CCM ni kama ndio wenye uchu wa madaraka

CCM ni kama ndio wenye uchu wa madaraka

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Habarini wapendwa wadau wa jf.

Kiukweli kabasa chama Cha ccm kwa Sasa nchini mwetu kimegeuka kero na kinatia hasira Sana kwa maneno na matendo yao, chama hiki hakijali Tena haki za watanzania walioupande wa upinzani unafikiri Hawa si watanzania, hasa linapokuja swala la madaraka wanaona wao ndio wenye hati miliki ya kutawala milele.

Hili bunge lao la chama kimoja limegeuka mwiba kwa wananchi wanaongeza tozo Kila kukicha Tena bila hofu wananchi wanalalamika mwenyekiti wao anaiambia dunia kwamba anawashukuru watanzania kwa kuikubali tozo inatia hasira Sana.

Ccm Ni kinyonga mzee aliyechanganyikiwa, kupitwa na wakati na asiyebadilikana tena kulingana na mazingira,
Kwa miaka 60 wametawala kwa hila, uongo,uzandiki, na Kila njia Sasa wamebakiwa na njia moja TU ya kutawala kwa ubabe, ukatili na mauaji ya wazi kabisa mpaka wananchi wa kawaida kabisa wanaona

Wananchi wanadai katiba toka miaka ya 90s na wamepitia michakato mingi na gharama kubwa sana, mpaka kufikia kukusanya maoni na kutengenezwa kwa rasimu ya katiba Leo anatokea mhuni mmoja anasema katiba si hitaji la wananchi duu!.

Wanadai Ni hitaji la wanasiasa wenye uchu wa madaraka, pengine Ni Mimi nisiyeelewa dhana ya uchu wa madaraka lakini Kuna swali dogo hapa,
(1) kwani kuwania madaraka katika nchi yetu Ni kosa?
(2) Kati ya anayezuia katiba mpya ili yeye abaki madarakani na ametawala kwa miaka 60 na yule anayetaka katiba Ili aingie madarakani na hajawahi kutawala hata sekunde 60 Ni Nani mwenye uchu wa madaraka?

CCM mmepitwa na wakati jirekebisheni muendane na Zama hizi tofauti na hapo mtakuwa vituko na watalii wataanza kuja Tanzania kutazama mgando wenu wa fikra.

pia kumbukeni katiba mpya Ni lazima ipatikane mtake msitake mda haupo upande wenu Sasa na vyama vya upinzani wanaipenda Sana hii kwani wamefikishwa kwenye maumivu,mateso na mauaji lakini bado wanatumia njia za kiungwana kudai haki zao

Wapinzani wa kweli endeleeni kuionyesha dunia na kuishawishi jumuiya ya kimataifa kuuona huu ukatili na Nina Imani wakishawishika ccm itasambaratika yenyewe maana ni wanafiki na waoga kuliko hata uoga wenyewe.

Hii ndio njia pekee ya amani ya kuweza kufikia malengo yenu bila kuwadhuru watanzania
Njia hii ikishindikana hakutakuwa na njia nyingine Tena zaidi ya jino kwa jino na hapo ndipo point ya mwisho wanayoisubiri ccm.

😁😁😁😁 Ni chalii wa ighanuda hapa😎😎😎😎
 
Viongozi wa CCM wamejimilikisha nchi! Lakini ipo siku isiyo na jina viongozi na familia zao watalia na kusaga meno!
 
Hivi upinzani wakichukua nchi kwa katiba hii ccm watakuwa na hali gani?
 
