CCM ni 'nambari one' katika nini?

CCM ni 'nambari one' katika nini?

Kwa fikra kama hizi nitaendelea kuwepo CCM sana tu, iwapo hizi ni fikra mbadala nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM daima.
Hebu get serious kidogo gavana hiyo ndio njia sahihi? hivi wazo lenu kuu ni kuing'oa tu CCM madarakani na mtafanya hivyo kwa kuorodhesha mabaya ya CCM bila hata kuonesha mbadala wa sera au muono wenu?
Ingekuwa ni kampuni basi CCM ingekwisha tangazwa kwamba ni "Mufilisi" na wale wote wanaoidai wasamehe madeni yao kwakuwa kampuni haina chochote cha kuwalipa na deni lake halilipiki kabisa, ama ingekuwa ni moja ya mashirika ya umma ingebidi ibinafsishwe na kutafutiwa tajiri wa kuinunu mara moja. Wala CCM hawana mpango wowote kwa ajili ya wananchi, hata mtu akiwauliza sasa wako madarakani kufanya nini na kwaajili ya nani, bila shaka jibu lake litakuwa kwamba tuko madarakani kwa sababu madaraka ni matamu. Wala hawana kile walichozea kuita mshikamano kwani kila mmoja yuko madarakani kwasababu zake binafsi.


