Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Ingekuwa ni kampuni basi CCM ingekwisha tangazwa kwamba ni "Mufilisi" na wale wote wanaoidai wasamehe madeni yao kwakuwa kampuni haina chochote cha kuwalipa na deni lake halilipiki kabisa, ama ingekuwa ni moja ya mashirika ya umma ingebidi ibinafsishwe na kutafutiwa tajiri wa kuinunu mara moja. Wala CCM hawana mpango wowote kwa ajili ya wananchi, hata mtu akiwauliza sasa wako madarakani kufanya nini na kwaajili ya nani, bila shaka jibu lake litakuwa kwamba tuko madarakani kwa sababu madaraka ni matamu. Wala hawana kile walichozea kuita mshikamano kwani kila mmoja yuko madarakani kwasababu zake binafsi.Kwa fikra kama hizi nitaendelea kuwepo CCM sana tu, iwapo hizi ni fikra mbadala nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM daima.
Hebu get serious kidogo gavana hiyo ndio njia sahihi? hivi wazo lenu kuu ni kuing'oa tu CCM madarakani na mtafanya hivyo kwa kuorodhesha mabaya ya CCM bila hata kuonesha mbadala wa sera au muono wenu?
KUNA wengine wapo madarakani ili kulinda utajiri wao maana siku watakapoachia madaraka utakuwa ndio mwanzo wa kufilisika kwakuwa ni madaraka ndiyo yaliyowatajirisha na siyo bidii ya kazi na maarifa ya kuutafuta utajiri.
Kuna wengine wamefanya makosa mengi ya jinai kiasi kwamba wanaogopa siku ya kuachia madarakal abda watashitakiwa, ndiyo maana wakati mwingine wamediriki kutunga miswada kwa madhumuni ya kuweka sheria za kujihami wasifikishwe mahakamani baada ya kuachia ngazi.
Kuna wengine ambao kwasababu ya ulevi tu na kula huduma kwenye madaraka kwa muda mrefu wamelemaa kiasi cha kuona haya kuishi bila ya wadhifa wowote, hawa ndio wenye ndoto za kufia madarakani kama walizokuwa nazo akina Idd Amin, Mathias Nuema, Bedel Bokasa, Kamuzu Banda, Mobutu Sese Seko na wale waliojiita "rais wa maisha."
Hapa Tanzania wapo "Mawaziri wa Maisha", "Wabunge wa maisha", "mabalozi wa maisha" n.k. Hawa hawawezi kupisha damu mpya, au kizazi kipya hadi kifo kitakapowatenganisha na madaraka yao. Pamoja na kwamba mkusanyiko wao ni katika msingi wa ubinafsi wa kila mtu na wake, lakini bado katika ubinafsi wao CCM wanaunganishwa na neno moja kuu nalo ni nguvu za dola.
Tumaini lao lote ni katika mapolisi na magereza. Siyo siri kwamba CCM imelipindua jeshi la Polisi na kuligeuza kuwa jeshi la kichama ambalo liko kulinda maslahi ya Chama Cha Mapinduzi, na siyo maslahi ya raia. Sababu za Polisi kuuvaa U-CCM ziko nyingi na nitazieleza kwa ufasaha katika toleo lijalo. Ili kulinda maslahi ya Chama Cha Mapinduzi inabidi Polisi ipambane na yeyote yule atakayejionyesha kuleta upinzani dhidi ya CCM na hasa ule upinzani makini unaoelekea kuing'oa CCM madarakani.
Siku za nyuma upinzani ulipojitokeza kwa waandishi wa habari ambao kalamu zao zilikuwa hazichoki kuandika mabaya ya watawala, mapambano kati ya Polisi na wanahabari yalikuwa makali na ya mara kwa mara, wengi bado wanakumbuka sakata za Polisi kuwapiga virungu waandishi na kunyang'anya kamera zao au kuziharibu.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, wamepamba moto kuendesha kampeni za kashfa, kejeli na matusi dhidi ya wananchi, wanaojaribu kuwazindua wananchi wenzao, juu ya umuhimu wa kuchagua viongozi bora, pamoja na baadhi ya vyama vya upinzani, hasa vile vinavyoonekana kuwa sasa, vinakubalika na wananchi wengi.
