Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maoni yepi?Zaidi ya Miezi minne iliyopita, tulijadili juu ya rasimu ya mafichoni ya CCM iliyo sheheni Viroja vya serikali Mbili zilizoboreshwa. Lakini Kama kawaida, Yao, wale wote ambao wamekuwa wanakaririshwa misimamo ya chama hivyo kushindwa kuchambua issues objectively walikejeli hoja zetu, huku wakihoji hiyo rasimu ya mafichoni Ipo wapi. Sasa tunaona jinsi gani Kamati za BLK kupitia wajumbe wanaojitambulisha Kama ni "wengi", wakileta maoni Yale Yale tuliyojadili miezi minne Iliyopita. Hivi ni Viroja ambavyo Kama Aliyosema EMT, ni sinema inayokaribia ukingoni muda sio mrefu.
Cc MwanaDiwani, chama, Kobello, Dingswayo, Mag3 Nguruvi3 JokaKuu, Jasusi, Pasco, MJINI CHAI, Bongolander, Mtanganyika
Sent from my iPhone using JamiiForums
Nyuma ya sinema hii ya kutisha sijui kuna nani........? kwani MaCCM na wenye mtazamo hafifu wa fikra hawalioni hili........lengo kuu la kundi hilo ni kuipeleka Zanzibar na Tanganyika kwenye inchi moja isiyo ya muungano.........swala la serikali moja ua tatu ni la kubabaisha ili wafunike kombe mwanaharamu apite tu...........................!!!!!!!!!Mchambuzi, hayo mambo sisi wengine tuliyaona toka mapema kabisa na kwa kweli nawapongeza sana UKAWA kutokubali kushiriki huu upuuzi unaofanyika ndani ya eti Bunge Maalum La Katiba. Nakumbuka jinsi Kobello alivyokuwa akitetea kwa kudai eti tukiacha vipengele viwili vilivyohusu muundo wa Muungano vilivyozua utata toka mwanzo vingine kwenye rasimu havingeleta taabu. CCM hawakuwa na nia wala hawajawahi kuwa na nia ya kuandika katiba mpya kwa sababu katiba mpya ingehatarisha mipango yao ya kuhakikisha hawatoki madarakani...tazama wanavyoichachana rasimu na hasa vile vipengele vinavyobana kutowajibika.
Kinachofanywa ndani ya BMLK ni marekebisho/maboresho ya katiba ya zamani na kusema kweli hayakuhitaji Bunge Maalum, yangeweza kufanywa na Bunge la kawaida na hivyo tungeokoa mabilioni yaliyotumika toka mchakato uanze. Hivi kuna mtu yeyote amewahi kuhoji pesa zilizokuwa walipwe wajumbe waliosusia hili Bunge zinakwenda wapi? UKAWA kususia Bunge imekuwa neema kubwa kwa utawala...hizo pesa ambazo wangelipwa si ajabu zinaingizwa kwenye mfuko ule ule zilikoenda za chengi ya rada na ESCROW. Usiku na mchana wanakesha wakiomba msimamo wa UKAWA usibadilike wazidi kufaidi kwa kutafuna shamba la bibi kama nzige.
Mkuu huo ndio ukweli wenyewe safi sana kwa comments zako.........Historia itajirudia na hapo ndipo wale wote wanaoliingiza taifa hili kwenye matumizi mabovu ya mali, machafuko ya fikra, na kutokutimiza majukumu yao lazima mkono wa sheria uwaguse.............Unafiki ni kitu kibaya sana.....baadhi ya Wajumbe wa BMLK wanakuwa 'Mabubu', nashangaa sana..........!!!!Ndugu wanajamvi,
Katika hotuba yake ndani ya Bunge la Katiba mjini Dodoma hivi karibuni, Rais Kikwete, pamoja na mengineyo, alinukuliwa akisema kwamba – muungano wa serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu ya katiba haufai kwa kuwa ni ‘mfumo legevu na utawaongezea wananchi mzigo'. Rais Kikwete pia alienda mbali na kueleza kwamba:
Hapa Rais Kikwete alikuwa akimaanisha mfumo wa serikali mbili ambao CCM imesema "itauboresha", kama njia ya kuondoa kero za muungano zilizodumu kwa zaidi ya miaka 30. Kufuatia hotuba hii ya Rais Bungeni, huu ukawa ndio msingi wa hoja za kile kilichoitwa "Maoni Ya Wengi" ndani ya bunge maalum la Katiba. Na ni msimamo huu wa "Maoni ya Wengi" ambao pia ukapelekea upande mwingine wa hoja, ulioitwa "Maoni ya Wachache", hatimaye kuamua kujiondoa katika bunge hili, chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa nia ya kwenda kuwaeleza wananchi jinsi gani waliojiita "wengi" bungeni walivyoamua kupuuza maoni ya wananchi kuhusiana na rasimu ya katiba.'