KUNA wengine wapo madarakani ili kulinda utajiri wao maana siku watakapoachia madaraka utakuwa ndio mwanzo wa kufilisika kwakuwa ni madaraka ndiyo yaliyowatajirisha na siyo bidii ya kazi na maarifa ya kuutafuta utajiri.
Kuna wengine wamefanya makosa mengi ya jinai kiasi kwamba wanaogopa siku ya kuachia madarakal abda watashitakiwa, ndiyo maana wakati mwingine wamediriki kutunga miswada kwa madhumuni ya kuweka sheria za kujihami wasifikishwe mahakamani baada ya kuachia ngazi.
Kuna wengine ambao kwasababu ya ulevi tu na kula huduma kwenye madaraka kwa muda mrefu wamelemaa kiasi cha kuona haya kuishi bila ya wadhifa wowote, hawa ndio wenye ndoto za kufia madarakani kama walizokuwa nazo akina Idd Amin, Mathias Nuema, Bedel Bokasa, Kamuzu Banda, Mobutu Sese Seko na wale waliojiita "rais wa maisha."
Hapa Tanzania wapo "Mawaziri wa Maisha", "Wabunge wa maisha", "mabalozi wa maisha" n.k. Hawa hawawezi kupisha damu mpya, au kizazi kipya hadi kifo kitakapowatenganisha na madaraka yao. Pamoja na kwamba mkusanyiko wao ni katika msingi wa ubinafsi wa kila mtu na wake, lakini bado katika ubinafsi wao CCM wanaunganishwa na neno moja kuu nalo ni nguvu za dola.
Tumaini lao lote ni katika mapolisi na magereza. Siyo siri kwamba CCM imelipindua jeshi la Polisi na kuligeuza kuwa jeshi la kichama ambalo liko kulinda maslahi ya Chama Cha Mapinduzi, na siyo maslahi ya raia. Sababu za Polisi kuuvaa U-CCM ziko nyingi na nitazieleza kwa ufasaha katika toleo lijalo. Ili kulinda maslahi ya Chama Cha Mapinduzi inabidi Polisi ipambane na yeyote yule atakayejionyesha kuleta upinzani dhidi ya CCM na hasa ule upinzani makini unaoelekea kuing'oa CCM madarakani.
Siku za nyuma upinzani ulipojitokeza kwa waandishi wa habari ambao kalamu zao zilikuwa hazichoki kuandika mabaya ya watawala, mapambano kati ya Polisi na wanahabari yalikuwa makali na ya mara kwa mara, wengi bado wanakumbuka sakata za Polisi kuwapiga virungu waandishi na kunyang'anya kamera zao au kuziharibu.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wamepamba moto kuendesha kampeni za kashfa, kejeli na matusi dhidi ya wananchi, wanaojaribu kuwazindua wananchi wenzao, juu ya umuhimu wa kuchagua viongozi bora, pamoja na baadhi ya vyama vya upinzani, hasa vile vinavyoonekana kuwa sasa, vinakubalika na wananchi wengi.
Vitisho na kejeli, ni sera ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, nina kumbuka tukio la mwezi wa Agosti mwaka 1999 wakati wabunge halipokuwa wanajadili makadirio ya fedha ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa mwaka huo, ambapo niliachwa hoi.
Mbunge wa Mtera, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mhe. John Malecela,alisimama na kuwataka Wapemba, waache kujishughulisha na mambo ya siasa, na warudi Chake Chake, kuuza mchele na kanga."
Japo kuwa maneno hayo, yalikuwa ni ya kibaguzi,yaliyojaa chuki na uchochezi, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, kama ilivyokawaida yao walishangilia kwa makofi na vicheko.
Cha kushangaza ni kwamba, Mzee Malecela alipandisha jazba, baada ya Mbunge wa Vitongoji Mhe. Nassoro Juma, kueleza kwamba, njia pekee ya kupata aina ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, unaofaa ni kwa wananchi kupiga kura ya maoni.
Kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake, tofauti za maoni na upinzani wa kisiasa ni uadui kati ya mtu na mtu, au chama na chama kingine, inatisha.
Inapofika wakati wa maandalizi ya kupata kula, mipaka hutoweka, wapiga debe, hupasha mikwasa moto.
Demokrasia ndani ya chama, ni jambo lisilokubalika ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni hii ndio sababu, hata chaguzi zinazofanywa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, mara nyingi ni za mizengwe mizengwe, na ghilba tupu.
Mara zote, nia ya wagombea huwa ni kupata madaraka na sio kuongoza kwa sera za kuinua wananchi.
Ndio sababu hata sera iliyokiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani , imeachwa, kwa maelezo kwamba haitekelezeki.
Yote haya yanafanyika katika mazingira ya kudumaa kwa maendeleo ya nchi, kielimu na kiuchumi.
Katika taarifa ya Benki ya Dunia na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Watoto(UNICEF) ya mwaka 1999, umeelezwa kwamba, asilimia 50 ya familia hapa nchini, ni maskini, na asilimia 36 kati ya familia hizo, haziwezi kumudu mahitaji muhimu yanayotambuliwa na jamii.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba, watoto wanaoingia shule wamepungua sana, zaidi ya watoto milioni 2,000,000 wanaopaswa kwenda shule, hawapelekwi.
Kwa takwimu hizo, Tanzania iko nyuma mno kielimu, ikilinganishwa na Uganda, Kenya na Ethiopia. Hali hii inazidi kuwa mbaya hata hii leo
Kwa viongozi wa Chama Cha Mainduzi, hili si jambo la kutisha linalostahili kutengenezewa mikakati maana wao wanaouwezo wa kupeleka watoto wao nje kwa masomo ili kesho na kesho kutwa waje kurithi madaraka ya baba zao.
Wananchi, tunatakiwa kuzingatia mambo yote haya, wakati wa kupiga kura mwezi Oktoba mwaka huu, ili kwa nguvu zetu, ambazo ni utashi na kura zetu, tukiondoe Chama Cha Mainduzi madarakani, na kukipa chama kingine hatamu ya uongozi wa nchi yetu, kwa matumaini kwamba tutapata maendeleo tunayoyataka.
Kukirudisha Chama Cha Mapinduzi madarakani, ni kukubali kuwa thamani ya maisha yetu ni, pilau, vikoi na kanga, kama Mheshimiwa Mangula,Katibu Mkuu wa CCM, alivyowahi kusema. Je,tuko tayari kuendelea kunyanyaswa kwa karamu za pilau na vikoi?
 
Badala ya kutoa tafsiri- dhania..kwani wenyewe haingii humu wakatoa tafsiri yao?
 
Kwa fikra kama hizi nitaendelea kuwepo CCM sana tu, iwapo hizi ni fikra mbadala nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM daima.
Hebu get serious kidogo gavana hiyo ndio njia sahihi? hivi wazo lenu kuu ni kuing'oa tu CCM madarakani na mtafanya hivyo kwa kuorodhesha mabaya ya CCM bila hata kuonesha mbadala wa sera au muono wenu?

Alaa?
CCM nambari one kwa lipi mkuu Burn?
 
