CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Duh sasa CCM naona wanatuletea mkorogo..
Mkuu Mchambuzi nina swali... Je ikitokea rais wa Muungano akafariki/au kuugua kwa muda mrefu ni nani atakahimu nafasi yake? Je ni makamo wa rais (Rais wa Zanzibar ambaye hakuchaguliwa na watanganyika (Bara) au ni Waziri mkuu ambaye hakuchaguliwa na wazanzibar (Maana nafasi ya rais wa Muugano ni muhimu kukahimiwa na kiongozi aliyechaguliwa pande zote za Muugano.

Swali la pili itakuwaje kama mgombea urais wa Muungano (tusema CCM) (Tanzania Bara) akapochaguliwa kwa kura nyingi bara. lakini kwa Zanzibar akapata kura chache saaaaana au hata hasipate kura kabisa na Mgombea urais wa Cuf apate kura za kutosha kutoka Zanzibar lakini kura pungufu Bara. Swali je nani atakuwa Rais wa Muungano maan rais wa Muugano inatakiwa akubaliwe sehemu zote.
mimi huwa nafikiri akifariki Rais Mtuu anayeitwa mgombea mwenza ambaye ndo makamu wa rais anachukuwa madaraka nifahamisheni zaidi naona pana matatizo hapo.
 
Wakuu JokaKuu na Mchambuzi
Linapokuja suala la muundo wa muungano binafsi nilishawahi kuonesha msimamo wangu humu ndani… kwamba, watu tunapofikiria mfumo Fulani tunatakiwa kufahamu ni nini hasa tunachohitaji. Kila mfumo una faida na hasara zake… so, ni wajibu wa kila mmoja kufahamu yupo tayari ku-sacrifice nini au ni nini hasa anahitaji. Ikiwa piga ua, huwezi kuacha kula kitimoto au kuingia nyumba ya ibada bila viatu, basi dini muafaka kwako ni Ukristo lakini ikiwa piga ua ni lazima uwe na mke zaidi ya mmoja… basi Ukristo si wako na badala yake opt Uislamu! Jambo hili wengi wetu hatuliangalii kwa kina.

Binafsi, kitu ambacho siwezi ku-forgo ni AMANI. Kwa maoni yangu, popote inapotokea kuvunjika kwa muungano lazima amani nayo itakuwa kwenye rehani… tumeshuhudia haya USSR na Yugoslavia kutaja mifano michache. God bless Czechoslovakia... hawa waligawana mbao kwa utulivu! Kwa upande mwingine, binafsi naamini kwamba, hakuna muundo wa muungano hapa nchini ambao uta-guarantee muungano wetu DAIMA DUMU… whether tuwe na serikali mbili, tatu au moja… it's just a matter of time… siku itafika na tutagawana mbao kama walivyofanya USSR na Yugoslavia ambao walidumu kwenye muungano kwa zaidi ya miaka 70, seuze 50! Hivyo, basi kwangu mimi muundo bora wa muungano hapa kwetu ni ule utakaotufanya, siku ikifika, basi tugawane mbao kwa amani. Mfumo wa serikali mbili wa SASA haufai… ikitokea tunagawana mbao leo hii lazima patokee kugombea kwa madaraka, hususanu Bara. Leo hii JK ni Rais ambae amechaguliwa na pande mbili za Muungano… leo hii tukigawana mbao, si tu kwamba JK anakosa uhalali wa kuongoza ZNZ bali hata huku Bara… coz’ alipigiwa kura na ZNZ pia regardless kama huko nako alipata kura au hapana! Makamu wa Rais nae automatically hana sifa za kuongoza Bara coz’ yeye ni Mzanzibari… panapotokea ugomvi wa madaraka, hata Speaker nae ataonekana hana sifa coz’ nae alichaguliwa na wabunge kutoka Bara na ZNZ!!! Jaji wa sasa nae, angalau kwa mazingira ya sasa… hawezi kuwa na sifa za kuongoza Bara coz’ nae ni Mzanzibari… so, mwaka wowote ikitokea muungano wetu unavunjika wakati Leadership Structure ndo kama iliyopo hivi sasa basi ni lazima kuwepo ugombeaji wa madaraka hususani huku Bara. Katika mazingira kama hayo, Jeshi wanakuwa na wajibu wa kuchukua nchi. Kule ZNZ, inaweza kuwa rahisi kuweka kipindi cha mpito coz’ Rais wa ZNZ amechaguliwa only na Wa-Zanzibari na hata ikitokea wa kupinga, bado kupata Kaimu kwa mujibu wa Katiba yao itakuwa ni rahisi.

Sasa basi, provided hakuna muundo unao-guarantee muungano daima basi muundo bora ni ule utakaotuwezesha kugawana mbao kwa amani siku ikifika. Muundo wa Serikali Tatu katika hili ni muafaka kabisa coz' unawezesha pande mbili za muungano kuwa na viongozi wake wakuu waliochaguliwa na wananchi. So, hata kama muungano unavunjika, hakuna sababu za kutokea ugomvi wa madaraka coz’ Kiongozi wa Bara anakuwa amechaguliwa na watu wa Bara peke yao hali kadhalika kule ZNZ! Lakini pamoja na ukweli huo, hapa sipendi kuwa mnafiki hata kidogo. Ingawaje hakuna muundo wa muungano unaoweza ku-guarantee muungano wetu kuendelea lakini ukweli upo pale pale hata kama hatutaki kwamba mfumo wa serikali unaweza ku-speed the rate of dissolution.

