GE2025 CCM Simiyu yamtupa nje Luhaga Mpina kuwania ubunge jimbo la Kisesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Maelekezo kutoka juu
 
Mpina ilikuwa uhitaji uwe mtabiri, sababu ilisha onekana na akihamia upinzani naona wataanza kumpa tuhuma za uongo ili wamsumbue na safari za kwa Pilato.
 
Ukiwa CCM ni swala la muda tu, Wanafiki hawajawah jenga nyumba moja mtu anachunga fito zake.
 
Mimi nilifikiri Mbunge anayetetea nafasi anakuwa miongoni mwa Wagombea watatu ambao majina yao yatarudi kwa ajili ya kupigiwa kura!
Hiki chama ni hatari sana!
Yaani hata usipokubali kuwa Tanzania inafanya vizuri kiuchumi kuliko US na West inakula kwako!
 
Ni kheri sana iwapo Mpina yuko ktk mioyo ya wana kisesa. Ni hazina isiyooza
 
Hivi Kisesa iko MAGU MWANZA ama ni Simiyu?
 
What goes around comes around
 
Hii ndiyo serikali ya Tanzania ndiyo maana hawataki kuwe na mgombea huru,
huyu angesimama kama mgombea huru angewapiga mapema,maana wanaomkubali ni wananchi siyo viongozi ambao nao wanafwata maelezo kutoka juu
 
Ila sa100 ana siasa za kijinga sana, yaani ndani ya chama chake hataki kukosolewa kbs..mbaya zaidi uwezo wake mdg hivyo makosa ni dhahiri so anataka mkae kimya tuu!
 
Wote wenye uthubutu wa kuhoji mamlaka hawatakiwi chamani
 
Ashukuru sio Magufuri,angekuwa Magufuri ambacho kingefata ingekuwa ni kumfilisi mali na kumuwekea figisu kwenye biashara zake
 
Wakitumaliza siye watahamia kuparurana wao Kwa wao.
 
Niambie mtu mmoja humu ambaye sio chawa kwa namna yake.
 
Wengi wao ni wanufaika wa uhuni wa jiwe na CCM hakuna haja ya kuwahurumia.

Kwenye Jimbo la Mpina lilizalisha wahanga wengi tu wa Uchaguzi wa 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…