Nambari one ni CCM kwa kuwa ndio chama pekee kilichoongoza toka uhuru hadi leo, na hadi sijui lini. Vile vile chama ambacho kina nguvu kuliko vyama vingine vya siasa kwa Tanzania.
Ila kuhusu ufisadi, sidhani kama ndio ni CCM tu. Kila sector bongo ni fisadi tu iwe ya serikali au private sector wote ni fisadi tu.
 
Mpende msipende, mtake msitake ni lazima nitashinda
Mnamo 1995, mgombea mmoja wa kiti cha Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi alifika eneo fulani ambapo aliarifiwa kwamba watu wa eneo hilo karibu wote ni wapinzani na kwamba wamedhamiria kumpa mgombea wa NCCR kura zao. Mara aliposimama kujinadi, badala ya kunadi sera, au sifa zake na mema aliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano ya Ubunge wake, mgombea huyo akatoa "nyodo" ya kufunga milenia, akawaambia wananchi "nasikia hapa ndio ngome kuu ya NCCR sasa nawaambia ya kwamba mpende msipende, mtake msitake, ni lazima nitashinda. Mpige kura au msipige kura mimi bado nitakuwa mbunge tu." Kisha akashuka toka jukwaani kwa jeuri na mikogo, akapanda gari akaondoka na kuwaacha waungwana wakiwa wameduwaa huku baadhi ya wananchi wachache bila shaka washabiki wa CCM wakisema "leo nimeipata freshi yake."
Nimeyatoa maneno hayo kama mfano hai wa kuthibitisha tatizo lililopo kwa Watanzania, maneno yenye "utemi", "ufedhuli", na "ubinafsi" uliokithiri yanapotoka kwenye kinywa cha mtawala au kiongozi, kwenda kwa wapiga kura au watu wanaoongozwa, basi hapo tatizo siyo huyo "mtu mwovu" bali tatizo halisi ni huo "mfumo mwovu" unaotumika hadi kuwapata watawala wa aina hii. Siku zote. Watawala wabaya au kwa lugha nyingine viongozi wabovu huwa hawashuki toka mbinguni wala hawajiweki wenyewe madarakani, bali huwa wanawekwa na watu kupitia mfumo ambao watu wamekubaliana nao kwamba huu ndio utaratibu wetu wa kuwapata viongozi wetu na watawala wa nchi.
Sasa mfumo mwovu ni lazima utatoa au utazaa viongozi waovu, sawa na mti mbaya unavyozaa matunda mabaya. Wengi wetu huwa tunaishia kuona ubaya wa mtu binafsi na kuujadili huku tukiufunika kabisa (overlook) ubaya wa mfumo. Huwa tu nashindwa kuona kwamba kiongozi mbovu ni zao au tunda la mfumo wetu, na kwahiyo tunapaswa kuujadili mfumo na kuuchukia kabla ya kumchukia mtu binafsi. Matokeo ya upofu wa kutokuuona uovu ndani ya mfumo yamekuwa ni utamaduni uliopo sasa wa kubadilisha watu mmoja baada ya mwingine yaani anatoka "mbovu huyu" na anaingia "mbovu yule" hadi wengine wanafikia hatua ya kukata tamaa kwamba haiwezekani kupata uongozi bora kumbe sababu yake ni ule ukweli kwamba utaratibu wetu wa kuwapata viongozi ndio haufai na kwahiyo hatuwezi kuwaepuka viongozi wasiofaa kwa kuwa chimbuko lao ni huo mfumo usiofaa, mfumo unaopaswa kuzikwa kama mzoga.
Tuchukulie mfano hai wa huyu mbunge jeuri anayetembeza utemi hata siku ya kampeni, je, tumaini lake ni nini? Ni wazi kwamba tumaini lake siyo hizo kura za wananchi wa jimbo lake bali ni CCM na zile mbinu zake au mbinu zao CCM ambazo wana hakika nazo kwamba hata kama watu wote watasusa kupiga kura bado mtu wao atashinda tu. Hata kama mtu wao atachukiwa hiyo ni kazi bure kwani bado atashinda tu. Hata kama atazembea kwenye kipindi chote cha miaka mitano ya uongozi wake bado atashinda tu, maana kinachomwezesha kushinda siyo hizo kura za wapiga kura bali ni "mbinu", uwongo na udanganyifu ambao kwa lugha nyingine unaitwa "rigging."