Hivyo basi, ikiwa ni kweli bado tunauhitaji muungano na kv hakuna shaka kwamba wote tunahitaji amani, basi muundo bora kwetu ni ule ambao utafanikisha mambo mawili...
1. Ikiwa tunagawana mbao, basi tugawane kwa amani bila kuacha ugomvi wa madaraka kutoka pande yoyote ile.
2. Kuupeleka muungano wetu miaka mingi zaidi kadri itakavyowezekana.

Ukiangalia maelezo yangu, option namba 1 inapatikana kwenye mfumo wa serikali 3 wakati namba 2 inapatikana kwenye mfumo wa serikali 2. Hivyo basi, naweza ku-conclude kwamba mfumo bora kabisa ni ule utakao-facilitate hayo mambo mawili... yaani combination ya mfumo wa serikali 2 na serikali tatu!

Nasikia mpango wa CCM ni kuwa na mfumo ambao huku Bara tutakuwa na Bunge la Wawakilishi. Binafsi sijaona mpango huu lakini ikiwa wanauweka vizuri basi huo ndio mfumo bora zaidi coz’ una-combine mfumo wa serikali mbili (wa kuwa na Rais wawili) na Mfumo wa serikali 3 (wa Tanganyika kuwa na serikali yake). Kwavile sifahamu mfumo wao upo vipi, basi maoni yangu ni kwamba tuwe na mfumo ambao Tanganyika itakuwa na bunge lake pamoja na kiongozi mkuu wa Tanganyika… call him PM or Chief Minister; it doesn’t matter. Huyu PM ama Chief Minister apigiwe kura na wananchi moja kwa moja na asiwe wa kuteuliwa kama ilivyo sasa (for PM wa Muungano or Chief Minister). Akishakuwa wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi anapata uhalali wa kuwa kiongozi wa nchi ya Tanganyika ndani ya Jamhuri ya Muungano. Siku tukigawana mbao, huku Bara tutakuwa na kiongozi tayari ambae amepigiwa kura na Watanganyika pekee hivyo kuwa na uhalali japo wa muda wa kuendelea kuongoza Tanganyika nje ya muungano! Ndani ya Muungano, huyu ndie atakuwa kiongozi wa serikali ya Tanganyika atakayehusika na masuala ya Tanganyika peke yake. Hapa tena pasiwe na suala la mambo ya Tanganyika kushughulikwa na Muungano... ya Tanganyika yabaki Tanganyika na yashughulikiwe na Tanganyika na ya Muungano yabaki ya Muungano na yashughulikiwe na muungano, hali kadhalika kule ZNZ! Aidha, linapokuja suala la mapato, tuwe na mamlaka moja tu, TRA... makusanyo ambayo hivi sasa yanaenda Hazina Kuu yaendelee kuwa hivyo... kwamba ni mapato ya muungano! Kile ambacho hivi sasa kinaitwa mapato ya ndani ya halmashauri zetu ndicho kiwe mapato ya Tanganyika yasiyo ya muungano. Aidha, inapotokea, say, serikali ya Tanganyika IMEBUNI, narudia, iwe IMEBUNI chanzo cha mapato yake yenyewe... mapato hayo yanaweza kuwa ya Tanganyika peke yake otherwise, mapato yote ya TRA leo yanayoenda kwenye fuko la muungano yaendelee kuwa hivyo!

Kwa upande mwingine, tusiwe too optimistic. Katiba ya Tanganyika iseme wazi kwamba inapotokea Muungano umevunjika, basi PM/Chief Minister wa Tanganyika ataendelea kuwa kiongozi wa Jamhuri ya Tanganyika hadi atakapomaliza kipindi chake… ama kwa kipindi itakachoonekana inafaa; yaani kipindi cha mpito.
Nguruvi3, Mwigulu Nchemba, Pasco, Yericko Nyerere, HKigwangalla, EMT
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

Asante kwa hayo yote nimekuambia kuwa ukitaka kujadili lete numbers. Economist tunasema no research no right to speak. Kakokotoe number zilete mie sikukuletea number nikazibandika nimekuambia hizi gharama zinazokuwa kila siku serikali kwa serikali mbili hazina umuhimu wala mantiki katika uchumi wa Tanzania. Intergovernmental fiscal relationship inatakiwa tuitoe na instead na uniform fiscal structure. Na hilo tunaweza kuwa nalo tutakapoanza kukubaliana kimsingi nini tunataka kuachive katika uchumi wetu. Tunapotengeneza uniform tarrifs, economic zone, etc we can achieve an economic union inayojumuisha interest za Tanganyika na Zanzibar. Hivyo tunakuwa uchumi shirikishi wa pamoja. Vile vile tunaweza kuhamia katika monetary union tukaweza kuharmonize policies zetu na eventually kuwa na economic union. Serikali tatu hayo nayokueleza hayataweza kufanikiwa unless tuwe na serikali ya muungano yenye mamlaka makubwa kuliko Serikali shirikishi.

Na hilo nyie wanasiasa hamlitaki mnataka zaidi kutetea maslahi ya nafasi zenu na fursa za kutafuna kodi zetu. Binafsi sijaona hoja ya mantiki unayojenga na nasubiri kwa hamu mada yako ya Serikali 3. Na sitaiona mada ya maana kama hujaja na numbers ambazo ni realistic kuniconvince 3 ni bora zaidi ya serikali moja.