Vitisho na kejeli, ni sera ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, nina kumbuka tukio la mwezi wa Agosti mwaka 1999 wakati wabunge halipokuwa wanajadili makadirio ya fedha ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, kwa mwaka huo, ambapo niliachwa hoi.
Mbunge wa Mtera, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mhe. John Malecela,alisimama na kuwataka Wapemba, waache kujishughulisha na mambo ya siasa, na warudi Chake Chake, kuuza mchele na kanga."
Japo kuwa maneno hayo, yalikuwa ni ya kibaguzi,yaliyojaa chuki na uchochezi, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, kama ilivyokawaida yao walishangilia kwa makofi na vicheko.
Cha kushangaza ni kwamba, Mzee Malecela alipandisha jazba, baada ya Mbunge wa Vitongoji Mhe. Nassoro Juma, kueleza kwamba, njia pekee ya kupata aina ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, unaofaa ni kwa wananchi kupiga kura ya maoni.
Kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake, tofauti za maoni na upinzani wa kisiasa ni uadui kati ya mtu na mtu, au chama na chama kingine, inatisha.
Inapofika wakati wa maandalizi ya kupata kula, mipaka hutoweka, wapiga debe, hupasha mikwasa moto.
Demokrasia ndani ya chama, ni jambo lisilokubalika ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ni hii ndio sababu, hata chaguzi zinazofanywa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, mara nyingi ni za mizengwe mizengwe, na ghilba tupu.
Mara zote, nia ya wagombea huwa ni kupata madaraka na sio kuongoza kwa sera za kuinua wananchi.
Ndio sababu hata sera iliyokiweka Chama Cha Mapinduzi madarakani , imeachwa, kwa maelezo kwamba haitekelezeki.
Yote haya yanafanyika katika mazingira ya kudumaa kwa maendeleo ya nchi, kielimu na kiuchumi.
Katika taarifa ya Benki ya Dunia na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Watoto(UNICEF) ya mwaka 1999, umeelezwa kwamba, asilimia 50 ya familia hapa nchini, ni maskini, na asilimia 36 kati ya familia hizo, haziwezi kumudu mahitaji muhimu yanayotambuliwa na jamii.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba, watoto wanaoingia shule wamepungua sana, zaidi ya watoto milioni 2,000,000 wanaopaswa kwenda shule, hawapelekwi.
Kwa takwimu hizo, Tanzania iko nyuma mno kielimu, ikilinganishwa na Uganda, Kenya na Ethiopia. Hali hii inazidi kuwa mbaya hata hii leo
Kwa viongozi wa Chama Cha Mainduzi, hili si jambo la kutisha linalostahili kutengenezewa mikakati maana wao wanaouwezo wa kupeleka watoto wao nje kwa masomo ili kesho na kesho kutwa waje kurithi madaraka ya baba zao.
Wananchi, tunatakiwa kuzingatia mambo yote haya, wakati wa kupiga kura mwezi Oktoba mwaka huu, ili kwa nguvu zetu, ambazo ni utashi na kura zetu, tukiondoe Chama Cha Mainduzi madarakani, na kukipa chama kingine hatamu ya uongozi wa nchi yetu, kwa matumaini kwamba tutapata maendeleo tunayoyataka.
Kukirudisha Chama Cha Mapinduzi madarakani, ni kukubali kuwa thamani ya maisha yetu ni, pilau, vikoi na kanga, kama Mheshimiwa Mangula,Katibu Mkuu wa CCM, alivyowahi kusema. Je,tuko tayari kuendelea kunyanyaswa kwa karamu za pilau na vikoi?