CCM semeni ukweli: Kinana na Makamba wameipuuza Kamati ya Maadili Dodoma wakaenda kuonana na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM hapa Dar

CCM semeni ukweli: Kinana na Makamba wameipuuza Kamati ya Maadili Dodoma wakaenda kuonana na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM hapa Dar

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Kuna mambo kadhaa ambayo CCM wanataka kutuchanganya hapa. Lakini kama usemi unavyoenda - you can fool some people sometimes but not all the people all the time.

Je, Kinana na Makamba wameonana na Kamati ya Maadili ya CCM au wamekutana na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM?

Tunaelewa kwamba Kamati ya Maadili ilikuwa Dodoma, ambako ndiko Membe alihojiwa. Je tuseme ilibidi wajumbe wa kamati ya maadili wakimbizwe kuja Dar Salaam kuwahoji Kinana na Makamba baada ya kuachwa solemba wakiwasubiri kule Dodoma?

Tuambieni ukweli kwamba:
  1. Kinana na Makamba wamegoma kwenda Dodoma kuifuata Kamati ya Maadili
  2. Kinana na Makamba wameifichia CCM aibu kwa kuonyesha kwamba wameitikia wito kwa masharti kwamba hawatakwenda Dodoma bali watakuja Dar esSalaam kuonana na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM
  3. Kinana na Makamba wamewapa masharti CCM kwamba lazima mapokezi yao yaonyeshe hakuna bifu kati yao na CCM kwa viongozi wakuu wa CCM kuwapokea kwa shangwe pale Lumumba kwa ajili ya kupigwa picha.
Ikiwa hivyo ndivyo, nawapongeza sana Kinana na Makamba kwa busara walizotumia hadi sasa. Natumaini walimwambia Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CCM kwamba awamu ya tano waache tabia chafu ya kudukua maongezi binafsi ya viongozi waliostaafu na waliopo madarakani, kwa kuwa sio tu ni tabia ya kimbea bali pia inavunja sheria za nchi.
 
Ukiiona ile picha ya Bwana Bashiru na Makamba inaonyesha kumbe wajumbe wa kamati ndio watuhumiwa! Kama piliton!!!

Na kingine hiyo mishati mzigo ya Mbogamboga hao mabwana hawakuivaa, kuna kitu kinaonyeshwa hapo!

Matusi ya mjumbe mmojawapo bwana Polepole yanatanabaisha kuna kitu hakiko sawa!
 
Na pia siku za nyuma kidogo wakati hili sakata linatrend Bashiru aliwaita hawa wazee wapumbavu. Sidhani kama hilo tusi limetoka kwenye vifua vya hawa wazee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri kuna uwezekano kweli wameandika barua za kujivua uanachama. Hapo ikabidi waombwe wakutane na baadhi ya viongozi. Inawezekana ndio hapo wamekuja kukutana nao dar. Hapo itakuwa wenyewe ndio wataombwa kusitisha kujivua uanachama

Si unaona hata yale matambara yao ya kijani hawakuyavaa, wazee hawataki upumbavu wa kihutu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iliyowaita wakakubali na kuitikia wito ni kamati ndogo ya maadili na usalama ya chama Cha Mapinduzi yenye wajumbe wanne na makamu mwenyekiti wa CCM ndio mwenyekiti wa kamati hiyo.

Kamati ya maadili na usalama inà wajumbe 12 na mwenyekiti wa CCM taifa ndio mwenyekiti wa kamati hiyo na kamati ya maadili haijawahi kuwaita.

Kama Vikao karibu vyote vya kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM vimefanyika Lumumba, Dar kwa Nini unang'ang'ania lazima wangefika dodoma wakati sio làzima?
.
 
Synthesizer,
_joy__joy__joy_ ( 426 X 640 ).jpg
 
Synthesizer, Hebu angalia maneno haya:
"The country has reached the end of the line. It has kiiled or tried to eliminate all opposition leaders one way or another and given rise to a perpetual political class that is arrogant in its views and brazen in its corruption------a political aristocracy that displays an indifference and contempt towards the public that is stunning...." Hapa ndio tulipo.
Waafrika tusitegemee wachina au wazungu kutufundisha kujitawala tumeamua tuwe wajinga kukumbatia udikteta wa chama kimoja. Kamwe hatufiki.
Tumeamua wenyewe kuelekea shimoni tukijisifu na kuchekelea! Hatutoki humo kamwe.

Tunajivunia kijana wetu Mtanzania M. Samata kafika hatua ya kucheza soka ulaya! Tunajenga viwanja vikubwa "vya kimataifa" vya michezo lakini tunabomoa nchi kwa kuvunja sheria zetu na za kimataifa kuhusu haki za binadamu. Heshima ya 'mwanetu Samata' kufika ulaya inatustahili sisi au wazungu?
Samata amefika alipo kwa "magoli ya mkono"?
Huu unafiki kupitia Samata msidhani waerevu duniani na hao wazungu wataufumbia macho milele!
Mnaua vipaji vya vijana wengi wa TZ kama Samata kwa kudhoofisha elimu zao, afya zao, uchumi na haki zao za kujitawala chini ya democracy and freedom of speech nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The country has reached the end of the line. It has kiiled or tried to eliminate all opposition leaders one way or another and given rise to a perpetual political class that is arrogant in its views and brazen in its corruption------a political aristocracy that displays an indifference and contempt towards the public that is stunning...."
Maneno mazito.
 
Na pia siku za nyuma kidogo wakati hili sakata linatrend Bashiru aliwaita hawa wazee wapumbavu. Sidhani kama hilo tusi limetoka kwenye vifua vya hawa wazee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Douglas, aliwaita akiwa wapi? Au kupitia platform gani? Una chanzo chochote cha uhakika kinacholithibitisha hili? Maana ikithibitika hivyo, kwa mfano kama kuna "tweet" yake au video huko "youtube" inayolithibitisha hili, basi CCM ndo itakuwa imekwisha.
 
Synthesizer,
Mimi ninadhani tuwache kejeli kwa mambo ambayo hayatuhusu kwani wengi wetu siyo wanancham na wale wanachama wakitaka kufahamu kinachoendelea wana utaratibu wao.
 
Mimi ninadhani tuwache kejeli kwa mambo ambayo hayatuhusu kwani wengi wetu siyo wanancham na wale wanachama wakitaka kufahamu kinachoendelea wana utaratibu wao.
Ukisha kuwa chama cha siasa, ambacho kisheria ni public organization, then una responsibilities to the general public, wawe wanachama au wasiwe wanachama. Kinachoendelea CCM kinaathiri kila mtu, hivyo huwezi kusema hayatuhusu hata kama sie sio wanachama.
 
Back
Top Bottom