By the way usidhani unajadiliana na asiyejua uchumi nina PhD ya uchumi na Degree za uchumi ya kwanza na ya pili. Na pia nina degree ya uanasheria ingawa lakini siutumii. Vile vile PhD yangu sikuipata kwa maprofessa wenu uchwara bali nimeipata kwa nobel laureate wa economics kwahiyo I am very keen to what I speak and write and discuss.

All the best Mchambuzi looking forward.

Alright Sir, nitakujulisha uzi ukiwa tayari. Hongera kwa mafanikio yako kielimu, I just hope you are not only educated, but also enlightened.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
nina PhD ya uchumi na Degree za uchumi ya kwanza na ya pili. Na pia nina degree ya uanasheria ingawa lakini siutumii. Vile vile PhD yangu sikuipata kwa maprofessa wenu uchwara bali nimeipata kwa nobel laureate wa economics kwahiyo I am very keen to what I speak and write and discuss.

Wote tungekuwa tunaweka CV zetu humu, pasingetosha!

I just hope you are not only educated, but also enlightened.

Nimeipenda hii, sentensi fupi lakini imejaa ujumbe mzito!
 
Wakuu JokaKuu na Mchambuzi
Linapokuja suala la muundo wa muungano binafsi nilishawahi kuonesha msimamo wangu humu ndani… kwamba, watu tunapofikiria mfumo Fulani tunatakiwa kufahamu ni nini hasa tunachohitaji. Kila mfumo una faida na hasara zake… so, ni wajibu wa kila mmoja kufahamu yupo tayari ku-sacrifice nini au ni nini hasa anahitaji. Ikiwa piga ua, huwezi kuacha kula kitimoto au kuingia nyumba ya ibada bila viatu, basi dini muafaka kwako ni Ukristo lakini ikiwa piga ua ni lazima uwe na mke zaidi ya mmoja… basi Ukristo si wako na badala yake opt Uislamu! Jambo hili wengi wetu hatuliangalii kwa kina.

Binafsi, kitu ambacho siwezi ku-forgo ni AMANI. Kwa maoni yangu, popote inapotokea kuvunjika kwa muungano lazima amani nayo itakuwa kwenye rehani… tumeshuhudia haya USSR na Yugoslavia kutaja mifano michache. God bless Czechoslovakia... hawa waligawana mbao kwa utulivu! Kwa upande mwingine, binafsi naamini kwamba, hakuna muundo wa muungano hapa nchini ambao uta-guarantee muungano wetu DAIMA DUMU… whether tuwe na serikali mbili, tatu au moja… it's just a matter of time… siku itafika na tutagawana mbao kama walivyofanya USSR na Yugoslavia ambao walidumu kwenye muungano kwa zaidi ya miaka 70, seuze 50! Hivyo, basi kwangu mimi muundo bora wa muungano hapa kwetu ni ule utakaotufanya, siku ikifika, basi tugawane mbao kwa amani. Mfumo wa serikali mbili wa SASA haufai… ikitokea tunagawana mbao leo hii lazima patokee kugombea kwa madaraka, hususanu Bara. Leo hii JK ni Rais ambae amechaguliwa na pande mbili za Muungano… leo hii tukigawana mbao, si tu kwamba JK anakosa uhalali wa kuongoza ZNZ bali hata huku Bara… coz’ alipigiwa kura na ZNZ pia regardless kama huko nako alipata kura au hapana! Makamu wa Rais nae automatically hana sifa za kuongoza Bara coz’ yeye ni Mzanzibari… panapotokea ugomvi wa madaraka, hata Speaker nae ataonekana hana sifa coz’ nae alichaguliwa na wabunge kutoka Bara na ZNZ!!! Jaji wa sasa nae, angalau kwa mazingira ya sasa… hawezi kuwa na sifa za kuongoza Bara coz’ nae ni Mzanzibari… so, mwaka wowote ikitokea muungano wetu unavunjika wakati Leadership Structure ndo kama iliyopo hivi sasa basi ni lazima kuwepo ugombeaji wa madaraka hususani huku Bara. Katika mazingira kama hayo, Jeshi wanakuwa na wajibu wa kuchukua nchi. Kule ZNZ, inaweza kuwa rahisi kuweka kipindi cha mpito coz’ Rais wa ZNZ amechaguliwa only na Wa-Zanzibari na hata ikitokea wa kupinga, bado kupata Kaimu kwa mujibu wa Katiba yao itakuwa ni rahisi.

Sasa basi, provided hakuna muundo unao-guarantee muungano daima basi muundo bora ni ule utakaotuwezesha kugawana mbao kwa amani siku ikifika. Muundo wa Serikali Tatu katika hili ni muafaka kabisa coz' unawezesha pande mbili za muungano kuwa na viongozi wake wakuu waliochaguliwa na wananchi. So, hata kama muungano unavunjika, hakuna sababu za kutokea ugomvi wa madaraka coz’ Kiongozi wa Bara anakuwa amechaguliwa na watu wa Bara peke yao hali kadhalika kule ZNZ! Lakini pamoja na ukweli huo, hapa sipendi kuwa mnafiki hata kidogo. Ingawaje hakuna muundo wa muungano unaoweza ku-guarantee muungano wetu kuendelea lakini ukweli upo pale pale hata kama hatutaki kwamba mfumo wa serikali unaweza ku-speed the rate of dissolution.