Kama tutakavyojadili, Muungano wa Serikali Mbili "Zilzoboreshwa", kama unavyopigiwa kampeni na CCM, hautaimarisha Muungano na hautamaliza malalamiko, lawama na shutuma za kero za Muungano. Badala yake, Serikali mbili "zilizoboreshwa", zitavunja na kuuzika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu tatu.
Sehemu ya kwanza tutajadili:
· Muundo Wa Serikali.
· Madaraka ya Viongozi.
· Muundo Wa Bunge.
Hapa tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa yataenda kuvunja muungano.
Sehemu ya pili tutajadili:
· Mapato na Matumizi Ya Kuendesha Muungano.
· Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mikopo, na Misaada.
· Mapendekezo ya Baraza la Mapinduzi kuhusu masuala ya kuyaondoa katika Orodha ya mambo ya Muungano.
Vile vile, tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili "zilizoboreshwa" yataishia kuvunja muungano.
Na Sehemu ya TATU tutajadili:
· Sheria Za Ndani na Nje ya Muungano.
· Mgongano wa Kikatiba.
· Kuzinduka kwa Utaifa kwa pande zote mbili za Muungano (Tanganyika na Zanzibar). Muungano.
Hapa pia tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili "zilizoboreshwa" yataenda kuvunja muungano.
SEHEMU YA KWANZA
MUUNDO WA SERIKALI, MADARAKA YA VIONGOZI NA MUUNDO WA BUNGE
Katika hotuba yake bungeni, Rais Kikwete aliwahimiza wajumbe wa Bunge la Katiba juu ya umuhimu wa kuwaenzi Waasisi wa Muungano (Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume), kwa vile wao ‘walitaka na walituachia mfumo wa serikali mbili'. Wanaojiita "Maoni Ya Walio Wengi" Bungeni, ambao wanapigia chepuo mfumo wa serikali mbili "zilizoboreshwa" wanafahamu kwamba – muundo wa muungano ulioachwa na waasisi wetu ulikuwa ni ‘muungano wa NCHI MOJA, yenye SERIKALI MBILI. Zanzibar ilikuwa ni SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO. Hiyo ndio hali ya Muungano ambayo Mwalimu Nyerere alipofariki kumi na tano iliyopita. Leo hii Zanzibar sio tu kwamba tayari imeshaondoa mambo mengi ya msingi juu ya "muungano", bali pia, kwa mujibu wa marekebisho ya kumi ya Katiba (2010), Zanzibar haitambuliwi tena kama ni "sehemu" ya muungano, bali inatambulika (Kikatiba) kama "nchi kamili", yenye bendera yake, wimbo wake wa taifa, na amiri jeshi mkuu.
Pamoja na Muungano sasa kuwa na Nchi MBILI, SERIKALI MBILI, CCM bado inasema kwamba serikali mbili hizi "zitaziboreshwa", huku chama kikipendekeza kwamba – katika katiba ijayo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano (ambae leo hii ni Dr. Bilal), anyang'anywe mamlaka aliyokuwa nayo ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, na badala yake, mamlaka hayo yahamie kwa Rais wa nchi jirani ya "Zanzibar". Kwa maana nyingine, chini ya serikali mbili "zilizoboreshwa" na CCM, Rais wa nchi jirani ya "Zanzibar" atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais wa Muungano kwa masuala ya Zanzibar, lakini pia atakuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa nchi (Tanzania). CCM haisemi lolote kuhusu kiongozi atakayekuwa msaidizi wa Rais wa Muungano katika masuala ya Tanganyika (ukipenda, sema - Tanzania Bara).
Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao – Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili – Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Kawawa).
Chini ya Katiba Mpya, CCM inapendekeza kwamba – Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM inadai kwamba – hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - "madaraka na hadhi" ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi.
MGOGORO UTAKAOJITOKEZA KUTOKANA NA MAPENDEKEZO YA RAIS WA ZANZIBAR KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
Chini ya mfumo huu wa serikali mbili "zilizoboreshwa", CCM haisemi iwapo Rais ni mmoja - yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanzania Bara katika mfumo huu wa serikali mbili "ulioboreshwa". Pamoja na kuendelea kupigia debe serikali mbili "zitakazoboreshwa", CCM bado imeendelea kukaa kimya juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni "nchi" kamili, yenye "mamlaka" kamili, ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:
· Rais huyu kutoka nchi jirani ya "Zanzibar" atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa "Tanzania Bara", ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?
· Iwapo Rais wa Muungano atatokea panapoitwa "Tanzania Bara", Rais huyu wa Muungano atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia mambo ya "Tanzania Bara" wakati yeye atakuwa amechaguliwa na wananchi wa pande zote mbili za muungano?
· Zipo wapi ‘pande mbili' za muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika?
CCM haina muda wa kutoa majibu kwa maswali haya muhimu. Kutokana na hali hii, serikali mbili "zilizoboreshwa", hazitaboresha muungano bali zitajenga mazingira ya kuvunja muungano. Hii ni kwa sababu:
Tuseme Rais wa Muungano anatokea upande wa nchi jirani ya "Zanzibar", ambaye chini ya mfumo wa serikali mbili ambao CCM inadai utakuwa "umeboreshwa", Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM inapendekeza kuwa iwe hivyo bila ya kujali Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano. Kitakachotokea ni kwamba - siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea nchi jirani ya "Zanzibar". Kwa maana hii, inachokifanya CCM, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM inaweka mazingira ambayo Zanzibar hawataweza tena kutoa Rais wa Muungano. Hii ni kwa sababu:
Kama tulivyoona, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Rais wa Zanzibar "automatically", atakuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM ikimsimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea nchi jirani ya "Zanzibar", nchi ambayo pia automatically itatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa "Tanzania Bara", upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, wengi ya wapiga kura hawa kutoka "Tanzania Bara", hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea nchi ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko "nchini" Zanzibar. Madhara yake ni yepi?
Ni kwamba – chini ya mfumo wa Serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Zanzibar ianze kusahau kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitachofuatia ni Zanzibar kuanza kulalamika kwamba wanabaguliwa, wanonewa, wananyimwa haki ndani ya Jamhuri ya muungano, kwahiyo waachwe "Wapumue". And interestingly enough, watakaongoza katika kutoa hoja hizi ni wale wale wazanzibari ambao Islaml Jusa alisema kwamba walipofika Dodoma "Waliufyata". Ni wale wale ambao leo wanapinga kwamba wao sio "wasaka tonge". Katika kundi hili, hatutashangaa kuja kuona viongozi kama Balozi Seif Iddi, Mohamed Seif Khatib, Hamad Rashid Mohamed, na wengine wakija unga mkono hoja hii. Hatujui bado, lakini haitashangaza! Hali hii haitadumisha au kuboresha Muungano bali itauvunja Muungano.
Kwa upande wa inayoitwa "Tanzania Bara", iwapo Mgombea Urais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake "automatically" pia atatokea Zanzibar, watakaoongoza katika kupinga hali hii haitakuwa watu wengine bali wale wale makada wa CCM ambao leo ndani ya bunge la katiba wanajiita "Maoni ya Walio Wengi", wanaotetea mfumo huu huu wa serikali mbili "zilizoboreshwa". Fitina zilizomkumba Dr. Salim Ahmed Salim 2005 hazitafua dafu kwa fitina zitakazojitokeza katika mazingira tunayojadili hapa. Wana CCM ambao watakuwa katika makundi ya kutafuta Rais wa Muungano wataendesha kampeni kubwa kupinga uongozi wa Muungano kwenda kwa "nchi jirani katika kofia zote mbili za juu – Rais wa Muungano na Makamu wa Rais wa Muungano.
Aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya, wanachoambiwa Wazanziri na CCM ni kwamba - chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, Wazanzibari wajiandae kuwa ni "wasindikizaji" tu wa Uongozi katika Jamhuri ya Muungano. Pia CCM nayo ijiandae kutupiwa lawama na malalamiko mapya juu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar. Mbegu ya kuvunjika kwa muungano itaanza kuchepuka.
Inaendelea bandiko linalofuatia…
cc - Nguruvi3, @FJM,@ tpaul, @Mag3, @JokaKuu, @Mwigulu Nchemba, @Nape Nnauye, @MwanaDiwani,@zomba, @Ritz, @ZeMarcopolo, @Gamba la Nyoka, @Mtanganyika , @Mzee Mwanakijiji, @Pasco, @Kitila Mkumbo, @EMT, @MTAZAMO, @Kobello,@Jasusi, @zumbemkuu, @Mimibaba, @Zakumi, @Invisible, Tumaini Makene, @Yericko Nyerere, @FaizaFoxy, @Dingswayo, @Makusudically, @Tumaini Makene, @Nicholas, @Mtu wa Pwani, @jmushi1, @Mwita Maranya, @Ngongo, @zumbemkuu, Zitto, @Mzawa Halisi, Barubaru, Mindi, Kiganyi, @Communist, Dr. F. Ndungulile, Ezekiel Maige, Anna Tibaijuka, HKigwangalla, candidscope, tpaul, Tetty, TIMING, chama
Ndiyo.Unafuatilia maoni ya Kamati za bunge Dodoma, hasa maoni ya walio wengi?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mbona mnayeyusha?
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.Ndugu wanajamvi,
Katika hotuba yake ndani ya Bunge la Katiba mjini Dodoma hivi karibuni, Rais Kikwete, pamoja na mengineyo, alinukuliwa akisema kwamba muungano wa serikali tatu uliopendekezwa katika rasimu ya katiba haufai kwa kuwa ni mfumo legevu na utawaongezea wananchi mzigo. Rais Kikwete pia alienda mbali na kueleza kwamba:
Hapa Rais Kikwete alikuwa akimaanisha mfumo wa serikali mbili ambao CCM imesema itauboresha, kama njia ya kuondoa kero za muungano zilizodumu kwa zaidi ya miaka 30. Kufuatia hotuba hii ya Rais Bungeni, huu ukawa ndio msingi wa hoja za kile kilichoitwa Maoni Ya Wengi ndani ya bunge maalum la Katiba. Na ni msimamo huu wa Maoni ya Wengi ambao pia ukapelekea upande mwingine wa hoja, ulioitwa Maoni ya Wachache, hatimaye kuamua kujiondoa katika bunge hili, chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa nia ya kwenda kuwaeleza wananchi jinsi gani waliojiita wengi bungeni walivyoamua kupuuza maoni ya wananchi kuhusiana na rasimu ya katiba.
Kama tutakavyojadili, Muungano wa Serikali Mbili Zilzoboreshwa, kama unavyopigiwa kampeni na CCM, hautaimarisha Muungano na hautamaliza malalamiko, lawama na shutuma za kero za Muungano. Badala yake, Serikali mbili zilizoboreshwa, zitavunja na kuuzika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu tatu.
Sehemu ya kwanza tutajadili:
· Muundo Wa Serikali.
· Madaraka ya Viongozi.
· Muundo Wa Bunge.
Hapa tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa yataenda kuvunja muungano.
Sehemu ya pili tutajadili:
· Mapato na Matumizi Ya Kuendesha Muungano.
· Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa, Mikopo, na Misaada.
· Mapendekezo ya Baraza la Mapinduzi kuhusu masuala ya kuyaondoa katika Orodha ya mambo ya Muungano.
Vile vile, tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa yataishia kuvunja muungano.
