Si kweli kwamba wananchi wote wanataka UKAWA iingie Ikulu bali Mafisadi na Mawakala wao
Yaani Lizaboni jinsi ambavyo tunaitaka hiyo CCM iingie kaburini haijalishi ni jiwe au binadamu anagombea nafasi hiyo.Kwa sasa Lizaboni mngekaa mjiulize ni wapi CCM ilikosea??Ni wapi JK alitakiwa kurekebisha akakosea???
Escrow tunaijua ya MKOMBOZI tu ya STANBIC nani muhusika???Je ni Lowassa??Tutajieni nani muhusika labda tutarudisha moyo.
Mmekaa miaka 54,shule hazina madwati,kama yapo ni yake ya ENZI ZA MWALIMU,yamechoka na mengine yameliewa na mchwa.
CCM tulijichangisha tukaweka SUPERMARKET (SUKITA) Mabasi ya wanafunzai yote haya yameenda wapi hivi ni Lowassa kweli???Mabehewa mabovu,barabara mbovu zilizojengwa chini ya kiwango,Meli ya mwaka 1978 kununuliwa kwa bilioni 8,malipo hewa kwa wakandarasi bilioni 258,hivi vyote hivi ni Lowassa???
Ukweli unauma japo mzuri kuusema,najua Lowassa ana madhambi yake mengi,vivyo hivyo Magufuli anayomengi pia,ambayo kwa kujifunika Ngozi ya utendaji kazi,basi mnataka kufunika na uovu wake.
Sumaye kasema kila mtu afunue uovu aliotufanyia WATANZANIA ili tupate kumhukumu Lowassa.
Pole ni mwizi anayejulikana bora kuliko mwizi anayefichwa kwa jina la utendaji kazi.Maana akiingia IKULU hakika tutamalizika,ni wakati wa MABADILIKO,tunayataka si kwa hiari ya CCM bali kwa lazima..
Watanzania ndiyo tulioamua.