CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Kodi, mikopo na mainly misaada
Kwa majibu haya huna sababu za kuhoji tume ya Warioba. Ingekuwa ni rahisi kiasi hicho tungeshapata katiba. Hata wewe mwenyewe unaona aibu kueleza maana ni aibu ab initio
 
Kobello please, hapa ni JF; hiyo analogy ya mke is below your dignity...tafadhali usitupeleke huko. On second thought, may be I jumped the gun...tafadhali naomba ufafanuzi; katika mada tuliyo nayo, ni nani huyo unayemsema kwamba pamoja na kutegemea msaada bado anataka kuongeza mke?
Mku hiyo ilikuwa ni njama ya kukwepa hoja. Kila jitihada inafanyika kuingiza S3 katika mjadala. Ni jambo zuri kwasababu S3 zinahoja. Kuna kurasa 106 na zaidi. S2 hakuna hoja ndiyo hayo ya mke, mchumba n.k.

Hakuna hoja kwa S2 watu wanaishi kwa mazoea tu. Nimeshangaa Mdondoaji ameikana znz huru. Nimesikitika sana.
Tukamuuliza hizo S2 alizokuwa anazilaani miaka nenda rudi zimeshawishi kitu gani? hakika hana jibu.

Huu uzi nilitegemea kusikia mengi kutoka S2 kwasababu ndiyo mada. Utashangaa watu wanarukia S3.
Hizo S2 zinakitu gani tukijadili halafu tufanye ulinganisho, hawataki wanataka tukijikite kumtukana Warioba.

Warioba ana substance, ungeona ITV interview ungejua kwanini alitangulizwa bungeni.
Sasa hivi ni star ndio maana ana 'nyodo' ya kwenda media yoyote. Yes, anacho cha kusema!
 
Ok kama unadhani njia njema ni kuvunja tugawane mbao kwanini unatetea S2?

Hilo la rasimu ya CCM , endapo rasimu ya CCM kutetea S2 haipo (assume), kwa maneno mengine CCM na akina Kobello na MwanaDiwani wanataka S2 kwasababu wanataka tu.

Hawana sababu wala hoja kwanini wanataka 2. Kungekuwa na hoja mbadala ungepatikana.
Hivi hapa huoni Warioba anasimama wima.
Yeye kaonyesha kitu hata kama hamkubaliani nacho.
Vipi mnachokubaliana nacho cha S2 kiko wapi?

Kwavile hakuna hoja za kukubaliana na Warioba, hoja kuu sasa ni kumdhalilisha, kumshambulia na kuzusha uongo.

Kobello sera za Lukuvi makanisani ndizo S2 imara na hakika mnasimama kutetea hilo?
Kobello, jeshi halitakuwa na fedha za kutosha, tuelezeni za sasa zinatoka wapi?
Serikali ya shirikisho haitakuwa na vyanzo vya uhakika, tuonyesheni vya sasa vinapatikanaje
Bunge la Tanzania bara (nchi ya ahadi) litakuwa linahudumiwa na serikali gani?

Kama hayo hamna majibu lipo hili rahisi
Kwa maiaka 50 kwanini kero hazikumalizwa hadi kutishia uhai wa muungano?
Ninyi wa S2 mnadhani nini kifanyike kwasasa tofauti na mapendekezo ya Warioba?

Ni ajabu kumshambulia Warioba kukiwa hakuna karatasi mezani kuonyesha mnataka kufanya nini.
Kama ni hayo ya Lukuvi fungukeni msione aibu.
[/FONT][/SIZE]
Mimi ninachosimamia ni kutokuwepo kwa federation. Hasa kwa federation inayoundwa na nchi mbili tofauti.
I am against EAC, EU, and the likes. I can understand fedrations za Nigeria, US, China etc ... but our federation will not be like US. It will be more like EU which is just a bureaucracy.

Tukiacha hayo, wewe niambie kinachokuaminisha kuwa mimi ni mhanga wa serikali mbili. Siyo ukisikia mtu ni mwana CCM basi unamuhusisha na S2, huo ni upotoshaji. Mimi wala sioni umuhimu wa katba mpya, ila nchi siyo yangu peke yangu na watachotaka wenzangu wengi(wananchi) ni wajibu wangu kukiheshimu.
 