Na Sehemu ya TATU tutajadili:
· Sheria Za Ndani na Nje ya Muungano.
· Mgongano wa Kikatiba.
· Kuzinduka kwa Utaifa kwa pande zote mbili za Muungano (Tanganyika na Zanzibar). Muungano.
Hapa pia tutaonyesha jinsi gani masuala haya chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa yataenda kuvunja muungano.
SEHEMU YA KWANZA
MUUNDO WA SERIKALI, MADARAKA YA VIONGOZI NA MUUNDO WA BUNGE
Katika hotuba yake bungeni, Rais Kikwete aliwahimiza wajumbe wa Bunge la Katiba juu ya umuhimu wa kuwaenzi Waasisi wa Muungano (Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume), kwa vile wao walitaka na walituachia mfumo wa serikali mbili. Wanaojiita Maoni Ya Walio Wengi Bungeni, ambao wanapigia chepuo mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa wanafahamu kwamba muundo wa muungano ulioachwa na waasisi wetu ulikuwa ni muungano wa NCHI MOJA, yenye SERIKALI MBILI. Zanzibar ilikuwa ni SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO. Hiyo ndio hali ya Muungano ambayo Mwalimu Nyerere alipofariki kumi na tano iliyopita. Leo hii Zanzibar sio tu kwamba tayari imeshaondoa mambo mengi ya msingi juu ya muungano, bali pia, kwa mujibu wa marekebisho ya kumi ya Katiba (2010), Zanzibar haitambuliwi tena kama ni sehemu ya muungano, bali inatambulika (Kikatiba) kama nchi kamili, yenye bendera yake, wimbo wake wa taifa, na amiri jeshi mkuu.
Pamoja na Muungano sasa kuwa na Nchi MBILI, SERIKALI MBILI, CCM bado inasema kwamba serikali mbili hizi zitaziboreshwa, huku chama kikipendekeza kwamba katika katiba ijayo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano (ambae leo hii ni Dr. Bilal), anyanganywe mamlaka aliyokuwa nayo ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, na badala yake, mamlaka hayo yahamie kwa Rais wa nchi jirani ya Zanzibar. Kwa maana nyingine, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Rais wa nchi jirani ya Zanzibar atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais wa Muungano kwa masuala ya Zanzibar, lakini pia atakuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa nchi (Tanzania). CCM haisemi lolote kuhusu kiongozi atakayekuwa msaidizi wa Rais wa Muungano katika masuala ya Tanganyika (ukipenda, sema - Tanzania Bara).
Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Kawawa).
Chini ya Katiba Mpya, CCM inapendekeza kwamba Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM inadai kwamba hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - madaraka na hadhi ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi.
MGOGORO UTAKAOJITOKEZA KUTOKANA NA MAPENDEKEZO YA RAIS WA ZANZIBAR KUWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
Chini ya mfumo huu wa serikali mbili zilizoboreshwa, CCM haisemi iwapo Rais ni mmoja - yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanzania Bara katika mfumo huu wa serikali mbili ulioboreshwa. Pamoja na kuendelea kupigia debe serikali mbili zitakazoboreshwa, CCM bado imeendelea kukaa kimya juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni nchi kamili, yenye mamlaka kamili, ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:
· Rais huyu kutoka nchi jirani ya Zanzibar atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa Tanzania Bara, ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?
· Iwapo Rais wa Muungano atatokea panapoitwa Tanzania Bara, Rais huyu wa Muungano atakuwa na mamlaka yepi ya kusimamia mambo ya Tanzania Bara wakati yeye atakuwa amechaguliwa na wananchi wa pande zote mbili za muungano?
· Zipo wapi pande mbili za muungano bila ya kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika?
