Hivi viwanja vingi vipo half way kumalizika, ukiondoa pitch kuwa mbaya ata majukwaa unakuta hayajaisha vizuri. Havina taa, ukiona wachezaji wanaingia dressing room kama wana ingia kwenye shimo la nyoka! Giza limetawala, no running water, vyoo vichafu, pembeni ya pitch ni vichaka. Ata ikipita miaka 10 bado hali itakua hivi hivi au mbaya zaidi kwasababu aliyepewa kumiliki hajui thamani yake, mwenye mali yake kanyang'anywa! Ubaya/uzuri ligi ina kuwa broadcasted live mpaka n'jee wanaona uchafu wetu. Itahitaji siku mwenyeketi wa chama awe anaona aibu kama sisi wapenda mpira tunayoiona kuja na solution ya hii kitu. Matumaini yangu yapo kwa Kassim Majaliwa kwenye hili. Magu kwa jinsi anavyo komaliaga vitu hili lilikuwa swala dogo ila naona ameangalia kwingine.