LGE2024 CCM naomba tubadilike kwenye teuzi zetu kuanzia mashinani...

LGE2024 CCM naomba tubadilike kwenye teuzi zetu kuanzia mashinani...

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mbuzi mee

Senior Member
Joined
Dec 29, 2022
Posts
156
Reaction score
217
Ukweli lazima usemwe hata kama ni mchungu...mwaka huu kumekuwa na ugumu sana kwenye haya mazoezi...

Kwenye vitambulisho vya kura watu wameenda tu tokana kuaambiwa vitawasaidia kwenye shughuli nyingine km ID...
Navuta picha kubwa nin kitatokea kwenye siku za kupiga kura.

CCM naomba tubadilike kwenye teuzi zetu kuanzia mashinani...Tuna tamani serikali yetu tunayoiunda ipendwe kuanzia mashinani

Tuteue viongozi watendaji wazuri,wenye kauli nzur hata wanapoongelea mambo ya vyama vya wapinzani,wenye maono...

Wenye kujua wananchi wao wanataka nini ..
Sio viongozi wanakaa miaka ishirini na si wawajibikaji katika maeneo yao wanayogombea na kupelekea chuki kali kwa wananchi .
 
Hapo ndiyo ugomvi ulipo ukijumlisha na uendeshaji mbovu wa zoezi la upugaji kura/wizi.
 
Wanawateua watu wao kwa upendeleo kwa ajili ya kulindana. Ngazi nyingine demokrasia hakuna inatolewa fomu moja badala ya kila mwenye sifa kugombea nafasi husika.
 
Hapo ndiyo ugomvi ulipo ukijumlisha na uendeshaji mbovu wa zoezi la upugaji kura/wizi.
Kazi ipo...kauli na matendo ya viongozi yanawakatisha tamaa wananchi...Tunapoelekea zoezi litakosa uhalisia..takwimu zitapikwa kuonesha muitikio mkubwa kuanzia ngazi ya vituo vya UANDIKISHAJI
 
Mbona watu wanajiandikisha kama kawaida wewe upo marekani nini?
 
Mbona watu wanajiandikisha kama kawaida wewe upo marekani nini?
Nipo Tanzania na naonge uhalisia..... Shida ipo na inachagizwa aidha na mambo haya

1. Watu kukata tamaaa
2. Elimu na hamasa iliyotolewa haikufika vizuri juu ya umuhimu wa mazoezi haya
3. Wananchi kuchanganya zoezi la awali lililokuwa la kuandikisha vitambulisho vya mpiga kura,ambalo wengi wao wanajua bado linaendelea
 
Safari hii mchuano ni mkali sana. CCM wasibeze Vyama vingine.
 
Back
Top Bottom