Hivyo basi, ikiwa ni kweli bado tunauhitaji muungano na kv hakuna shaka kwamba wote tunahitaji amani, basi muundo bora kwetu ni ule ambao utafanikisha mambo mawili...
1. Ikiwa tunagawana mbao, basi tugawane kwa amani bila kuacha ugomvi wa madaraka kutoka pande yoyote ile.
2. Kuupeleka muungano wetu miaka mingi zaidi kadri itakavyowezekana.

Ukiangalia maelezo yangu, option namba 1 inapatikana kwenye mfumo wa serikali 3 wakati namba 2 inapatikana kwenye mfumo wa serikali 2. Hivyo basi, naweza ku-conclude kwamba mfumo bora kabisa ni ule utakao-facilitate hayo mambo mawili... yaani combination ya mfumo wa serikali 2 na serikali tatu!

Nasikia mpango wa CCM ni kuwa na mfumo ambao huku Bara tutakuwa na Bunge la Wawakilishi. Binafsi sijaona mpango huu lakini ikiwa wanauweka vizuri basi huo ndio mfumo bora zaidi coz’ una-combine mfumo wa serikali mbili (wa kuwa na Rais wawili) na Mfumo wa serikali 3 (wa Tanganyika kuwa na serikali yake). Kwavile sifahamu mfumo wao upo vipi, basi maoni yangu ni kwamba tuwe na mfumo ambao Tanganyika itakuwa na bunge lake pamoja na kiongozi mkuu wa Tanganyika… call him PM or Chief Minister; it doesn’t matter. Huyu PM ama Chief Minister apigiwe kura na wananchi moja kwa moja na asiwe wa kuteuliwa kama ilivyo sasa (for PM wa Muungano or Chief Minister). Akishakuwa wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi anapata uhalali wa kuwa kiongozi wa nchi ya Tanganyika ndani ya Jamhuri ya Muungano. Siku tukigawana mbao, huku Bara tutakuwa na kiongozi tayari ambae amepigiwa kura na Watanganyika pekee hivyo kuwa na uhalali japo wa muda wa kuendelea kuongoza Tanganyika nje ya muungano! Ndani ya Muungano, huyu ndie atakuwa kiongozi wa serikali ya Tanganyika atakayehusika na masuala ya Tanganyika peke yake. Hapa tena pasiwe na suala la mambo ya Tanganyika kushughulikwa na Muungano... ya Tanganyika yabaki Tanganyika na yashughulikiwe na Tanganyika na ya Muungano yabaki ya Muungano na yashughulikiwe na muungano, hali kadhalika kule ZNZ! Aidha, linapokuja suala la mapato, tuwe na mamlaka moja tu, TRA... makusanyo ambayo hivi sasa yanaenda Hazina Kuu yaendelee kuwa hivyo... kwamba ni mapato ya muungano! Kile ambacho hivi sasa kinaitwa mapato ya ndani ya halmashauri zetu ndicho kiwe mapato ya Tanganyika yasiyo ya muungano. Aidha, inapotokea, say, serikali ya Tanganyika IMEBUNI, narudia, iwe IMEBUNI chanzo cha mapato yake yenyewe... mapato hayo yanaweza kuwa ya Tanganyika peke yake otherwise, mapato yote ya TRA leo yanayoenda kwenye fuko la muungano yaendelee kuwa hivyo!

Kwa upande mwingine, tusiwe too optimistic. Katiba ya Tanganyika iseme wazi kwamba inapotokea Muungano umevunjika, basi PM/Chief Minister wa Tanganyika ataendelea kuwa kiongozi wa Jamhuri ya Tanganyika hadi atakapomaliza kipindi chake… ama kwa kipindi itakachoonekana inafaa; yaani kipindi cha mpito.
Nguruvi3, Mwigulu Nchemba, Pasco, Yericko Nyerere, HKigwangalla, EMT

Mkuu.
Hoja zako zina mashiko na kusema kweli ni sahihi lakini kigingi cha kutekelezeka ni ubinafsi wa watawala na wasaka madaraka 2015. Tusingekua na matatizo kama Rais wetu ajaye angeomba uongozi akijua kwamba yeye anakwenda Ikulu kazi zake ni kuongoza muungano wa nchi washirika ambazo mambo yasiyo husu muungano yapo chini ya serikali za Tanganyika na Zanzibar.

Kinyume watawala waliopo hawataki kubadili mazoea. Wanataka mambo yabakie kama kawaida licha ya kero nyingi ambazo huko usoni zitaleta machafuko na tuachane kwa uhasama.Wanata serikali ya JMT isimamie kila kitu licha ya ufanisi mdogo tumeshuhudia. Muhimu viongozi waheshimu katiba na mipaka ya utendaji wa kila Serikali . Serikali kuu ikiwa ni ya Shirikisho.
 
Last edited by a moderator:
Hata kiswahili huwezi kuongea.
http://www.afrobarometer.org/files/documents/media_briefing/tan_r5_mediabriefing.pdf
ukurasa wa 21. Asilimia 14 wanataka serikali tatu.

Mkuu sijasoma HKL kama wewe hivyo najua lugha ya kuikomboa Tanganyika tu. Tuseme ukweli bila kumung'unya maneno, hivi ukiondoa sababu za kisiasa Tanganyika imepata faida gani kujiunga na Zanzibar. Mimi naona faida pekee labda ni ubatizo wa jina kutoka Tanganyika kuwa Tanzania the rest ni hasara tu, kama faida nyingine tofauti na hiyo tuambie wewe.