Mnamo mwaka 1995, CCM walifanya "rigging" ya hali ya juu kwa kuwatumia usalama wa Taifa na wakurugenzi wa Wilaya ambao walifanywa kwa makusudi wawe Returning Officers au Wasimamizi wa Uchaguzi na waliweza kuchezea matokeo kama walivyotaka wao. Kwa ,mfano katika kituo kimoja kwenye jimbo langu la uchaguzi la Mpwapwa, kulikuwa na kituo kimoja cha wapiga kura 300, baada ya zoezi la upigaji kura kwisha, ni watu 285 ndio walipiga kura na katika kura hizo mgombea wa kiti cha Urais wa NCCR-Mageuzi wa wakati huo Bw. Mrema alipata 0.
Baada ya matokeo kubandikwa watu walianza kujiuliza ina maana hata wakala wa Mrema hakumpigia kura? Mmoja akasema mimi nawahakikishia kwamba kura yangu nimempa Mrema, mara ghafla ukatokea kama mkutano wa hadhara watu wengi waliopiga kura pale kwenye kituo hicho wakajitokeaza kukiri hadharani kwamba walimpa "tik" Mrema, wakajihesabu hadi wakafika 160 wakaamua kuandamana hadi Wilayani lakini kwa bahati mbaya wakafika siku ya tatu na kuambiwa na msimamizi (Mkurugenzi wa Wilaya) kwamba tayari kura zimeshajumlishwa na wala zoezi haliwezi kurudishwa nyuma na kuanza tena kuhesabu kura upya ili kuhakiki nani kapata ngapi, zaidi ya yote masanduku yameshachanganywa.
Katika hatua nyingine msimamizi msaidizi mmoja akawasilisha matokeo yake kwamba mgombea wa kiti chaUrais wa Chama cha TADEA amepata kura nne na kumfanya mkurugenzi huyo awe hoi kiasi cha kumhoji hizo kura za Rais wa TADEA ziko wapi kwani TADEA HAIKUWA IMEWEKA MGOMBEA! Masanduku yalipofunguliwa ikadhihirika kwamba hakuna kura yoyote kwa rais wa CCM alikuwa amezidishiwa kura 26. Hapo ndipo nilipobaini kwamba kumbe matokeo yote yanayowasilishwa pale na wasimamizi wasaidizi ni kitu cha kubuni tu, hizo tarakimu zote ni za kupanga nani apate ngapi, na nani awe mshindi.
Chini ya mfumo wa namna hii au utaratibu wa jinsi hii tunaweza kuona ni kwanini mgombea anaweza kudiriki kuwatamkia watu maneno yenye fedhuli kiasi hicho kwamba Mpende Msipende, Mtake Msitake bado mimi ni mshindi. Mpige kura msipige bado nitakuwa mbunge! Wabunge wanaochaguliwa na Usalama wa Taifa ni kweli watakuwa na mzigo wowote wa bungeni kutetea matakwa ya Serikal?
Nasikia mwaka huu utawala wa Mkapa umeagiza kwamba jimbo lolote ambalo CCM itapoteza basi afisa usalama wa wilaya na mkuu wa wilaya watapoteza kazi. Sasa kuna swali jingine kuu la kujiuliza, nalo ni kwamba nchi ambayo viongozi wake wanapatikana kimizengwe namna hii, kweli inaweza kupata maendeleo? Watu tusiishie kuufananisha uchaguzi wetu na ule wa Wamarekani au nchi zingine zilizoendelea ambapo wagombea hupeana mikono ya pongezi na kutakiana heri baada ya kutangazwa nani mshindi na nani mshindwa, kwani uchaguzi wetu watawala wameufanya kuwa "drama", uchaguzi wetu ni sawa kabisa na mchezowa kuigiza. Uchaguzi mkuu unapogeuka kuwa sawa na mchezo wa TAUSI na akina Bishanga, tutarajie nini katika nchi hiyo?