Viongozi wa CCM wamejimilikisha nchi! Lakini ipo siku isiyo na jina viongozi na familia zao watalia na kusaga meno!
Kuwaelewa CCM na ndoto yao ya maendeleo ya vitu vingi,vikubwa au vya kwanza na mfano.Kama ni daraja lazima liwe kubwa,kama ni elimu tunahesabu madarasa,matundu ya vyoo,wanafunzi wengi kuandikishwa,kufaulu bila vitabu,waalimu na madawati etc.Kila kitu ni cha ajabu na chaweza kuwa kivutio cha utalii/maajabu ya dunia.Only in Tanzania.Nchi mbili zinaungana,moja inafahamika Bali nyingine imejikana hata jina na kujivika koti la muungano.
Kiujumla:Bila Katiba Mpya ya Wananchi CCM haiwezi kwa vyovyote kuiendeleza nchi hii.Wamekuwa na tamaa ya madaraka na wamejawa na hofu ya kushtakiwa kwa maovu waliyowatenda Watanzania kwa miaka na mikaka.
Let's Stand for Our Rights in a Brand New Constitution,we are done with CCM's blah blah blah.
 
Habarini wapendwa wadau wa jf.

Kiukweli kabasa chama Cha ccm kwa Sasa nchini mwetu kimegeuka kero na kinatia hasira Sana kwa maneno na matendo yao, chama hiki hakijali Tena haki za watanzania walioupande wa upinzani unafikiri Hawa si watanzania, hasa linapokuja swala la madaraka wanaona wao ndio wenye hati miliki ya kutawala milele.

Hili bunge lao la chama kimoja limegeuka mwiba kwa wananchi wanaongeza tozo Kila kukicha Tena bila hofu wananchi wanalalamika mwenyekiti wao anaiambia dunia kwamba anawashukuru watanzania kwa kuikubali tozo inatia hasira Sana.

Ccm Ni kinyonga mzee aliyechanganyikiwa, kupitwa na wakati na asiyebadilikana tena kulingana na mazingira,
Kwa miaka 60 wametawala kwa hila, uongo,uzandiki, na Kila njia Sasa wamebakiwa na njia moja TU ya kutawala kwa ubabe, ukatili na mauaji ya wazi kabisa mpaka wananchi wa kawaida kabisa wanaona

Wananchi wanadai katiba toka miaka ya 90s na wamepitia michakato mingi na gharama kubwa sana, mpaka kufikia kukusanya maoni na kutengenezwa kwa rasimu ya katiba Leo anatokea mhuni mmoja anasema katiba si hitaji la wananchi duu!.

Wanadai Ni hitaji la wanasiasa wenye uchu wa madaraka, pengine Ni Mimi nisiyeelewa dhana ya uchu wa madaraka lakini Kuna swali dogo hapa,
(1) kwani kuwania madaraka katika nchi yetu Ni kosa?
(2) Kati ya anayezuia katiba mpya ili yeye abaki madarakani na ametawala kwa miaka 60 na yule anayetaka katiba Ili aingie madarakani na hajawahi kutawala hata sekunde 60 Ni Nani mwenye uchu wa madaraka?

CCM mmepitwa na wakati jirekebisheni muendane na Zama hizi tofauti na hapo mtakuwa vituko na watalii wataanza kuja Tanzania kutazama mgando wenu wa fikra.

pia kumbukeni katiba mpya Ni lazima ipatikane mtake msitake mda haupo upande wenu Sasa na vyama vya upinzani wanaipenda Sana hii kwani wamefikishwa kwenye maumivu,mateso na mauaji lakini bado wanatumia njia za kiungwana kudai haki zao

Wapinzani wa kweli endeleeni kuionyesha dunia na kuishawishi jumuiya ya kimataifa kuuona huu ukatili na Nina Imani wakishawishika ccm itasambaratika yenyewe maana ni wanafiki na waoga kuliko hata uoga wenyewe.

Hii ndio njia pekee ya amani ya kuweza kufikia malengo yenu bila kuwadhuru watanzania
Njia hii ikishindikana hakutakuwa na njia nyingine Tena zaidi ya jino kwa jino na hapo ndipo point ya mwisho wanayoisubiri ccm.

😁😁😁😁 Ni chalii wa ighanuda hapa😎😎😎😎
CCM haipo tena imebaki chama cha kina Siro na wale wengine wavaa Kaunda
 
Back
Top Bottom