Kuhusu takwimu kuwa 14% bado ni wengi ukilinganisha 0.000000% ya Nyerere na Karume. Hata wabunge 400 wa ccm ndani ya BMLK na hata ukichanganya na wale 201 wapiga Tarumbeta waliokodiwa na Mwenyekiti wa ccm kwenda kupiga meza bungeni na kuharibu furniture zetu bado ni wachache compared to 14% na statistical report ya warioba hivyo hamna haki kisheria kupindua maoni ya wananchi.
Ifike mahali tuwe wawazi ifike wakati ccm ikubali wananchi tumechoka kuburuzwa na ccm. Kama tangu mwanzo Wananchi wangekataa kuburuzwa na Nyerere tusingefika hapa tulipo ila Kuna uzembe ulifanyika. Lazima hiki si kile kizazi cha ndiondio bila kuhoji wala kufikiri.
 
Alright Sir, nitakujulisha uzi ukiwa tayari. Hongera kwa mafanikio yako kielimu, I just hope you are not only educated, but also enlightened.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Likewise hapo pekundu na pia I also hope you have learned economics instead of politics sir. Uje na hoja zenye mashiko katika economics and sio siasa. I am waiting.
 
Mkuu sijasoma HKL kama wewe hivyo najua lugha ya kuikomboa Tanganyika tu. Tuseme ukweli bila kumung'unya maneno, hivi ukiondoa sababu za kisiasa Tanganyika imepata faida gani kujiunga na Zanzibar. Mimi naona faida pekee labda ni ubatizo wa jina kutoka Tanganyika kuwa Tanzania the rest ni hasara tu, kama faida nyingine tofauti na hiyo tuambie wewe.

Kuhusu takwimu kuwa 14% bado ni wengi ukilinganisha 0.000000% ya Nyerere na Karume. Hata wabunge 400 wa ccm ndani ya BMLK na hata ukichanganya na wale 201 wapiga Tarumbeta waliokodiwa na Mwenyekiti wa ccm kwenda kupiga meza bungeni na kuharibu furniture zetu bado ni wachache compared to 14% na statistical report ya warioba hivyo hamna haki kisheria kupindua maoni ya wananchi.
Ifike mahali tuwe wawazi ifike wakati ccm ikubali wananchi tumechoka kuburuzwa na ccm. Kama tangu mwanzo Wananchi wangekataa kuburuzwa na Nyerere tusingefika hapa tulipo ila Kuna uzembe ulifanyika. Lazima hiki si kile kizazi cha ndiondio bila kuhoji wala kufikiri.
Nakubaliana na wewe 199%
Haya kawaambie walimu wako nasubiri majibu yangu.
 
Likewise hapo pekundu na pia I also hope you have learned economics instead of politics sir. Uje na hoja zenye mashiko katika economics and sio siasa. I am waiting.

Learning politics isn't a bad thing, not all. What's bad ni kuwa mchumi mtumwa wa siasa.

Unaweza kutuambia umesomea economics chuo gani (PhD) level, na research yako ilihusu kitu gani? You might inspire some - in terms of achievements, but importantly kujua unakuja from what background of economics katika kujadili hoja hizi, na pia iwapo utafiti wako ulilenga Tanzania, na nini watanzania wenzako wanaweza kujifunza, na ikiwezekana kuangalia what further areas of research zinaweza patikana from your work.

I hope hili nalo hautasema napiga "siasa".

You have to wear boots za PhD (econ) humu, especially if supervised by a nobel laurette. This is important because you have decided to bring that up and make it a factor in your contributions.

Wengine hatujaliwa hayo, so tunaweza jifunza mengi.

On another note:

Posts #3 and posts #108 have gone fatigue waiting for you. Haujathubutu kujadili hata mstari mmoja, badala yake, hapo juu unarudia makosa yale yale niliyokueleza. Usidondoe dondoe hoja, jadili hoja.

Unaulizwa what analytical framework do you use to arrive to to your conclusions kwamba serikali moja ina faida in fiscal terms kuliko tatu, hauna majibu, una copy and paste bajeti. PhD holder.

Unaelekezwa kwenda angalia hoja zetu kule kwenye uzi wa Nguruvi3 juu ya gharama, na kwamba ule mjadala ni indicative tu, mwingine unakuja, unasema umeupitia juu juu, but still make concluding remarks about it. Unaelekezwa uende kwenye uzi wangu "Nape, Tujadili Faida Za Serikali Tatu", nayo pia kama maandalizi wakati tunasubiri uzi maalum kabisa nilio ahidi, Dr. Mdondoaji anasema tunapiga siasa wakati ni yeye ndiye anayefanya political spinning, na kwa vile analemewa, anajieleza kwamba kasoma sana kwamba tulazimike kuona hoja zake ndio absolute.

Dr. Mdondoaji...

Kwanza usiniite Dr Mdondoaji bali niite muuza kahawa wa kariakoo. Nimekuambia elimu kwasababu ulisema sina uelewa wa economics ndio nikakutahadharisha ninaufahamu mzuri sana wa economics, sina haja kukupa kazi zangu hatuko hapa kujuana bali kujadiliana so I think my identity and contribution is relevant to those of my field of research. It is irrelevant for JF.

Kuhusu maswali yako nimekujibu ila kama hujanielewa niulize. Ila nasubiri mchakato unaoundaa kuhusu serikali 3 na urahisi wake dhidi ya serikali 2 na hata moja I am very interested to know the numbers. I am just curious sir
 
Basi tueleze Phd uli specialize kwenye kitu gani. Unavyojadili hoja ni kama uli specialize vitu nje kabisa - kama vile labour economics, industrial economics. Na ulipoonja kozi ya masuala tunayojadili humu as one of your elective courses, ukaona umekuwa mwelewa. Phd in economics una support centralization of fiscal system kwamba it brings more efficiency?

