PreGE2025 CCM tujipange naona vijana wameamua agenda yao ni 'No Reforms, No Election'

PreGE2025 CCM tujipange naona vijana wameamua agenda yao ni 'No Reforms, No Election'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sasa Gen Z wetu nao wameielewa agenda baada kushtuliwa na Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kuwa Betting Gambling sio ajira.

NO REFORMS NO ELECTION
 
Jana katika kipindi cha MALUMBANO YA HOJA iliyohusu NINI NAFASI YA VIJANA KWENYE UCHAGUZI 2025. Kwa kweli vijana walisema mengi kuhusu mustakabali wa nchi yetu kuelekea uchaguzi wa 2025.

Kwanza waligusia Tume Huru ya Uchaguzi na wakasema kwa uwazi kuwa Tume hii si huru. Pili walisema kuwa ili kuwe na uchaguzi ulio huru basi marekebisho kwanza yafanyike kwenye Tume huru. Tatu waliunga dhana ya No reform No election na dhana hii kwa kweli imekwishaenea kwa vijana wengi nchini na hivyo kama Wana CCM inatubidi tujipange kuwaelemisha wananchi juu ya dhana hii.

Kama inavyoonekana mwaka huu wapiga kura wengi watakuwa vijana. Vijana safari hii wamepata mwamko mkubwa sana. CCM tujipange.
Elimu gani mtakayoitoa juu ya wizi wakura katika chaguzi na mkaeleweka labda vichaa pekee ndio mtawaza waelewesha wakaelewa kuwa hamuibi na hamtaiba kura kwenye chaguzi mbali mbali.
 
Msifananishe Gen Z wa Kenya na wabongo. Kwanza VIJANA wetu wana uelewa tofauti sana juu ya Haki na wajibu wao kwa nchi yao. Wapo wapo na shughuli zao zinazowaingizia kipato. Fursa ni nyingi ktk nchi hii kwa vijana kuweza kujipatia vipato vyao japo vidogo ukilinganisha na wale wa Kenya ambao hata siha zao tu zinaonyesha dhahiri ni mafukara waliopoteza matumaini.
VIJANA wa kitanzania hawalii njaa kwa sababu wanaweza kupata riziki zao ndogo ndogo bila kupigana.
Ninakuhakikishia hata kama CDM wataitisha maandamano, VIJANA hawatashoboka nayo kwa sababu wameshaona wapinzani wa nchi hii hawana tofauti na watawala. They look like the same.
Kwahiyo unamaanisha wako tayari kura zichezewe na ccm.
 
Hawawezi kuhangaikia na maandamano ya kijinga ya kususia uchaguzi. Hivyo tu
Ni kweli, na hata kura zao zikichezewa hawana tatizo, ili mradi wanaopora kura hizo ni ccm.
 
Back
Top Bottom