Tetesi: CCM si wamoja, hamna siri. Kumbe kamati kuu yenu iligawanyika pakubwa kuhusu sakata la kufukuzwa Membe?

Tetesi: CCM si wamoja, hamna siri. Kumbe kamati kuu yenu iligawanyika pakubwa kuhusu sakata la kufukuzwa Membe?

Na mgogoro wote huo mkubwa unaouona humo CCM hao wote waliopinga kutumbuliwa kwa Membe hamna kitu watafanya zaidi ya kulia lia tu huko pembeni.

Mwana CCM yoyote yule hata hao wa kamati kuu wakiwa nje ya CCM ni dhaifu sana na wanaweza kupigwa makofi hata na bodaboda au na mwanamke na chakufanya hawana.

So hawana namna zaidi ya kuikumbatia CCM kwa hali yoyote ile.
 
Hata wewe ungekuwa Magufuli usingetoka nje ya hicho maana ana taarifa nyingi kuhusu hilo jambo kuliko mwingine yeyote huenda hata kuliko Membe mwenyewe
Taarifa nyingi anazopewa, huwa ni udaku. Anazifanyia kazi, anaishia kuwaumiza watu bila sababu.
 
Kwenye maamuzi walitofautiana kwenye kuhitimisha wakakubaliana. Ndio maana unaona kilichotokea. Vinginevyo ungesikia wengine walijitoa au wasingefikia muafaka. Kwa hiyo usidhani walipofika kikaoni alichokuwa anawaza mangula ndio alichokuwa anawaza bashiru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya wajumbe wote wa kamati kuu ni watu watatu tu pamoja na msemaji wao ndiyo waliounga mkono Membe kufukuzwa. Hata aliyeongoza Tume ya Maadili, yaani Mzee Philip Mangula alipinga Membe kuvuliwa uanachama wa chama hicho, imedokezwa.

Wajumbe wengi walipendekeza Benard Membe kufungiwa kufanya siasa ndani ya chama hicho kwa muda maalum kama adhabu mbadala ili kuepuka kukigawa chama.

Adhabu kama hiyo ndiyo alipewa Kinana ambaye hata hivyo haiwezi kumuathiri kwa lolote lile kwani alishaachana na mambo ya siasa. Adhabu hiyo mbadala ilipingwa kwa nguvu zote na Katibu Mkuu wa chama hicho Dr. Bashiru Ally ambaye alisimamia Membe na Kinana kufukuzwa.

Taarifa zilizovuja ndani ya kamati hiyo zinadai kuwa wajumbe wa kikao hicho waliondoka bila ya kupata muafaka wa pamoja huku wababe wanne ambao walisimamia Membe kufukuzwa wakitoka na maamuzi yao.

My take: Upo uwezekano kuwa ndani ya CCM kuna mgogoro unaoendelea licha ya wachache kutuaminisha kuwa wanachama wake ni wamoja. Tusubiri tuone watakaoanza kuunga mkono msimamo wa Membe wazi wazi.
Duh!
yaani hizo statistics tu zinaonesha kama hii habari ni ya kutunga au la.
Kweli Akili za kuambiwa - Changanya na zako.
 
Bashiru anamini alichodanganywa kuwa nikitoka miye 2025 unaingia wewe tusafishe chama ajui ccm ina wenyewe yeye na pole pole wamepitiwa tu kama upepo wamejikuta wapo hapo walipo siku na tarehe azidanganyi nani alikuwa kiburi ndani ya ccm kama nape nauye, makamba junior, kina mwakyembe, kina lukuvi sasa hivi wapo kam watoto wa kambo kwa baba wa kufukia yani urithi hawana mpaka huruma ya baba amue awape nini sababu alikuwa nakaa na mama yao
 
Yeye na Chakubanga wanajiona ndiyo waasisi wa chama kumbe ni wa kuja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa siku watakayoondolewa suruali zitaloa mkojo. Kwakweli wanajisahau sana. Wanagawa adhabu tu mpaka kwa waasisi na mapapa wa chama.

Ngoja tuwaone hiyo siku chama kitakaporudishwa kwa wenye nacho.

Namwona bashiru akifukuzwa mpaka UD. Bashiru ni wa kuonea huruma sana. Angalau chakubanga alikulia kwenye kubangaiza hana kikubwa sana cha kupoteza.
 
Back
Top Bottom