Ni wazi kwamba kila neno litafanywa kwa namna ya kuigiza, viongozi wataigiza kana kwamba wanaongoza. Wafanyakazi nao wataigiza kana kwamba wanafanya kazi kumbe hakuna kinachofanyika. Wanafunzi wataigiza kana kwamba wanasoma kumbe hali yao ikilinganishwa na wanafunzi wa nchi nyingine wa kwetu ni kama wanakwenda shuleni kupoteza muda, na baada ya miaka saba wanatunukiwa vyetiv ya kuhitimu elimu ya msingi huku wakiwa hawana msingi wowote wa elimu wala kisomo, kwani misingi yote ya elimu imekwisha bomolewa.
Wakulima nao wataigiza kana kwamba wanalima kumbe mtu makini akitazama anaona ni kichekesho, kwani hakuna kilimo na kwa hiyo atacheka na kusema ngoja tuone mwisho wake. Kweli mwisho wa yote, ni nchi kugeuka kuwa nchi yenye njaa kila mwaka na taifa omba omba wa chakula toka mataifa mengine. Nchi iliyotangaza kwamba siasa yake ni ya ujamaa na kujitegemea na dunia nzima ikaielewa hivyo lakini kinyume chake ikawa nchi tegemezi yenye kuagiza chakula toka nchi zingine wakati yenyewe ina ardhi yake, maji yake, na wakulima wake, hicho ni kitendawili kama siyo mzaha!
Inabidi wananchi tujiulize Je, huo sio utani? Ama tusema ni mchezo wa kuigiza ambao lengo lake ni kuwapa watu burdani? TX mmoja aliyepata kufanya kazi Tanzania miaka ya 1980 aliwahi kusema "In Tanzania the workers pretend to work and the employers pretend to pay." Akiwa na maana katika Tanzania, wafanyakazi hujifanya kufanya kazi na waajiri wao nao hujifanya kulipa mishahara.
Ukweli ni kwamba, wenye kazi hawafanyi kazi na hicho wanacholipwa hakistahili kuitwa mishahara. Kwasababu haitoshi kuwafanya watu waishi, na kwa kuwa kipato halali hakitoshi basi pengo lake ni lazima lizibwe na kipato cha haramu. Hapo ndipo muungwana anapolazimishwa kula haramu ili aweze kuishi, kwa sababu mfumo wa maisha haumwezeshi kuishi kwa kipato halali. Hawezi kusomesha watoto kwa mshahara wa kuigiza, wala hawezi kujitibu au kutibu familia kwa mshahara wa kuigiza, wala hawezi kumudu gharama za maisha zinazopanda kila mara kwa mshahara wa kuigiza.
Kumbe mlalahoi afanye nini? Jibu lililo wazi ni rushwa. Utawala wa CCM hauwezi kuondoa rushwa badala yake utawala ndio unaolazimisha hata wasiopenda rushwa, waitafute kwa udi na uvumba ili kunusuru maisha yao. Vinginevyo mtu anayelipwa mshahara wa kuigiza yaani mshahara wa kumwezesha kutumia kwa siku kumi tu, akiridhika nao ni wazi kwamba atakufa kabla ya kuufikia mwisho wa mwezi.
Sasa ni nani aliye tayari kuwa mwaminifu hadi kufa? Ni mfanyakazi gani atakayekuwa tayari kusema ee Mungu ipokee roho yangu, ninakufa kwasababu serikali ya CCM haikunipa malipo ya haki kuniwezesha kupata ugali? Ni mkulima gani atakayekuwa tayari kusema ee Mwenyezi Mungu ipokee roho yangu, nina kufa kwasababu Serikali ya CCM imekopa mazao yangu? Ukweli ni kwamba hakuna mtu aliye tayari kuachia maisha yake kirahisi hivyo, ni lazima atafanya kila awezalo. Kwa vyovyote vile utawala wa CCM ukubali, usikubali bado ukweli uko pale pale kwamba ndio umewafanya watu kuwa "corrupt" baada ya kuua morali za watu na kuziba kabisa njia za kupata na kuishi kwa halali
 
