peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 18,223
- 31,465
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Oddo Mwisho, amesema CCM haijakurupuka kufanya maamuzi ya kumfukuza uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hana mgogoro na Dkt. Nchimbi. Amesema mwanachama yeyote anayekiuka taratibu za chama, chama kina uwezo wa kuchukua hatua dhidi yake bila kujali nafasi yake.
Akizungumza na wananchi wa kata za Langiro, Kipapa na Maguu zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama tarehe 31/8/2026, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Oddo Mwisho, amesema Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni mwana wa Ruvuma na ni ndugu yao.
Soma Pia: Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM
Amesema Mkoa wa Ruvuma ulikuwa unamtegemea kutokana na nafasi aliyokuwa nayo ya Makamu wa Rais, lakini amewaangusha wananchi wa Ruvuma kwa bahati ambayo Rais Samia aliipa mkoa huo kwa kumchagua mmoja wa vijana wa mkoa huo kuwa msaidizi wake namba moja.