CCM haina muda wa kutoa majibu kwa maswali haya muhimu. Kutokana na hali hii, serikali mbili zilizoboreshwa, hazitaboresha muungano bali zitajenga mazingira ya kuvunja muungano. Hii ni kwa sababu:
Tuseme Rais wa Muungano anatokea upande wa nchi jirani ya Zanzibar, ambaye chini ya mfumo wa serikali mbili ambao CCM inadai utakuwa umeboreshwa, Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM inapendekeza kuwa iwe hivyo bila ya kujali Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano. Kitakachotokea ni kwamba - siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea nchi jirani ya Zanzibar. Kwa maana hii, inachokifanya CCM, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM inaweka mazingira ambayo Zanzibar hawataweza tena kutoa Rais wa Muungano. Hii ni kwa sababu:
Kama tulivyoona, chini ya serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Rais wa Zanzibar automatically, atakuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM ikimsimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea nchi jirani ya Zanzibar, nchi ambayo pia automatically itatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa Tanzania Bara, upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, wengi ya wapiga kura hawa kutoka Tanzania Bara, hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea nchi ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko nchini Zanzibar. Madhara yake ni yepi?
Ni kwamba chini ya mfumo wa Serikali mbili zilizoboreshwa na CCM, Zanzibar ianze kusahau kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kitachofuatia ni Zanzibar kuanza kulalamika kwamba wanabaguliwa, wanonewa, wananyimwa haki ndani ya Jamhuri ya muungano, kwahiyo waachwe Wapumue. And interestingly enough, watakaongoza katika kutoa hoja hizi ni wale wale wazanzibari ambao Islaml Jusa alisema kwamba walipofika Dodoma Waliufyata. Ni wale wale ambao leo wanapinga kwamba wao sio wasaka tonge. Katika kundi hili, hatutashangaa kuja kuona viongozi kama Balozi Seif Iddi, Mohamed Seif Khatib, Hamad Rashid Mohamed, na wengine wakija unga mkono hoja hii. Hatujui bado, lakini haitashangaza! Hali hii haitadumisha au kuboresha Muungano bali itauvunja Muungano.
Kwa upande wa inayoitwa Tanzania Bara, iwapo Mgombea Urais wa Muungano atatokea nchi jirani ya Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake automatically pia atatokea Zanzibar, watakaoongoza katika kupinga hali hii haitakuwa watu wengine bali wale wale makada wa CCM ambao leo ndani ya bunge la katiba wanajiita Maoni ya Walio Wengi, wanaotetea mfumo huu huu wa serikali mbili zilizoboreshwa. Fitina zilizomkumba Dr. Salim Ahmed Salim 2005 hazitafua dafu kwa fitina zitakazojitokeza katika mazingira tunayojadili hapa. Wana CCM ambao watakuwa katika makundi ya kutafuta Rais wa Muungano wataendesha kampeni kubwa kupinga uongozi wa Muungano kwenda kwa nchi jirani katika kofia zote mbili za juu Rais wa Muungano na Makamu wa Rais wa Muungano.
Aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya, wanachoambiwa Wazanziri na CCM ni kwamba - chini ya mfumo wa serikali mbili zilizoboreshwa, Wazanzibari wajiandae kuwa ni wasindikizaji tu wa Uongozi katika Jamhuri ya Muungano. Pia CCM nayo ijiandae kutupiwa lawama na malalamiko mapya juu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar. Mbegu ya kuvunjika kwa muungano itaanza kuchepuka.
Inaendelea bandiko linalofuatia
cc - Nguruvi3, @FJM,@ tpaul, @Mag3, @JokaKuu, @Mwigulu Nchemba, @Nape Nnauye, @MwanaDiwani,@zomba, @Ritz, @ZeMarcopolo, @Gamba la Nyoka, @Mtanganyika , @Mzee Mwanakijiji, @Pasco, @Kitila Mkumbo, @EMT, @MTAZAMO, @Kobello,@Jasusi, @zumbemkuu, @Mimibaba, @Zakumi, @Invisible, Tumaini Makene, @Yericko Nyerere, @FaizaFoxy, @Dingswayo, @Makusudically, @Tumaini Makene, @Nicholas, @Mtu wa Pwani, @jmushi1, @Mwita Maranya, @Ngongo, @zumbemkuu, Zitto, @Mzawa Halisi, Barubaru, Mindi, Kiganyi, @Communist, Dr. F. Ndungulile, Ezekiel Maige, Anna Tibaijuka, HKigwangalla, candidscope, tpaul, Tetty, TIMING, chama