Numbers gani unataka kujua bila ya kwanza kuangalia competence ya mapato na matumizi ya fedha za umma zipo wapi between central government and sub national governments? Unaulizwa framework of analysis, unakuja na budget? Mara mia ungekuja na Public Expenditure Review, but the union budget? You want us to use that as a framework of analysis kubaini mfumo upi ni bora? I must say huu ni uvivu wa kufikiri, unasema tunapiga siasa lakini ni wewe unapiga siasa kwani unaiga tabia ile ile ya wanasiasa pale bungeni kutumia bajeti kama analytical framework to determine mfumo upi ni bora, tena budget ambayo wewe kama kweli mchumi na mwelewa wa constraints zilizopo (za kujitakia na za kupandikizwa na donors), ulitakiwa uweke bajeti kama kiporo and instead do what I suggested pale post #108 .

Ningependa kujua PhD ulifanya research on what area, and key findings zako zilikuwa nini. This won't reveal your identity for sure.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Dr. Mdondoaji,

Na kwanini nikuite muuza kahawa wa kariakoo and not a Dr (PhD)? and you seriously want to convince us hapa kwamba tujadiliane na wewe kama muuza kahawa na kashata kwa sababu your academic background isn't relevant for JF? Sasa why did you went that far kutueleza in the first place? You should have just maintained kwamba wewe ni muuza kahawa lakini unaelewa unachokisema from experience ya kahawa and the like, yangeishia hapo. Mbona hata sisi ni wabangaizaji? Do you know of my academic qualifications? I can be just a reader in economics na nikawa mwelewa mzuri tu, na baada ya kusoma hayo, nikaendelea na kusoma magazeti ya udaku, etc, maisha yakaenda tu.

Na kwanini nisikuite doctor (phd) wakati hivyo ndivyo umejitambulisha? Na nikuite Dr. Nani kama sio mdondoaji? Nadhani nina haki ya kukuita hivyo, na nitaendelea na jina hili kukupa heshima yako. Naheshimu sana wasomi by the way.

Mkuu,

Unatoka nje ya mada jadili hoja za msingi na sio elimu yangu. Pia kama umenielewa nimekuambia njoo na numbers kwa unitary government (Serikali moja), Federal government (Serikali 3) na A combination of unitary and federal structure (Serikali 2). Pia tueleze intergovernmental relations between these government zitakuwaje? Fiscal and Monetary Relations zikoje. Toa figures zenye kuonyesha huo unafuu unaopatikana katika Serikali 3 ambao haupo serikali mbili na wala moja. Vile vile budget contribution itokanayo na hivyo vyanzo vitakavyokuwa apportion kwa serikali washirika na serikali kuu na athari zake katika nchi. Kwani naona dalili tusipokuwa makini tunaweza kuwa kama Kenya na mfumo wao wa federal government ambapo sasa inabidi waanze kuanzisha kodi zisizokuwa na kichwa na miguu kujaribu kuongeza mapato na kuanza kulazimisha wananchi wapunguziwe mishahara kupunguza matumizi ya serikali.

Achana na findings zangu mie zangu zishanipa PhD, zimenipa uassociate na wengine wanazitumia kutafuta na wao PhD. Ukifanya research katika economics huenda ukanikuta ila kwa kupiga siasa hapa JF it is irrelevant na wala hainisaidii kitu .

Do your work mkuu tupate kuelimika kwani elimu haina mwisho tunajifunza kila siku. Mie sifaidiki na serikali 2 wala 3 wala 100 nitaendelea kula mkate wangu kama kawaida. Ila nyie wanasiasa ndio mnatetea mifumo ambayo inawanufaisha kulinda nafasi zenu huko CCM na kwenye vyama vyenu vya siasa.

Tujadili mada hasa kama wewe mchumi ninatarajia uje na numbers na sio siasa.
 
Dr. Mdondoaji,

Na kwanini nikuite muuza kahawa wa kariakoo and not a Dr (PhD)? and you seriously want to convince us hapa kwamba tujadiliane na wewe kama muuza kahawa na kashata kwa sababu your academic background isn't relevant for JF? Sasa why did you went that far kutueleza in the first place? You should have just maintained kwamba wewe ni muuza kahawa lakini unaelewa unachokisema from experience ya kahawa and the like, yangeishia hapo. Mbona hata sisi ni wabangaizaji? Do you know of my academic qualifications? I can be just a reader in economics na nikawa mwelewa mzuri tu, na baada ya kusoma hayo, nikaendelea na kusoma magazeti ya udaku, etc, maisha yakaenda tu.

Na kwanini nisikuite doctor (phd) wakati hivyo ndivyo umejitambulisha? Na nikuite Dr. Nani kama sio mdondoaji? Nadhani nina haki ya kukuita hivyo, na nitaendelea na jina hili kukupa heshima yako. Naheshimu sana wasomi by the way.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kaka Mchambuzi,

Kama unaniita kwa heshima nashukuru ni haki yangu ila sasa hivi heshima ya PhD kwa Tanzania sijui kama bado ipo kwani hadi honoraria causa zinaitwa Dr. Niliwahi kuja mkutano mmoja hapo Nyerere Complex nikakutana na honoraria mmoja anaitwa Dr I felt a bit ashamed! I hope you understand why.

