Mkuu Pasco licha ya kwamba sijarejea nakwenda kuisoma ile post ya wa 16 kuhusiana na vifaa vya kijasusi,sidhani kama ni kweli alisema anatumia vifaa hivyo,nakumbuka akisema na kutoa reference kuwa kuna uwezekano kwa namna moja ama nyingine ya kupata data hizo kwa njia za tofauti,na alimention vifaa hivyo kama miwani,viatu nk kuwa vinaweza kufanikisha zoezi hilo,lakini hakusema specifically kuwa yeye ama wao wametumia njia gani,hapa JF tukishapata hiyo audio hatuna haja ya kujua wametumia nini,hiyo si kazi yetu hapa unless ni mtu mwenye madhumuni mengine ya tofauti.....tunachotaka sisi ni kuvery tu kuwa contents ni legit,and then ndicho tunachojadili (content)
Lastly, nakubaliana na wewe kuwa tuwape benefit of doubt.....Unajua JF kama darasa,ukikosa baadhi ya vipindi(mijadala/Threads)Ni lazima uwe makini kabla ya kuchangia mjadala utakaoukuta,kwasababu sometimes ni lazima urejee mijadala iliyopita,la sivyo hutauelewa uliopo,kwa mtu kama wewe ni msoma ramani kwani pia uko karibu na matukio hayo,uko updated na uko familiar na the whole situation,na ndio mana ukakubali pia kutoa benefit of doubt, maana kuna watu wanapata shida ya kuweza kutumia common sense based on the knoweledge aquired here in JF,either previously or currently,kuweza kutenganisha kati ya pumba na mchele,kimtizamo, inaonyesha wazi kuwa kutokana na mtiririko wa matukio mbali mbali ya siku za karibuni na hata pia siku za nyuma,habari hii still bado inamake sense,na siwezi kusema moja kwa moja kuwa si za kweli kwasababu uwezekano wa kuwa kweli ni mkubwa... ..Hata hivyo wa 16 pia nampa ushauri kuwa alitoa ahadi na hivyo ahadi huwa deni,ahadi hiyo iliwaexcite wengi wetu,kama ana uhakika na habari zake hizo alikuwa hana haja ya kusema hayo kwani when the whole story comes out,watatoka nishai,na kama hawajui,wamwulize Mh Mo Dewji.
Hata hivyo cha muhimu si hayo yanayoendelea humo ndani,cha muhimu ni hatma yake,hatma ya chochote kinachoendelea humo ndani,na pengine hatma ya mustakabali wa Taifa letu changa kimiaka lakini lililokubuhu kwa ukahaba wa kifisadi......Kwamba Sitta alikunywa maji akatoka nje kwa zaidi ya lisaa na JK kutokufahamu baadhi ya mambo yanayoendelea huku ukweli ukisemekana kuwa mafisadi ndo wenye nguvu na kwa hivyo ccm=ufisadi,havitabadilisha sana chochote kwasasa,hayo yote tisa,kumi ni hatma ya mjadala huo,Sasa kuna taarifa kuwa kamati ya Mwinyi ambayo primarily iliundwa kwa mdhumuni ya kutoa mapendekezo kuhusiana na wanachama wenye kashfa za ufisadi,imeongezewa muda huku terms of reference zikibadilishwa,sasa hivi kamati hiyo itaendelea kulifuja jasho la watanzani kwa kutafuta namna ya kuwasuluhisha wana ccm hao vs mafisadi...2010 hii hapa,nachelea kusema siwezi cheza mbali na JF kwasababu nataka kujua ni nini hatma ya Tanzania na watu wake.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki JF.