GE2025 CCM Simiyu yamtupa nje Luhaga Mpina kuwania ubunge jimbo la Kisesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ili ukubalike na ku -survive ndani ya CCM, ni lazima uwe chawa kama kina Tlaatlaah, mihapase, Lucas Mwashambwa, Shotocan, Mtoto wa Shule etc kwa kukubali kulamba miguu ya walio juu yako, uuze utu na heshima yako na kuikana dhamira yako...

Mpaka hapo, luhaga Mpina, Mrisho Gambo, Kassim Majaliwa, Job Ndugayi na wengine sasa wataelewa maana na dhana iliyobebwa na kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION..

Lazima waelewe kuwa, hata huko ndani ya CCM yao, mabadiliko (reforms) ni hitaji la sasa na la lazima sana. Else, wakubali kukana dhamiri zao, wauze heshima na utu wao, wauze roho na nafsi zao kwa Jezebel...

La, wanajipenda kuuheshimu utu na dhamiri zao, basi, haraka sana, wajiunge na timu #NoReformsNoElection haraka, waingie vitani na kupigania nchi na taifa letu la Tanganyika...

Ninavyowafahamu CCM na mfumo wao, inawezekana kabisa hata mafao yake yote ya ubunge ya 400+M amenyimwa au yamekatwa kwenye mikopo huku wenzake wakisamehewa na kuvuta zote...
Sisi tunaosema ukweli CCM huwa hatupendwi. Angalia Masele kipindi cha jiwe
 
Ccm acheni kuonea kisa mtu Fulani anahoji serikali
Sasa wanacho shabikia kuwa upinzani hawana demokrasia sijui ni kitu gani sasa hapo na wao wana practice yale yale tena wao kwa nguvu ya mkono wa chuma CCM hovyo kabisa
 
Mbunge wa Taifa Luhaga Mpina Sasa ni wakati wa kuunga mkono juhudi za kuzuia uchaguzi wa hovyo twende na NO REFORMS NO ELECTION ✌️
 
Nchi hii wananchi ni chaguo la mwisho kwenye mikakati ya wanasiasa.
Ukijifanya uko upande wetu wanakuvunja ugoko
 
Mbunge wa Jimbo la Kisesa anayemaliza muda wake Luhaga Mpina huenda safari yake ya kuwawakilisha wananchi wa Kisesa ikafikia tamati ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu baada ya vikao vya mchujo kwa ngazi ya wilaya ya Meatu na mkoa wake wa Simiyu kumtupa nje ya mbio za kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu; vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya kikao cha kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu vimeitonya Jambo TV.

Mpina Mbunge machachari ndani na nje ya Bunge aliyejipatia umaarufu kwenye takribani miaka mitano sasa kwa kuibana serikali ndani ya Bunge na hata nje ya Bunge kwa hoja mbalimbali amekumbana na rungu la chama chake ngazi ya wilaya na mkoa baada ya vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Meatu kumtupa nje kwa kutopendekeza jina lake- maamuzi ambayo yamebarikiwa na chama ngazi ya mkoa hivyo sasa nafasi ya mwisho ya yeye kupenya jina lake kwa ajili ya kwenda kwenye mchakato wa kura za maoni ikibakia vikao vya ngazi ya taifa kwa maana ya Kamati Kuu ambayo imepewa mamlaka ya kufanya uteuzi wa mwisho.

Katika jimbo hilo, wagombea waliokuwa wakichuana katika hatua ya awali walifikia 14, lakini kupitia kikao cha wilaya na mkoa, majina yaliyopendekezwa ni Sitta Risinge, Mussa Mbuga, na Silinde Gumada.

Kiujumla, majina yote yaliyopendekezwa ngazi ya wilaya na mkoa hupelekwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, na Kamati kuu hiyo ina uwezo wa kuja na mapendekezo yake ya majina kwa kurejea majina ya awali ya wote waliochukua fomu, waliopendekezwa nkwa upande wa wilaya na hata yale ya mkoa.

Baada ya hapo Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitapokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge kwa ajili ya maandalizi ya vikao vya uteuzi, kisha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitafikiria na kuteua majina ya WanaCCM wasiozidi watatu walioomba nafasi ya Ubunge na ili wakapigiwe kura za maoni na hatua zaidi ndani ya chama zitafuata kabla ya kumpata mgombea atakayekiwakilisha chama katika jimbo husika.

Source: Jambo TV
Mbona tayari maagizo yashatolewa,!! Kuwa wasimchague!!
 
Yule mama alisema msiwapitishe magwajima...
 
Maelekezo toka juu.
 
Wananchi hawasikilizwi -father kitima

Ova
 
Wengi wao ni wanufaika wa uhuni wa jiwe na CCM hakuna haja ya kuwahurumia.

Kwenye Jimbo la Mpina lilizalisha wahanga wengi tu wa Uchaguzi wa 2020.
Kabisa, hata naye wakimfanyizia ni sawa tu.
 
Nchi hii ukijifanya kuwa mtetezi wa wananchi kwa kuihoji serikali. Basi inakuwa mwisho wako kisiasa. Nayo ni kwa sababu watu wameiendekeza Ccm kama hakimu wa mstakbali wao. Ccm ni ugonjwa
sio kuindekeza ccm, bali kundi la wahuni wanaoiendesha
 
Angalia wajumbe wenye bashasha,
Wamekuja wamevalia kijani,
Na khanga safi mabegani wameweka,
Kapero zao kichwani zinapendeza,
aeeeeeeeeh alo.
 
Back
Top Bottom