Mkuu
laiza mbona unachangia kwa uoga sana, hujiamini? Tuliza akili zako upate kuelewa ujumbe ninaotaka kuufikisha kwa watanzania. Haya maswali yote uliyouliza naona umejikanaganya ama kwa makusudi au kwa kutokujua:
1.
Vyanzo vya mapato vitaongezwa kwa kuzuia UFISADI wa fedha za umma tofauti na CCM wanaowatetea mafisadi kwa nguvu zao zote. Wewe hujui kwamba mabilioni ya fedha yanayopotea kila siku ni fedha za wananchi ambazo zingetumika kuwaletea maendeleo? Na je unadhani kwamba yale mabilioni ya EPA aliyoyachukua Kikwete kutoka kwa wezi wa EPA yangejenga barabara ngapi kama angeyarejesha kwa wananchi?
2.
Pesa za NSSF sio za UMMA...hizi ni fedha za wanachama zinazotumiwa vibaya kujengea miundombinu ya serikali huku wenye fedha zao hawanufaiki na kitu chochote kutokana na vitega uchumi hivyo. Huoni kwamba ni UCHIZI serikali kutegemea fedha za wanachama huku ikiwaachia wezi wanajichotea fedha za umma? Aidha NHC ni shirika la umma linalojiendesha kibiashara na nyumba wanazojenga wanakaa mafisadi huku wananchi wa kawaida wakiwa hawana mahali pa kuishi. Pia, fahamu kwamba zaidi ya 50% ya nyumba zote zilizojengwa na NHC zimeishanyakuliwa na mafisadi...wamejiuzia kwa bei ya kutupa. Ina maana hata hili hilifahamu au umeamua tu kujitoa akili?
3.
Shida ya maji nimeishaionglea kwenye uzi mama hapo juu...hebu tazama picha tu kama hujui kusoma. Unataka SHIDA hii ya maji niiongelee mara ngapi?
4.
Ni kweli kabisa kwamba haya matatizo niliyotupia humu ni machache ukilinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania. Hali ya maisha ya wananchi ni mbaya kuliko hii inayoonekana kwenye picha hapo juu. Ni juzi tu mwananchi mmoja aliamua kunadi figo lake ili apate fedha za kujikimu....hali ya maisha ya wananchi ni mabaya kuliko kawaida. Nakupongeza kwa kuuona huo ukweli. Ungana na wazalendo tukaikomboe nchi kutoka mikononi mwa mwa wakoloni weusi (CCM) mwezi wa Oktoba mwaka huu wa 2015.