, na kama ripoti yenyewe itakuwa na tija kwa Watanzania au tija kwa mafisadi wachache ‘wanaokingiwa kifua' na Serikali kwa makusudi. Shaka ya wengi ni kwamba itakuwa sawa na ripoti nyingine zilizoishia kwenye makabati ya maofisi ya watawala wetu!

Wakati gharama za malipo ya kitanda katika hospitali kuu ya rufaa nchini ya Muhimbili zikitangazwa kupandishwa wiki iliyopita (na bila shaka huduma nyingine nazo zitapanda) kuna madai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinajiandaa kukijaza mapesa chama kipya cha siasa kilichoanzishwa hivi karibuni ili kiweze kuvuruga jitihada za vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) visifurukute na viondokewe na maelfu ya wanachama.

Hapo ndipo Tanzania yetu ya sasa ilipofikia. Yaani mahospitalini hakuna dawa, shuleni wanafunzi wanakaa chini, maabara hakuna na walimu hawana nyumba - bila kusahau akina mama wanaotembea Kilomita 10 kusaka maji, lakini bado chama tawala kinapanga mbinu ya kuchota fedha za walipakodi serikalini ili kufadhili chama kimoja kipya cha siasa kivuruge muungano wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mkuu ujao. Yaani CCM kinapanga hivyo kwa lengo la kukiwezesha tu kubaki madarakani milele na milele!

Ndiyo maana waliomtazama Katibu wa Propaganda wa CCM, Nape Nnauye, siku moja tu baada ya UKAWA kuweka msimamo wa kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu ujao, walibaini kuwa ndani ya sakafu ya moyo wake alitambua kuwa jambo hilo litaikwaza CCM kwenye uchaguzi ujao, na hiyo ndiyo asili ya kutafuta mbinu ya kuuvuruga muungano huo mapema.
Kama habari za CCM kujipanga kukijaza mapesa chama hicho kipya cha siasa ni za kweli (ni dhahiri wahusika watakanusha tu), basi Watanzania wasitarajie kupungua kwa gharama za maisha katika sekta muhimu hadi baada ya mwaka 2015.


Nasema hivyo maana; chama hicho kipya kitapewa mamilioni ya fedha zilizochotwa kijanja serikalini (kama ilivyokuwa kwa EPA) ili ‘kukinunua' chama hicho kipya cha siasa kiuvuruge muungano huo wa UKAWA.
Si hivyo tu, mapesa hayo yatatumika pia ‘kuwanunua' wananchi wenye njaa, wasioweza kulipia kitanda hospitalini, wasioweza kulipa michango ya shule kwa watoto wao na wale wanaopenda sana kunywa pombe na kuvaa sare na leso za CCM ili wajiunge nacho.


Kwa kufanya hivyo, taarifa zinasema watakuwa wamepunguza nguvu za vyama vya upinzani; hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na CUF vinavyolengwa zaidi kufifishwa.
Ushauri wangu kwa hao watakaorubuniwa kwa fedha hizo chafu za CCM na serikali yake ni kuwa, kama hawawezi kuzikataa, basi wafuate ushauri wa Mzee Ndesa (Ndesamburo) kupitia kauli yake ile ya "pesa zao chukueni, kura kwa mwingine".

Na ndiyo maana tunaposema CCM kimepoteza dira yake, hatukionei; maana, kusema kweli, hivyo ndivyo kinavyoiendesha nchi tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, afariki Oktoba 14, 1999 – yaani kihila hila. Angelikuwepo hai Baba wa Taifa wanajua asingekubali mambo haya ya kupanga njama za kushinda uchaguzi kihila.

Vyovyote vile, itakuwa ni jukumu la wananchi wenyewe kuamua kupokea fedha hizo chafu ili wavibomoe vyama vya upinzani lakini baadaye waendelee kulipia gharama mpya za tiba, shule nk ama wazikatae, na hivyo kutoa fursa ya kuiondoa CCM madarakani mwaka 2015 na kuleta mageuzi ya kweli nchini.

Wakati mwingine huwa nawauliza vijana na wale wanaotetea mifumo isiyowasaidia wananchi wengi kuondokana na shida kuwa wanapata faida gani kwa kukumbatia yale yale na watu wale wale na chama kile kile (CCM) wakati dukani bei ya sukari, saruji, mabati, maharage, sabuni nk hupanda kila siku?
Na hiyo haijalishi kama wewe ni CCM, CHADEMA, CUF au TLP. Kama kungekuwa na utofauti wa bei kwa msingi wa uanachama wa vyama vya siasa, ningeelewa; lakini walio ndani ya vyama na wasio na vyama wote wanapigwa na bei zile zile kali zisizoendana na vipato vyao.

Nimalizie kwa kusema kuwa, wakati Serikali ikidaiwa matrilioni ya pesa na mifuko ya jamii karibu yote nchini, na pia wafanya biashara wanaotoa huduma mbalimbali, inasikitisha kuwa upande wa pili inashindwa kudhibiti matumizi ya fedha za umma kwa kuchagua vipaumbele stahiki.

Busara inahitajika hivi sasa kuamua nini kinatangulia. Ni kuandaa daftari la wapiga kura kwanza, kufanya chaguzi za serikali za mitaa, na kisha baadaye uchaguzi mkuu au kura ya maoni kuhusu Katiba Pendekezwa itangulie kabla ya Uchaguzi Mkuu au kura hiyo isubiri mwaka 2016 ili kwanza hospitali zipate madawa na shule zitoe huduma stahili?
Kura ya maoni kuhusu Katiba tata inayopendekezwa inawezaje kuwa ndiyo kipaumbele cha matumizi ya fedha za umma katika nchi ambayo karibu mahospitali yote nchini (ikiwemo hospitali kuu ya Muhimbili) hayana madawa na watu wanakufa kila siku?

- See more at:Raia Mwema - Huku Serikali ikidaiwa matrilioni, CCM yapanga hila kushinda uchaguzi 2015!
 

Hatimaye mmaranguoriginal ametangaza kumng'oa mrema vunjo kwa tiketi ya magamba! Je haogopi moto wa UKAWA ?
 
kwa ufisadi huu wa CCM,ni bora waanze kujichimbia kaburi. wananchi wanaishi maisha magumu kama haya wakati CCM inaalika matepeli ya kisingasinga kutoka Malaysia kuja kutapeli pesa za wananchi. wagonjwa wanaokufa hospitalini kwa kukosa dawa, ni LAANA tosha kwa CCM na serikali yake. wafahamu kwamba hata kama wamewatupa walalahoi na kukumbatia mafisadi, Mungu atazidi kuwambua tu kwani Mungu huwa hawatupi waja zake.
 
Watu wanaiba mabilioni ya fedha halafu wanafutwa kazi tu inaishia hapo...Prof Kikwete aliwahi kuwasamahe wezi wa EPA na kuwabembeleza wamrejeshee fedha na walipofanya hivyo akawaachia huru waende zao mitaani ili waendelee kutuibia. Nchi hii aliyeiloga kafa. Ama kweli CCM ni ukoo wa panya-babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining'ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2015 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari' ya bei ya juu ya umeme, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha, EPA na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It's a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that's when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM's tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave in a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits the minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that many Tanzanians hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrendously, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!

The only weapon we have today, if we wish to change the history of our country that has been exploitative since independence, is UNITY AND SOLIDARITY. We must understand that our government and the ruling party will not easily accept to quit the state and leave all fruits they are enjoying currently. We must ensure our people join us in this struggle. I believe one day we shall all enjoy living in a country without discrimination, exploitation, suffering and humiliation.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…