Mie ndio maana kijiweni JF napenda kujiita muuza kahawa kariakoo kwani nimekulia karibu na muuza kahawa hapo kariakoo na ni rafiki yangu kipenzi sana hapo kariakoo. Nampa heshima kubwa sana huyu bwana ndio maana najifagharisha na yeye.

Tuendelee na mjadala mkuu
 
Learning politics isn't a bad thing, not all. What's bad ni kuwa mchumi mtumwa wa siasa.

Unaweza kutuambia umesomea economics chuo gani (PhD) level, na research yako ilihusu kitu gani? You might inspire some - in terms of achievements, but importantly kujua unakuja from what background of economics katika kujadili hoja hizi, na pia iwapo utafiti wako ulilenga Tanzania, na nini watanzania wenzako wanaweza kujifunza, na ikiwezekana kuangalia what further areas of research zinaweza patikana from your work.

I hope hili nalo hautasema napiga "siasa".

You have to wear boots za PhD (econ) humu, especially if supervised by a nobel laurette. This is important because you have decided to bring that up and make it a factor in your contributions.

Wengine hatujaliwa hayo, so tunaweza jifunza mengi.

On another note:

Posts #3 and posts #108 have gone fatigue waiting for you. Haujathubutu kujadili hata mstari mmoja, badala yake, hapo juu unarudia makosa yale yale niliyokueleza. Usidondoe dondoe hoja, jadili hoja.

Unaulizwa what analytical framework do you use to arrive to to your conclusions kwamba serikali moja ina faida in fiscal terms kuliko tatu, hauna majibu, una copy and paste bajeti. PhD holder.

Unaelekezwa kwenda angalia hoja zetu kule kwenye uzi wa Nguruvi3 juu ya gharama, na kwamba ule mjadala ni indicative tu, mwingine unakuja, unasema umeupitia juu juu, but still make concluding remarks about it. Unaelekezwa uende kwenye uzi wangu "Nape, Tujadili Faida Za Serikali Tatu", nayo pia kama maandalizi wakati tunasubiri uzi maalum kabisa nilio ahidi, Dr. Mdondoaji anasema tunapiga siasa wakati ni yeye ndiye anayefanya political spinning, na kwa vile analemewa, anajieleza kwamba kasoma sana kwamba tulazimike kuona hoja zake ndio absolute.

Dr. Mdondoaji...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi, Mimi nina uhakika kutokana na rasimu iliyotolewa kama itakuwa jinsi ilivyo na kama vyanzo vya mapato vitakua ni hivihivi. Basi gharama za kuendesha serikali tatu zitakuwa ni kubwa zaidi ya gharama za kuendesha serikali moja.

Serikali moja, bila kupotoshana inaweza kuwa decentralized. Serikali ya JMT ni decentralized na bado haina ufanisi wowote. Lakini tuyaache hayo.

Nitakachokuunga mkono wewe ni kuwa kama matakwa ya wananchi ni S3, basi gharama siyo issue kwa sababu haki haijali gharama.

Pia, kila mchumi anaweza kuja na mahesabu yake kuonyesha uzuri wa mfumo fulani, but so far humu jamvini watu wa S3 angalau wameweka wazi mawazo yao.
 
Last edited by a moderator:
Dr. Mdondoaji:

Unajaribu sana kujenga hoja juu ya numbers na kutumia hoja hiyo kutafuta ushindi wakati kama wewe kweli ni PhD holder, majadiliano sio kutafuta ushindi bali kuelimishana, kubadilishana mawazo, ujuzi na uzoefu.

Nadhani sasa ni muhimu for me to explain to you why I don't want to deal with numbers as a starting point, pamoja na wewe kushinikiza sana kwamba Numbers should be the starting point, huku ukija na hoja kwamba nyinyi wachumi mnaamini katika "no facts, no right to speak".

Dr:
Napingana na wewe kuja copy and paste ya bajeti kama framework of analysis to determine mfumo upi wa serikali ni bora for our union. Hii ni kwasababu, nikiazima maneno yako hapo juu
"no facts, no right to speak"
, naunga mkono hoja lakini kuna kitu muhimu zaidi, ninacho amini kama mwananchi wa Kijiweni, nacho ni kwamba:

Numbers don't lie but, the very same numbers may ignore our most important TRUTH

Nikuulize:

Do you know how our most important truth that has been ignored for the last 50 years? Jibu ni kwamba - a lot of it, na ndio maana tunaoitwa "maoni ya wachache" tunajaribu kutumia fursa iliyopo to rectify tatizo lililopo. Lakini kikwazo kikubwa ni kwamba wanaojiita "maoni ya wengi" wanajaribu kuboresha tatizo kupitia serikali tatu, sio kutatua tatizo (rejea mabandiko yangu mwanzoni mwa uzi huu). Kinachoshangaza zaidi ni kwamba, for 50 years, tumegundua serikali mbili hazitufai. Badala ya kuwa na consensus kwamba two subnational governments with fiscal autonomy are inevitable, PhD holders kama Dr. Mdondoaji wanashauri jibu ni serikali moja. Hawa wapo out of touch completely kwani the zanzibar question (1984, 2010), has been all about autonomy and self determination kwa sababu ya mfumo wa serikali mbili. Serikali moja sasa ya nini tena???

Dr. mdondaji pamoja na wanasiasa wetu wana tabia to "over use") statistics, figures, na hilo ndio limekuwa linaendelea katika mfumo wetu wa bajeti na uchumi kwa ujumla. Mnafanya kama vile - it’s for anyone who ‘doesn’t believe it until they see the numbers’.