Kwa majibu haya huna sababu za kuhoji tume ya Warioba. Ingekuwa ni rahisi kiasi hicho tungeshapata katiba. Hata wewe mwenyewe unaona aibu kueleza maana ni aibu ab initio
Tatizo lako wewe ni kukariri talking points. Ni kama mtu fulani ambaye ushaamini mambo fulani ni lazima yaende na mambo fulani.

Mimi nimeshakujibu sana kwenye uzi huu, tena sana na sababu siyo kwamba sina vitu vya maana vya kufanya ila nataka nisikie kile unachokitetea labda mawazo yangu yanaweza kubadilika. Mimi mpaka sasa naona mnarudia talking points, mnaquote vitu ambavyo mkiambiwa mvilete humu mnayeyusha.

Nimetoa links, tables, arithmetic concepts ila ninachoona toka kwako ni maneno tu as if upo unahutubia. Usitegemee a one traffic flow of information when arguing with me, thats a nah nah. Ukiuliza maswali rahisi nakujibu kirahisi, usiporidhika na majibu ujsikimbilie kwenye kejeli na dhihaka bali kuwa gentleman au elezea exaCTLY ni kitu gani unachotaka.

Hizo ndiyo sources za mapato ya serikali na kuna bandiko chini yake nimekupa data kutoka BOT. Kwa kifupi hizo ndiyo sources za mapato na ni vitu very basic wala usitake kuvifanya ni vigumu.
 
MwanaDiwani
Katika dunia kuna watu ni vituko huyu Mchambuzi ni mmoja katika vituko hivyo; hivi inakuingia akilini kwamba Mchambuzi yupo hapa kupayuka kwa minajili ya kutetea watanzania wa kawaida??.
Sitetei watanzania, natetea hoja ambayo pia inaungwa mkono na watanzania wengi walitoa maoni kwa tume ya mabadiliko ya Katiba. Wewe na MwanaDiwani mnatetea "ujinga", kwa kuazima maneno ya Mwalimu kwamba yapo ya maana na yapo ya kijinga kufanyia wananchi. Ujinga mnaotetea nimeujadili kwenye mabandiko yangu ya awali, lakini mmekuwa hodari wa kukwepa hoja iliyo mbele yenu, na badala yake kubwabwaja tu kama mlivyofundishwa na kukaririshwa na kina Nape na Mwigulu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Asilimia 76 ya wazanzibari walitoa maoni yao kuhusu muungano, na asilimia 6 ya watanzania bara walitoa maoni yao kuhusu muungano.
Asilimia 14 ya watanzania walitoa maoni yao juu ya muungano. Wazanzibari kwa ujumla walizungumzia muungano na watanzania bara waigawaqnmyika katika issues mbalimbali.
Huwezi kumuuliza mtoa maoni, ni suala lipi linamtatiza, halafu umpe limit ya kuzungumzia suala moja. Halafu uca-compile data na kusema asilimia kubwa ya watanzania walizungumzia muungano; Hapo utakuwa umekosea.

Ingetakiwa watu 200,000 walizungumzia muungano, 101,000 walitaka serikali tatu ... hapo utaconclude kuwa majority walitaka serikali 3.
Jedwali na taarifa zimekanganya watu, kubalini tu.

Mkuu Kobello kwani hapa ukunijibu
Naomba tafsiri yako kwa hili jedwali hapo chini ili nione tafsiri yako ni kwa muundo tu au mambo mengine.

Maaeneo yaliyozungumziwa yalikua Maeneolilizungumziwa sana eneo la haki za binadamu (watu 105,969 sawa na 13.7% ya wazungumzaji wote) ikifatiwa na muungano (watu 80,119 sawa na 10.4% ya wazungumzaji wote).

Naomba unijibu maswali yangu haya
  1. Unakubali wananchi waliozungumza na tume walizungumzia muungano?
  2. Na asilimia kubwa walizungumzia muundo wa muungano?
  3. Na asilimia kubwa walipendekeza s3?

