CCM ndani ya viwango vya mishahara (Salary Scales) huwa mnaweka nini??

CCM ni matapeli haswa
 
Mada muhimu sana hii. Hakuna waziri,mbunge wala mgombea uraisi anayeweza kuhutubia kuhusu wages huwa wanakwepa hii mada sababu wanajua ina.machungu mengi.

Nashangaa takwimu zetu za uchumi huwa hawaongelei wages hata waziri Rizone toka ameingia wizarani mpaka atatoka hutosikia anaongelea wages. Sijui uchumi wa wapi usiongelea wages, employment rate, unempolyment data.
 
Kuna mishahara ya aina mbili;
(i) Living Salary ambayo ndio inazingatia mchanganuo ulioonesha hapo juu. Mara nyingi mishahara hii inatolewa na nchi za Dunia ya Kwanza.

(ii) Basic Salary ambayo inatolewa na nchi za Dunia ya Tatu kama Tanzania.

NB: Suala la mishahara ni la kiulimwengu sio la CCM. Sidhani kama Afrika kuna nchi zaidi ya tano zenye kutoa Living Salary. Sidhani.
 
Kwa nini sisi tusiwe miongoni mwa hizo nchi tano?

Hivi kiswahili Cha "Basic salary" ni nini na kama hautojali weka tofauti kati ya hiyo living na Basic Salaries!?
 
Mtoto wa Shule ukipata nafasi naomba utoe Elimu kuhusu "Basic salary" na hiyo "Living salary".

Kama hautojali tuelimishe imekuwaje hiyo living salary haiwezekani kulipwa hapa Tanzania.

Maana Kwa mtazamo wangu ni kuwa watu wanalipwa mishahara ili waendeshee maisha yao. Kumbe kwa nchi yetu ni tofauti.
 
Nafikiri swali lingekuwa 'wanatoa nini katika mishahara?'; maana katika hiyo 350,000/= wanatoa PAYE, PSSF/NSSSF, NHIF, nk na kinachobaki ukapambanie mtaani kwa Mangi..!
 
Nafikiri swali lingekuwa 'wanatoa nini katika mishahara?'; maana katika hiyo 350,000/= wanatoa PAYE, PSSF/NSSSF, NHIF, nk na kinachobaki ukapambanie mtaani kwa Mangi..!
Kabla ya kutoa si lazima uweke? Unatoaje usipoweka?

Kama wanatoa PAYE, Social security fund, NHIF nk. Ina maana wanajua mwisho wa siku mfanyakazi anabakiwa na nini.

Sasa ukokotozi wao hutumia kigezo gani? Yaani wanaposema huu mshahara ulipwe hivi huwa wanakusudia umnufaishe mfanyakazi kivipi?
 
Sawa mkubwa ntajitahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…