CCM tumemaliza risasi zote tetevu za Mkataba wa Bandari. Tunatokaje?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Mwanzoni, sikuwa namwelewa Wakili Mwambukusi. Alisema kuwa suala hili la Bandari halitaisha kirahisi kama ilivyozoeleka. Akasisitiza kuwa suala hili litapingwa mahakamani na siasasi. Ingawa nami tangu mwanzo naupinga bila kuvunga Mkataba wa Bandari wa DP World, niliitazama kwa wepesi kauli ya Mwambukusi.

Kama mwanasiasa mbobevu Serikalini na chamani, nikajipa muda na nfasi ya kufuatilia na kujionea ukweli wa kauli ya Mwambukusi. Ikatokea kesi ya kuupinga Mkataba huo kule Mbeya. Nikafika mahakamani mara mbili siku za kusikilizwa. Hakika, wapingaji walikuwa na hoja za haja. Lakini, Uamuzi ni wa Mahakama.

Kikaitishwa kikao cha NEC na Kamati Kuu Dodoma kujenga picha ya kuwa CCM imeitana kuusoma, kuuelewa, kuujadili na kuishauri Serikali juu ya Mkataba wa DP World. Kwakuwa nilikuwepo Dodoma kwenye vikao hivyo, mipango ikapangwa na kupangika. Likatoka tamko la kichama kuwa CCM inaunga mkono na kuishauri Serikali. Mambo yakagoma.

Ikamea na kuenea mikutano ya hadhara iliyoongeza hasira ya viongozi na makada wetu wa CCM. Makataba ukatetewa na kutetewa. Hauteteeki. ukaelezewa na kuelezewa. Hauelezeki. Hoja zikajibiwa na kujibiwa. Hazijibiki. Mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wakapanda majukwaani; wakashuka bila suluhisho.

Ikabaki risasi moja. Kumtafuta mtanzania yeyote 'anayeonekana' na 'kuaminika' kama mpinga Serikali na msemakweli ili auunge mkono Mkataba wa DP World. Yaani, apingane na wanaoupinga. Akapatikana Prof. Musa Assad, Mhadhiri na CAG wa zamani. Akapangwa na kupangika. Akatoka. Akasema. Amepuuzwa!

Inasubiriwa kwa hamu Hukumu ya Mbeya ili ipatikane njia ya kupitia. kesi ikitupwa, imepangwa kuzunguka na karatasi la Hukumu nchi nzima kuwaambia wananchi kuwa mabishano ya Mkataba wa Bandari yameisha. Amini nawaambia makada wenzangu wa CCM, huko ni kujidanganya. Mkataba wa DP World umekataliwa na mambo yake hayatapoa hadi uwekwe kando.

Tunatokaje kama chama tawala? Tukubali kuachana na mkataba huo na tuanze upya mchakato.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilwa, Lindi)
 
Hii aibu Samia aliyoamua kujibebesha hajui madhara yake, kosa wamefanya, wanaoneshwa kosa lao, wanaliona, ajabu wanakataa kulikubali, wanaamua kutuzungusha kwa maneno wakidhani sisi ni watoto wadogo mwishowe tutalala, hawataamini kwenye hili.
 
VUTA-NKUVUTE hembu fanya mpango hapa fisi round about tunywe supu ya pweza kwanza na karanga za kukaangwa kwa maganda huku tukisoma hukumu ya kubumba huko Mbeya!!
 
Mwanzoni, sikuwa namwelewa Wakili Mwambukusi. Alisema kuwa suala hili la Bandari halitaisha kirahisi kama ilivyozoeleka. Akasisitiza kuwa suala hili litapingwa mahakamani na siasasi. Ingawa nami tangu mwanzo naupinga bila kuvunga Mkataba wa Bandari wa DP World, niliitazama kwa wepesi kauli ya Mwambukusi.

Kama mwanasiasa mbobevu Serikalini na chamani, nikajipa muda na nfasi ya kufuatilia na kujionea ukweli wa kauli ya Mwambukusi. Ikatokea kesi ya kuupinga Mkataba huo kule Mbeya. Nikafika mahakamani mara mbili siku za kusikilizwa. Hakika, wapingaji walikuwa na hoja za haja. Lakini, Uamuzi ni wa Mahakama.

Kikaitishwa kikao cha NEC na Kamati Kuu Dodoma kujenga picha ya kuwa CCM imeitana kuusoma, kuuelewa, kuujadili na kuishauri Serikali juu ya Mkataba wa DP World. Kwakuwa nilikuwepo Dodoma kwenye vikao hivyo, mipango ikapangwa na kupangika. Likatoka tamko la kichama kuwa CCM inaunga mkono na kuishauri Serikali. Mambo yakagoma.

Ikamea na kuenea mikutano ya hadhara iliyoongeza hasira ya viongozi na makada wetu wa CCM. Makataba ukatetewa na kutetewa. Hauteteeki. ukaelezewa na kuelezewa. Hauelezeki. Hoja zikajibiwa na kujibiwa. Hazijibiki. Mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wakapanda majukwaani; wakashuka bila suluhisho.

Ikabaki risasi moja. Kumtafuta mtanzania yeyote 'anayeonekana' na 'kuaminika' kama mpinga Serikali na msemakweli ili auunge mkono Mkataba wa DP World. Yaani, apingane na wanaoupinga. Akapatikana Prof. Musa Assad, Mhadhiri na CAG wa zamani. Akapangwa na kupangika. Akatoka. Akasema. Amepuuzwa!

Inasubiriwa kwa hamu Hukumu ya Mbeya ili ipatikane njia ya kupitia. kesi ikitupwa, imepangwa kuzunguka na karatasi la Hukumu nchi nzima kuwaambia wananchi kuwa mabishano ya Mkataba wa Bandari yameisha. Amini nawaambia makada wenzangu wa CCM, huko ni kujidanganya. Mkataba wa DP World umekataliwa na mambo yake hayatapoa hadi uwekwe kando.

Tunatokaje kama chama tawala? Tukubali kuachana na mkataba huo na tuanze upya mchakato.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilwa, Lindi)
HAAA unajidanganya mkuu mkataba uko kihalali na hauna tatizo mmeumbuka vibaya na kesi yenu ya mchongo hahaaaa
 
Ndio hela pekee ya Uchaguzi kwa chama.
Ni mabilioni ya kutosha.

CCM hawawezi kuiachia hiyo.
 
Back
Top Bottom