Nanukuu maneno ya Warioba akihutubia bunge maalum la katiba
Warioba said:
Tume ilianza kazi kwa madhumuni ya kupata maoni ya wananchi ili kuboresha Muungano. Wananchi wengi waliotoa maoni kuhusu Muungano, walijikita kwenye Muundo wake kama njia ya kuondoa kero. Kwa Tanzania Bara, wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu Muungano na kati ya hao, karibu 27,000 walizungumzia muundo. Kwa Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwenye suala la Muungano. Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni kuhusu Muungano, wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano. Mchanganuo wa takwimu hizi unaonyesha kuwa wananchi waliotoa maoni kuhusu muundo wa Muungano kwa upande wa Tanzania Bara, 13% walipendelea Serikali Moja, 24% walipendekeza Serikali Mbili na 61% walipendekeza Serikali Tatu. Kwa upande wa Zanzibar, 34% walipendekeza Serikali mbili na 60% walipendekeza Muungano wa Mkataba, na 0.1% (watu 25)walipendekeza Serikali Moja

Jedwali hapa chini linaonyesha maeneo yalizungumzwa kwa wingi.
changiwa.jpg

4. Sasa naomba uniambie zaidi ya haki za binadamu eneo gani lingine kati ya maeneo 47 lililozungumziwa sana zaidi ya Muungano?
 
Attachments

  • muundo.jpg
    muundo.jpg
    76 KB · Views: 62
Last edited by a moderator:
Sitetei watanzania, natetea hoja ambayo pia inaungwa mkono na watanzania wengi walitoa maoni kwa tume ya mabadiliko ya Katiba. Wewe na MwanaDiwani mnatetea "ujinga", kwa kuazima maneno ya Mwalimu kwamba yapo ya maana na yapo ya kijinga kufanyia wananchi. Ujinga mnaotetea nimeujadili kwenye mabandiko yangu ya awali, lakini mmekuwa hodari wa kukwepa hoja iliyo mbele yenu, na badala yake kubwabwaja tu kama mlivyofundishwa na kukaririshwa na kina Nape na Mwigulu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Bado unadhihirisha ujinga wako; wewe unatetea nafsi yako au watanzania?? watanzania sio mahayawani wanajua wanachokitaka; wewe unatumika tu hao watanzania unaowatetea wewe wako wapi??? watanzania wapo shwari wanasubiri wapelekewe machakato wautolee maamuzi; wewe endelea kutumika utapayuka kama uliyekunywa maji ya chooni lakini huna utakachofanikiwa.
 
Ungeweza kuandika bila matusi na kueleweka vema tu.
Kwa mfano ungesema hivi tungekuelewa ''watanzania sio mahayawani wanajua wanachokitaka.watanzania wapo shwari wanasubiri wapelekewe machakato wautolee maamuzi''

chama , hivi watapelewa nini maana hadi sasa S2 hazina cha kupeleka. Si unaona hata jamvini hakuna kinacholetwa kuhusu S2, sasa kitapelekwa kipi?

Zaidi ya hapo watanzania wakiambiwa muundo ni serikali 20 kila mmoja na rais na balozi UN, baasi watolee mamuuzi tu kwasababu wanasubiri kupelekewa, hawana nafasi ya kufikiria.
Ndivyo unavyomaaninsha !!!

Nijuavyo, wananchi wanatakiwa wawe sehemu ya mchakato na si sehemu ya 'kupelekewa'
Walipelekewa mwaka 1965, 1967 na 1977 matatizo tunayaona. Je, wasubiri kupelekewa tena 2014?

Yale yanayosemwa Tanzania ina watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri ni matusi au ni ukweli?

Last edited by a moderator:
Nguruvi3
Nilichosema sio tusi ni kiswahili fasaha kinachoeleweka tatizo lenu mkipewa makavu mnalia sana; watanzania ni watu wenye mkubwa sana wa kifikra na ndio maana tunakuwa tukiwapuuza watu wa aina yenu vinginevyo tungeshakuwa na boko haram; wewe humu jamvini unataka tuseme nini wakati sisi wanaCCM tumeshaweka wazi misimamo yetu? rudia kusikiliza hotuba ya mwenyekiti wa CCM utapata majibu yako siyo lazima ukubaliane nayo lakini hicho ndicho tulichosimamia tunasubiri mchakato umalizwe kwenye bunge la katiba wananchi watolee maamuzi. Tatizo lako na hao Chadema wenzako kina Mchambuzi ni kutaka kufanya mawazo ya Chadema yanawakilisha watanzania wote; nyie endeleeni na UKAWA sisi CCM ni chama dume tunakubalika hatuhitaji ndoa za mikeka.
 
