CCM pawaka moto Dodoma

Hakuna kulala mtu leo Acha kieleweke tuu,Mkuu Invisible mpigie Kileo atupe za uhakika zaidi!Ama zao CCM ama mafisadi watajijua wenyewe sisi raia wa kawaida tunataka Taifa letu lenye heshima na uadilfu siyo kama JK anakotupeleka.
 

Nimekutunuku senks mkuu kwa kutuliza mzuka wangu.
Acha mi nlale, ntafatilia kesho muvi hii.
 

Pasco inaonyesha kuwa you have so much faith in them labda unaweza kutuambia na sisi hiyo imani ya kuwaamini hawa wanaoleta data pungufu unaitoa wapi mwenzetu ili nasi tushawishike kwani ni tokea mwanzo tuliwaomba watutajie walau hao wachangia mada ili mioyo yetu iweze kuwa nao lakini walifail nadhani unakumbuka wakati unaleta updates za Mswada wa Richmond jisi ulivyokuwa ukitiririka kimantiki lakini sioni sababu za hawa kutuletea segements zisizo na muuanganiko wowote
 


...na mind you wote hawa ni wanafunzi wa Mwalimu, yaani kichwa chetu taifa ...

- Ni vyema historia yoyote ya taifa letu inayowahusisha hawa watu hapo juu na Mwalimu...kumuabisha sana Mwalimu...

Respect.


FMEs!


Heshima na wewe kaka.

Pole na msiba, jikaze Mkuu.

Hivi kwa mfano, Makamba, Karume, Kikwete hao hapo pichani, walifundishwa na Mwalimu katika mazingira ya kazi gani, idara zipi, au shule gani, wapi, masomo gani, lini?

Ahsante Mkuu.
 
Inaelekea Mwenyekiti kazi imemshinda lakini hana ujasili wa kusema hivyo nadhani itakuwa jambo la busara kama viongozi wenzie watamsaidia kuutua mzigo uliomlemea!! Binadamu kwa hulka yake hawezi kukubali kuwa kazi imemshinda mpaka hapo watu watakapomsaidia kushuka toka huko juu alikonasa!!
 
.
Nimesema tuwape benefits of doubt, mimi bado nawaaminia kwa sababu kwanza wana guts za ajabu, kwa maoni yangu, kwanza hawa jamaa, sio wajumbe, wao humo ndani ni wahudumu tuu, wawe ni wapitisha maji, fundi umeme, ama watu wa PA Systeam ya sound.

Kutokana na mapenzi makubwa ya JF na walijua mkutano unafanyika hapo, last week, wote wawili ndio wakajiunga JF wiki iliyopita, bahati mbaya mkutano ukasogezwa mpaka wiki hii, kwa vile wako behind the scenes, ndio wameweza kupost.

Huyo mwenye 4 GB sound recorder, ana tenda ya sound kurekodi kila kitu officially, ili apate kutuletea na sisi, lazima kwanza amalize kazi aliyotumwa ndipo usiku atuibie na sisi.

Jamaa wa UWT, wanamonitor JF, 24/7, hivyo by now, wameshamjua huyo ni nani, na leo atashangaa hawatamruhusu kuondoka na chochote. Alitaja highy sophisticated soind recording kama kwenye fremu za miwani ama kwenye sole ya viatu ili kutupa make belive yeye ni mtu muhimu mule ndani. Wenye vifaa hivyo kiukweli wako na ni watu wa ukweli wao wamejinyamazia, ma impostors ndio wapiga kelele!.

Kushindwa kutaja majina, hajui who is who, alimkumbuka Sitta tuu kwa sababu ni known face kufuatia live za bungeni.

Hivyo jamaa kweli wako ukumbini, huyu thread starter amesha log out asije shtukiwa, na 16 bado yuko on line. Ndio maana nasisitiza lets give them the benefits of doubt.
 


Na wewe naanza kukupa doubt of benefits unajuaje wanatumia highly sophisticated recording tools, pale chuo kikuu wakati wa mikutano ya kunji mnapofikia consensus kuandamana utawaona traitors katika ku buy time wanainua mikono mwishoni jamani tuupe muda utawala labda utakuja na solution kumbe wanawasiliana na FFU bado wako mbali wanakuja kutuzunguka, sorry Pasco kwa kukutolea mfano huu.
 
Jamaa ndio alijisifu kuwa anatumia vifaa hivyo vya kisasa na alivitaja, wenye kazi zao, hawawezi kufanya upuuzi kama huo, ndio maana nikasema tuwape benefts of doubt.

Hata mimi siwezi kuzuia mtu kunipa benefits of doubt kwa vile ni vigumu sana kujua for sure, who is who, mimi kwa vile najijua mwenyewe who I am, niko very comfortable na vyovyote ninavyoweza kufikiriwa as long as my conscious is right.
 
Toka lini kuwashugulikia mafisadi equals to kutafuta suluhu?Kama ulivyosema Dotori,terms of reference zimebadilika hence the overall basic ideas and motives to form the committee.
Unajuwa ccm wana kazi kubwa sana,wamezoea kuwadanganya wananchi,na kwasababu kizazi kinabadilika na si kama cha zamani,namna ya kudanganya nayo inabidi iwe more sophisticated than before,lets wait n c if wananchi will buy it.
 
Usanii Mtupu! Hawatafanya lolote lile jipya la kukibadilisha chama hiki kilichoamua kuwa chama cha mafisadi badala ya chama cha mapinduzi.
Tena siyo wapuuzi kiasi hicho!,waache kujadili jinsi ya kuwalaghai wananchi waanze kuumbuana muda huu, wanaitaji punishment japo bungeni wajae watu wengine!
 
