CCM ndani ya viwango vya mishahara (Salary Scales) huwa mnaweka nini??

CCM ndani ya viwango vya mishahara (Salary Scales) huwa mnaweka nini??

Serikali ya fisiemu walichofanya waliondoa allowances kusomeka kwenye salary slip ili kuficha mishahara kiduchu, fikiria mshahara wa laki tatu uuainishe katika allowance zile za muhimu, mfano, nyumba, usafiri, maji, umeme......ina maana allowances peke yake zinakula mshahara mzima....hapo hatujaweka posho ya chakula unapokuwa kazini.
CCM ni matapeli haswa
 
Mada muhimu sana hii. Hakuna waziri,mbunge wala mgombea uraisi anayeweza kuhutubia kuhusu wages huwa wanakwepa hii mada sababu wanajua ina.machungu mengi.

Nashangaa takwimu zetu za uchumi huwa hawaongelei wages hata waziri Rizone toka ameingia wizarani mpaka atatoka hutosikia anaongelea wages. Sijui uchumi wa wapi usiongelea wages, employment rate, unempolyment data.
 
Watanzania wengi walioajiriwa hutazama zaidi ukubwa wa viwango vya mishahara lakini sidhani kama huwa wanahoji ndani ya viwango hivyo vya mishahara kunawekwa nini !!??

Kwa mfano labda kiwango cha mshahara kiwe ni shilingi 350,000. Je muajiri ndani ya hiyo 350,000 ameweka vitu gani na kwa mngawanyo upi? Maana kabla ya kodi haijaanza kukatwa ni vizuri mtu akajua amewekewa nini na nini kwenye mshahara wake.

Kwa mfano kwenye mshahara wa Shilingi 350,000 muajiri kakadiria huo mshahara utamudu kununua nini na nini mpaka utakapolipwa mshahara mwingine?? Kodi ya nyumba, nauli ya kukufikisha kazini na kukurudisha nyumbani, gharama za nishati, chakula?

bila ya kujua muajiri kakusudia nini kwenye mshahara anaokulipa ni kazi bure kudai nyongeza ya mshahara maana hata huo ulio nao hujui ilikuwaje muajiri wako akaamua ulipwe hivyo??

CCM mishahara ya watanzania hukokotolewa kwa kutumia kigezo gani??
Kuna mishahara ya aina mbili;
(i) Living Salary ambayo ndio inazingatia mchanganuo ulioonesha hapo juu. Mara nyingi mishahara hii inatolewa na nchi za Dunia ya Kwanza.

(ii) Basic Salary ambayo inatolewa na nchi za Dunia ya Tatu kama Tanzania.

NB: Suala la mishahara ni la kiulimwengu sio la CCM. Sidhani kama Afrika kuna nchi zaidi ya tano zenye kutoa Living Salary. Sidhani.
 
Kwa nini sisi tusiwe miongoni mwa hizo nchi tano?

Hivi kiswahili Cha "Basic salary" ni nini na kama hautojali weka tofauti kati ya hiyo living na Basic Salaries!?
 
Mtoto wa Shule ukipata nafasi naomba utoe Elimu kuhusu "Basic salary" na hiyo "Living salary".

Kama hautojali tuelimishe imekuwaje hiyo living salary haiwezekani kulipwa hapa Tanzania.

Maana Kwa mtazamo wangu ni kuwa watu wanalipwa mishahara ili waendeshee maisha yao. Kumbe kwa nchi yetu ni tofauti.
 
Nafikiri swali lingekuwa 'wanatoa nini katika mishahara?'; maana katika hiyo 350,000/= wanatoa PAYE, PSSF/NSSSF, NHIF, nk na kinachobaki ukapambanie mtaani kwa Mangi..!
 
Nafikiri swali lingekuwa 'wanatoa nini katika mishahara?'; maana katika hiyo 350,000/= wanatoa PAYE, PSSF/NSSSF, NHIF, nk na kinachobaki ukapambanie mtaani kwa Mangi..!
Kabla ya kutoa si lazima uweke? Unatoaje usipoweka?

Kama wanatoa PAYE, Social security fund, NHIF nk. Ina maana wanajua mwisho wa siku mfanyakazi anabakiwa na nini.

Sasa ukokotozi wao hutumia kigezo gani? Yaani wanaposema huu mshahara ulipwe hivi huwa wanakusudia umnufaishe mfanyakazi kivipi?
 
Mtoto wa Shule ukipata nafasi naomba utoe Elimu kuhusu "Basic salary" na hiyo "Living salary".

Kama hautojali tuelimishe imekuwaje hiyo living salary haiwezekani kulipwa hapa Tanzania.

Maana Kwa mtazamo wangu ni kuwa watu wanalipwa mishahara ili waendeshee maisha yao. Kumbe kwa nchi yetu ni tofauti.
Sawa mkubwa ntajitahidi.
 
Back
Top Bottom