KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
Kuna wazee kule Dodoma walilalamika kuhusu matibabu. Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutumia ofisi za Kata ikatuma wafanyakazi wao kuja kuchukua picha za wazee wote wa Jiji na baadae wakatengenezewa vitambulisho. Waliambiwa kuvitumia hivyo vitambulisho kila waendapo hospitalini ili kupata matibabu ya bure.
Cha kusikitisha ni kwamba hivyo vitambulisho havikubaliki mahali popote hata huko vilikotolewa! Sera ya Wazee ya 2003 ipo lakini hakuna Sheria yeyote ambayo inawawezesha Wazee kupata matibabu bure kama ilivyoainishwa katika Sera hiyo. Hivyo hata hao Wazee wa Tabora wajue kabisa hicho ni kiini macho tu. Watumie kichinjio chao kwa busara ili kuweza kupata haki zao na si vinginevyo.