Hv, mbona mie sidanganyiki na CCM? Hao wanaodanganyika na kuvaa nguo zile za kijani, kukesha kwenye vikao vyao na kuwapigia kura huwa wanapewa nini? Naomba kura yangu na yakwako kwa mara nyingine tena ziungane kuing'oa CCM kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Jiandikishe kwenye daftari la wapiga kura kama bado hujafanya hivyo.
 

Is true mtoto wa mwaka mmoja akilia unaweza kumpa pipi akanyamaza akifikisha miaka 10 pipi haifai tena atalilia baiskeli kwa hiyo hao wajumbe wa NEC nao sasa si wa kudanganywa kama zamani walivyokuwa wanatishwa kufukuzwa uanachama taratibu mambo yanabadilika hata wananchi wa vijijini nao wamebadilika si wa mwaka 1995.
 
Mkuu naona hapa wanaongea kinyumbani mawaziri wakuu wastaafu naona wote wanatokea nyumba moja i mean kwa baba mmoja.
 
Inashangaza kuona kwamba watu wote hapa jamvini walijiweka katika mkao wa kufuatilia kinachotokea kwenye kikao cha CC.. wakiamini kina mustakabali wa Taifa. Ni nani aliwadanganya hilo linaweza kutokea? Siamini kama kuna mtu mwenye dhamira ya dhati kwa Tz ndani ya hicho chama, wapo kwa ajili yao na vizazi vyao.
Kwa nini tusiamue kuwa hawa watu hawawezi kutupangia nini cha kufanya? Uchaguzi ni wetu, tukianza kwa mmoja mmoja kuamini, natumaini inawezekana.
 
Wa 16 vipi tena, nakuona bado upo, tujulishe kinachoendelea, usisuse, hii ndiyo JF, vumilia twende nayo hivyo hivyo. Tujulishe tuu kama kikao bado kinaendelea.
 

Mhh!!!!! mambo kweli kweli kwa data hizi inaonyesha Pasco kilewo na wa16 wanajuana kwa karibu sana wanapeana data kila wakati yetu macho tunasubiri.
 

Mkuu Pasco licha ya kwamba sijarejea nakwenda kuisoma ile post ya wa 16 kuhusiana na vifaa vya kijasusi,sidhani kama ni kweli alisema anatumia vifaa hivyo,nakumbuka akisema na kutoa reference kuwa kuna uwezekano kwa namna moja ama nyingine ya kupata data hizo kwa njia za tofauti,na alimention vifaa hivyo kama miwani,viatu nk kuwa vinaweza kufanikisha zoezi hilo,lakini hakusema specifically kuwa yeye ama wao wametumia njia gani,hapa JF tukishapata hiyo audio hatuna haja ya kujua wametumia nini,hiyo si kazi yetu hapa unless ni mtu mwenye madhumuni mengine ya tofauti.....tunachotaka sisi ni kuvery tu kuwa contents ni legit,and then ndicho tunachojadili (content)

Lastly, nakubaliana na wewe kuwa tuwape benefit of doubt.....Unajua JF kama darasa,ukikosa baadhi ya vipindi(mijadala/Threads)Ni lazima uwe makini kabla ya kuchangia mjadala utakaoukuta,kwasababu sometimes ni lazima urejee mijadala iliyopita,la sivyo hutauelewa uliopo,kwa mtu kama wewe ni msoma ramani kwani pia uko karibu na matukio hayo,uko updated na uko familiar na the whole situation,na ndio mana ukakubali pia kutoa benefit of doubt, maana kuna watu wanapata shida ya kuweza kutumia common sense based on the knoweledge aquired here in JF,either previously or currently,kuweza kutenganisha kati ya pumba na mchele,kimtizamo, inaonyesha wazi kuwa kutokana na mtiririko wa matukio mbali mbali ya siku za karibuni na hata pia siku za nyuma,habari hii still bado inamake sense,na siwezi kusema moja kwa moja kuwa si za kweli kwasababu uwezekano wa kuwa kweli ni mkubwa... ..Hata hivyo wa 16 pia nampa ushauri kuwa alitoa ahadi na hivyo ahadi huwa deni,ahadi hiyo iliwaexcite wengi wetu,kama ana uhakika na habari zake hizo alikuwa hana haja ya kusema hayo kwani when the whole story comes out,watatoka nishai,na kama hawajui,wamwulize Mh Mo Dewji.

Hata hivyo cha muhimu si hayo yanayoendelea humo ndani,cha muhimu ni hatma yake,hatma ya chochote kinachoendelea humo ndani,na pengine hatma ya mustakabali wa Taifa letu changa kimiaka lakini lililokubuhu kwa ukahaba wa kifisadi......Kwamba Sitta alikunywa maji akatoka nje kwa zaidi ya lisaa na JK kutokufahamu baadhi ya mambo yanayoendelea huku ukweli ukisemekana kuwa mafisadi ndo wenye nguvu na kwa hivyo ccm=ufisadi,havitabadilisha sana chochote kwasasa,hayo yote tisa,kumi ni hatma ya mjadala huo,Sasa kuna taarifa kuwa kamati ya Mwinyi ambayo primarily iliundwa kwa mdhumuni ya kutoa mapendekezo kuhusiana na wanachama wenye kashfa za ufisadi,imeongezewa muda huku terms of reference zikibadilishwa,sasa hivi kamati hiyo itaendelea kulifuja jasho la watanzani kwa kutafuta namna ya kuwasuluhisha wana ccm hao vs mafisadi...2010 hii hapa,nachelea kusema siwezi cheza mbali na JF kwasababu nataka kujua ni nini hatma ya Tanzania na watu wake.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…