Last edited by a moderator:
Bado unadhihirisha ujinga wako; wewe unatetea nafsi yako au watanzania?? watanzania sio mahayawani wanajua wanachokitaka; wewe unatumika tu hao watanzania unaowatetea wewe wako wapi??? watanzania wapo shwari wanasubiri wapelekewe machakato wautolee maamuzi; wewe endelea kutumika utapayuka kama uliyekunywa maji ya chooni lakini huna utakachofanikiwa.
chama,

Unatumika lakini bado unatafuta kutumika ili uweze kutumikia tumbo lako vilivyo. Hauwezi kujifananisha na mimi, wewe ni mtu unayelipwa na Lumumba elfu kadhaa kwa siku just to make a statement for ccm. Mimi nilishaingia humo lakini nimeona hatari iliyipo kwa ccm na muungano, so I decided to side na maoni ya wananchi kwani wao ndio waamuzi. Given my background, if I wanted kutumikia ujinga (refer mwalimu), ningekuwa maili elfu moja mbele yako na hata MwanaDiwanin lakini nimeona mantiki ipo wapi, siwezi tetea ujinga (refer mwalimu).

Rejea mabandiko yangu ya awali - serikali mbili zilizoboreshwa zinadumisha na kuboresha vipi muungano? Kwanini unakimbia kujibu hii hoja?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
We unasema muungano Utakufa,mbona umedumu kwa miaka hamsini pamoja na mapungufu yaliyopo? Kwa nini usingevunjika huko tulikotoka?
 
chama,

Unatumika lakini bado unatafuta kutumika ili uweze kutumikia tumbo lako vilivyo. Hauwezi kujifananisha na mimi, wewe ni mtu unayelipwa na Lumumba elfu kadhaa kwa siku just to make a statement for ccm. Mimi nilishaingia humo lakini nimeona hatari iliyipo kwa ccm na muungano, so I decided to side na maoni ya wananchi kwani wao ndio waamuzi. Given my background, if I wanted kutumikia ujinga (refer mwalimu), ningekuwa maili elfu moja mbele yako na hata MwanaDiwanin lakini nimeona mantiki ipo wapi, siwezi tetea ujinga (refer mwalimu).

Rejea mabandiko yangu ya awali - serikali mbili zilizoboreshwa zinadumisha na kuboresha vipi muungano? Kwanini unakimbia kujibu hii hoja?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi
Mimi sio tegemezi siishi kwa posho za Lumumba sijawahi na sitawahi; wewe ndiye unayetumika unajionesha kadri ya siku zinavyokwenda ndio maana upo hapa kuipiga madongo CCM; kwanza badili avater vaa khaki ili tujadialIne kwa mapana na marefu. Unajichanganya sana na shati la kijani!!
 
Last edited by a moderator:
chama unavuruga mjadala, inaonekana umepotea njia kuingia humu, hii hoja inakuzidi kimo...umekazania tu kutukana na kujadili watu, hapakufai hapa, yaonekana haujui hata mada inayoongelewa inahusu nini!
 
wewe acha hizo mjadala mnauvuruga nyie kwa kulamizimisha mambo; hapa lazima kieleweke kama mmeshindwa kuhilimili makavu uhamisheni kule kwa Nguruvi3 Duru za siasa.
 
Last edited by a moderator:
chama unavuruga mjadala, inaonekana umepotea njia kuingia humu, hii hoja inakuzidi kimo...umekazania tu kutukana na kujadili watu, hapakufai hapa, yaonekana haujui hata mada inayoongelewa inahusu nini!