Mpende msipende, mtake msitake ni lazima nitashinda
Mnamo 1995, mgombea mmoja wa kiti cha Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi alifika eneo fulani ambapo aliarifiwa kwamba watu wa eneo hilo karibu wote ni wapinzani na kwamba wamedhamiria kumpa mgombea wa NCCR kura zao. Mara aliposimama kujinadi, badala ya kunadi sera, au sifa zake na mema aliyoyafanya katika kipindi cha miaka mitano ya Ubunge wake, mgombea huyo akatoa "nyodo" ya kufunga milenia, akawaambia wananchi "nasikia hapa ndio ngome kuu ya NCCR sasa nawaambia ya kwamba mpende msipende, mtake msitake, ni lazima nitashinda. Mpige kura au msipige kura mimi bado nitakuwa mbunge tu." Kisha akashuka toka jukwaani kwa jeuri ................................

Hii kali.
Amakweli CCM ni nambari wani kwa .........................................
 
CCM = Chama Cha Majambazi (ditto...)

CCM= Chukua Chako Mapema (chenge,rostam,karamagi...etc)

CCM= Chama Cha Mabwege (watanzania sio mabwege tena.. mwakyembe)

CCM= Chama Cha Mafisadi (lowasa,karamagi.....ben)

CCM= Chama cha Mapambano ( pemba...rorya...etc)
 
Kwanini wafanikiwe kila uchaguzi?
Inawezekana kuiba kila wakati?

Uwezekano ni mkubwa sana, hasa kama mlinzi ni mtu wako au mwajiriwa wako. Tanzania mtu hapewi nafasi yoyote ile iwe ya Ukuu wa wilaya, mkoa, ukurugenzi(DPP, Director of TAKUKURU), ukatibu wa wizara, Usalama wa taifa, ukuu wa polisi, ukuu wa majeshi, uenyekiti wa tume ya uchaguzi, ukurugenzi wa tume ya uchaguzi, Usimamizi wa uchaguzi, usajili wa vyama, ujaji, etc etc etc. Kama huna kadi ya CCM na kuonesha upo kwa ajili ya CCM. Sasa hawa wote ndiyo walinzi wa haki na utaratibu wa demokrasia na maendeleo ambao wanamtumikia mama yao CCM. Unatarajia CCM ishindwe uchaguzi halafu wao wakale wapi?, kinachofanyika hapo ni kuhakikisha CCM inashinda "KWA VYOVYOTE" ILI waendelee na ulaji wao kwani kikiingia chama kingine nani anajua kuwa atabaki na nafasi yake.

Ushahidi wa kujua kuwa bila kuwa CCM hujapata kazi ya juu serikalini angalieni jamaa wanapostaafu wanakimbilia ubunge wa CCM (Mboma, Mahita, Tibaigana, Masilingi(alikuwa jaji huyu)). Kweli kuna uwezekano wa wananchi kuchagua viongozi wao au kuchaguliwa na hawa niliowataja?. Ndiyo maana tunasema "CCM NI WEZI WA KURA" Na watu makini wanalijua hilo.
 
CCM ni baba yao wote.
Chadema hoi,
NCCR patupu,
CUF hakuna kitu.
CCM Nambari one eeeee,
 
CCM ni baba yao wote.
Chadema hoi,
NCCR patupu,
CUF hakuna kitu.
CCM Nambari one eeeee,

OMEGA,
Wewe ni mgeni wa siasa hapa TZ?
Mimi nitakisemea tu hiki chama CHADEMA.
Je huna habari kuwa CHADEMA ndo inatarajiwa kuongoza nchi baada ya uchaguzi mkuu mwakani?
Uko wapi wewe?
 
Mfumwa nimekuaminia mkuu, watu kama ninyi wenye data ndio tunawataka, asante mkuu
 
Mfumwa nimekuaminia mkuu, watu kama ninyi wenye data ndio tunawataka, asante mkuu

ROBIN,
Kuna watu wenye data si utani.
Naona wanaichambua CCM sana'
Tarajia mengi kama haya ya Mfumwa hapa hapa.
 
Ya kwanza kuinua elimu kama hivi

WANAFUNZI12.jpg
Kidumu chama cha mapinduzi!
 
RAMBIRAMBI YA MSIBA WA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA IDODI - IRINGA

Chama Cha Mapinduzi kimestushwa na kusikitishwa sana na vifo vya wanafunzi kumi na wawili na wengine wengi kuumia kutokana na ajali ya moto uliounguza bweni lao. CCM inaungana na wazazi, wanandugu na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika Taifa letu. Aidha CCM inaishukuru Serikali, wazazi wa watoto, uongozi wa Shule, Wauguzi na Madaktari kwa hatua zote zilizochukuliwa kuwahudumia wanafunzi walioumia na kuandaa mazishi ya heshima kwa vijana waliopoteza maisha.
 
CCM nambari wani kusajiliwa
CCM nambari wani kuiba kura
CCM nambari wani kwa Ufisadi
 
Back
Top Bottom