Ukiwa kama mchumi, ulitakiwa uelewe kwamba huwa pia kuna a false correlation between ‘numbers’ and ‘evidence’. Baadae nitakuonyesha jinsi gani this conflation undermines trust and na pia jinsi gani inapelekea to less-than-honest results, kwa kutumia namba zako hizo hizo za copy and paste.

Tatizo la msingi with numbers halipo katika numbers, per se; tatizo ni where numbers fall in our order-of-operations. Wanasiasa wetu (including you Doctor), mnazitazama numbers kama vile "they are an end point", "they are the holy grail of research and analysis". Kwa miaka 50, matokeo yake yamekuwa ni nini nchini? Halafu mnasema jibu ni serikali mbili au moja????

Nilichojadili #108 ni kujenga hoja kwamba numbers aren't the end to themselves kama wewe na kina Mwigulu mnavyotaka tuaminisha kwa kuchukua bajeti na kuichambua kwa miwani ya mbao. Badala yake,
numbers zinatakiwa kuchukuliwa as a step along the journey towards a better understanding. Ni bahati mbaya sana wewe, mwigulu, "MwanaDiwani" na wengine mnajaribu kufanya numbers kuwa ni
"An end". Katika muktadha huo, ndio maana hamuishiwi na pressure ya kuzichakachua, fiddle them, reconfigure them, ili mradi tu numbers zikidhi matakwa yenu. Ndio maana katika mchezo wa numbers hizo za bajeti, tena ambazo hazina input ya wananchi, hautanipata n'go. Call me foolish or whatever.

As much as you might like to pretend, and even force us kwamba hizo numbers represent "an infallible scientific rigor", tupo wachache wenye uzoefu ambao tunajua fika kwamba hata a figure ambayo may not look as a significant, kwa mfano 0.00000000000000000000000000000000000001, bado namba hii has an interpretive flexibility, hasa kama unaihitaji kuchomeka maslahi ya kisiasa kama yenu.

Kuwa na subira, uzi wa gharama utakuja tu dr Mdondoaji. Iwapo nimekuja na threads nyingi tu (visit my profile), hii ya gharama kwanini inishinde. Yote uliyogusia hapo juu nitayajadili. Sitaki kuja na vitu nusu nusu au kwa mtindo wa viporo. Nadhani umeona hata katika uzi huu, niliandaa kwanza content yote pembeni kisha nikaiweka katika mabandiko mbalimbali ili kuepuka unnecessary interruptions.

Until then, ujue tu kwamba mimi sio msomi kama wewe, ni raia tu mwenye interest ya kujisomea masuala ya siasa, uchumi na kijamii - a reader in these areas. Na kila nikipata muda, nayachambua and share my ideas, hence jina la "mchambuzi".

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe 199%
Haya kawaambie walimu wako nasubiri majibu yangu.

Hahahaaaaaa...
Haya heshima mbele mkuu tuishie hapa na
kazi njema mkuu ila wananchi tunawadai Tanganyika yetu.
Nalala naamka naiota Tanganyika na tutaandika historian mpya.
 
Kama tulivyotabiri, mheshimiwa MwanaDiwani ametukimbia. Ana lundo la hoja za kujibu kutoka kwa wadau, hasa Nguruvi3. Next time tunamuona active in JF pengine ni katika majukwaa ya siasa akiweka picha za makada wa ccm wakipokewa uwanja wa ndege kwa ngoma na nyoka, akijenga hoja kwamba 'hakuna kama CCM, CCM ni nambari wani, chama kinachanja mbuga, vyama vingine ni vya kilaghai, vyama vingine ni vya kifamilia'. Anasahau kwamba taifa hili limeishia kwa ulaghai kwa miaka 50 (cheti cha kuzaliwa muungano kimechakachuliwa); na suala la familia CCM, ndio usiseme kabisa.

Sera ya JF ya kulinda identity ina umuhimu wake, lakini pia ina mapungufu yake kwa vile inatufanya wengi wetu tuwe kama tunaongea na "majini". Inawezekana isiwe na shida katika masuala mengine lakini ni tatizo iwapo inahusisha masuala ya kitaifa, hasa iwapo wahusika ndio decision makers wa maisha ya wananchi milioni 45.

Na misukule ya Lumumba ndio inatumia fursa hii kuleta porojo za nguvu ya giza humu. Lakini wana haja ya kujificha kwani kama wanaojitokeza, hoja zao ndio zile za kina nape, lemutuz, makonda, kigwangalla, tutarajie kitu gani zaidi.

Kilicho Muhimu ni kwamba, Tanganyika inarudi, hata kama sio kesho, na wale wasaliti wote hawatakuwa na nafasi katika ujenzi wa Tanganyika yetu kwani wakipewa nafasi, wataenda kuivuruga ili ionekane ni "failure". Misukule itafanikiwa kupenya penya kwani unafiki wao unawa ficha. Lakini haitachukua muda mrefu kabla na wao kugundulika na watanganyika. Nao watang'oka tu.

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaaaa...
Haya heshima mbele mkuu tuishie hapa na
kazi njema mkuu ila wananchi tunawadai Tanganyika yetu.
Nalala naamka naiota Tanganyika na tutaandika historian mpya.
Tanganyika ni jina tu mkuu. Kuna watu ninaowajua (wamefariki sasa) wameikuta hii ardhi haiitwi jina hilo.
 
Back
Top Bottom