Hadi sasa chama hajajibu hoja, sijui kama anajua hilo. Serikali mbili zilizoboreshwa zitaboresha vipi muungano? Nimejadili kwanini maboresho hayo yatakuwa ni "kero zilizoboreshwa", na sio kingine. Sio yeye wala Mwanadiwani ambao wamejibu hoja hii.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hadi sasa chama hajajibu hoja, sijui kama anajua hilo. Serikali mbili zilizoboreshwa zitaboresha vipi muungano? Nimejadili kwanini maboresho hayo yatakuwa ni "kero zilizoboreshwa", na sio kingine. Sio yeye wala Mwanadiwani ambao wamejibu hoja hii.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi
Napata wasiwasi sana na upeo wako wa kuelewa; kuna tofauti kubwa sana kati ya mapendekezo na maamuzi , uliyoleta hapa ni mapendekezo ambayo hayajatolewa uamuzi kumbuka rasimu ya katiba mwisho wa yote itapelekwa kwa wananchi kwa uamuzi wa mwisho; katiba ni maridhiano kwa hiyo hoja yako bado haina nguvu kinachofanyika sasa hivi ni kuangalia namna gani kero zinazosemwa zipo zitaondolewa; kwa mapendekezo ya CCM yanaweza yasiwe suluhisho ya kero lakini lengo lake ni kuleta sura ya kitaifa zaidi na kuulinda muungano. Sio serikali 2 wala 3 zitaondoa kero; serikali moja tu ndiyo jibu sahihi; mapendekezo ya CCM ukiyaangalia kwa makini yanalenga kuelekea kwenye serikali moja; huko ndipo tunapoelekea. wanaopigania serikali 3 lengo kuu ni kuuvunja muungano na sio vinginevyo kuna maswali mwengi ya msingi mnashindwa kuyajibu. mimi ni muumini wa serikali 1 kwani naamini huo ndio utaleta sura moja ya kitaifa; hapa tulipo kwenye 2 ni rahisi sana kupata maridhiano ya serikali 1; napingana sana nyie kwasababu moja kubwa ni mnataka kuhodhi majadala wa katiba badala ya kujadili mambo ya msingi ambayo yanamgusa kila mtanzania mnatupotezea muda kujadili muungano; hivi mwananchi wa kawaida mkulima wa Sumbawanga kweli anahitaji kupotezewa muda kujadili huu muungano badala ya ardhi?? I don't give a fu2k if Zanzibar decides to break away, mainland we have nothing to loose!!
 
Nadhani mkuu unashindwa kutuelewesha hizo serikali mbili zilizoboreshwa zimeboreshwa vipi?
Maana mimi binafsi sijawahi kuona hiyo hoja unayoizungumzia. nA NDIYO UNACHOAMBIWA HUMU, labda it's just a matter of bad timing ungesubiri iwasilishwe kwanza.
 
chama, ndio maana nikawa na wasi wasi na uwezo wako katika kujadili hoja...cha kwanza kabisa unachosahau ni kwamba sisi wote, mimi na wewe tulikuwa waumini wazuri tu wa serikali moja. Tofauti na wewe ni kwamba sisi wengine hatutaki unafiki; we are realists who will call a spade a spade! Hoja ya serikali moja katika hali ya sasa inajaribu kujengwa katika msingi wa udanganyifu na watu walaghai ambao hawako tayari kuukubali ukweli kwamba hilo haliwezekani tena, si kwa hiari. Njia ya ushawishi imejaa visiki na misumari na njia pekee iliyobaki ni kulazimisha kwa kutumia nguvu.

Tuchukue mfano mdogo tu wa kero iliyoikumba Muungano kutokana na Katiba ya Jamhuri ya Tanzania kuvunjwa tena mchana kweupee! Aliyeapa kuilinda na kuitetea Katiba hakuweza kutumia mamlaka aliyopewa na Katiba hiyo hiyo kuhakikisha kuwa wahusika wanawajibika ama ikiwa lazima wanawajibishwa. Ni kuvunjwa huko kwa Katiba kulikoiua nia ya serikali moja kwa kuzaa nchi ndani ya nchi, kitendo ambacho duniani kote kinatambulika kama uhaini na kitendo ambacho hakiwezi kufumbiwa macho kwani kinahatarisha usalama wa nchi na kutia ufa katika msingi mkuu wa taifa.

chama, jaribio lolote la kuondoa hii kero haliwezi kufanikiwa bila mamlaka ya nchi kukiri kwamba Katiba ilivunjwa na kukiri hivyo maana yake ni kwamba aliyepewa mamlaka ya kuilinda na kuitetea Katiba anawajibishwa. Kila mwenye akili timamu anajua kwamba hilo haliwezekani katika mazingira ya sasa na ushahidi ni namna utawala ulivyo na hofu hadi umekataa kuheshimu maoni huru ya wananchi wake. Tumeshuhudia ndani ya BMLK jinsi wajumbe wengi walivyojikita katika kutoa kejeli na matusi kuliko kuelezea namna kero ya serikali mbili ndani ya nchi mbili inavyoweza kupatiwa ufumbuzi.

Kama Zanzibar iliweza kuthubutu kutenda hilo bila kukemewa, ni kitu gani , chama, kinakufanya uamini kwamba huu muundo wa serikali mbili, ulioruhusu Katiba kuchezewa bila hatua kuchukuliwa, utaweza kuondoa hizo kero zinazoongezeka siku hadi siku? Huo ubavu nani anao kama Raisi mwenyewe kwa miaka mitano kaufyata? Toka lini mafahali wawili wakakaa zizi moja na hali ikabaki salama? Jamani tuache utani na tuache kudanganyana, muundo wa serikali mbili unatetewa tu na jamii ya kifisadi inayoogopa kuwajibishwa na Wananchi kwa usaliti na hujuma walioifanyia Tanganyika.
 
Nadhani mkuu unashindwa kutuelewesha hizo serikali mbili zilizoboreshwa zimeboreshwa vipi?
Maana mimi binafsi sijawahi kuona hiyo hoja unayoizungumzia. nA NDIYO UNACHOAMBIWA HUMU, labda it's just a matter of bad timing ungesubiri iwasilishwe kwanza.
BLK lilianza kwa mjadala wa sura ya kwanza na sita. Katika hatua hiyo, ccm ililenga kuhakikisha inabomoa chochote kinachojenga mazingira ya serikali tatu au uzinduzi wa Tanganyika. Baada ya kufanikisha hilo, CCM ingepenyeza maboresho niliyojadili humu. Wazungumzaji wakuu na rasmi kwa haya wannasubiri muda muafaka. Lakini pia Kama ulikuwa unafuatilia bunge, wapo baadhi wa wachangiaji waliojitambulisha kutokea makundi ya "walio wengi" walisikika wakisema kwa juu juu kwamba Zanzibar itaruhusiwa kukopa, na mengine mengi niliyojadili, huku wakijenga hoja kwamba serikali mbili zitaboreshwa na kutatua kero za muungano. Inawezekana ukawa sahihi kwamba hoja yangu ni "bad timing", inahitaji kusubiri, lakini pia wapo wenye kuona kwamba, since huo ndio ukweli, hakuna ubaya kufanya a pre-emptive strike. All that said and done, you have a choice kusubiri kuchangia hadi August kama una amini ndio "good or best timing".
 
Nadhani mkuu unashindwa kutuelewesha hizo serikali mbili zilizoboreshwa zimeboreshwa vipi?
Maana mimi binafsi sijawahi kuona hiyo hoja unayoizungumzia. nA NDIYO UNACHOAMBIWA HUMU, labda it's just a matter of bad timing ungesubiri iwasilishwe kwanza.

Wakuu nadhani hali kwa kiasi fulani hali ya jukwaa au uzi huu, inaakisi tunachokiona kwenye bunge la katiba. Kuna baadhi wana busara, wengine wana matusi na wengine wanapiga porojo tu.l

Hoja ni kwamba serikali moja, ambayo kwa sababu zisizojulikana CCM haitaki, serikali mbili pia inaonekana CCM hiyo hiyo inaona zina dosari lakini na inataka kubadilisha inakiri kuwa sio nzuri, na serikali tatu CCM inasema kuwa haitaki.

Naweza kuelewa sintofahamu ya CCM, kwa kuwa kimsingi sasa haijui kama inasimamia maslahi ya serikali, ya chama, ya nchi au watanzania wote.

Tukiangalia hoja zinazotolewa hasa na upande wa CCM, kimsingi hazionesheni substance ya kukataa serikali moja, kung'ang'ania serikali mbili (na kutaka kuzibadilisha kujaribu kuondoa kero za muungno), na hata kupinga serikali tatu. Nadhani kwa kiasi fulani inaweza kueleweka ni kwanini baadhi wanatoa lugha mbaya, sababu ni kukosa hoja.
 
Back
Top Bottom