CCM tumshauri Rais Samia asigombee 2025

Usilete ulaghai katiba sio tatizo. Wala hata ukileta katiba mpya unafikiri itawasaidia vipi wapinzani?
Kwa ufupi wapinzani hawana nguvu kwa sasa. Ila nakubali kitu kimoja kitawapa nguvu wapinzani. Mama sio visionary na anashindwa kuelewa uungwaji mkono ccm ni kwa msimamo wake hasa chini ya magufuli wa kutetea maslahi ya umma. Kitendo chake kuingia mkenge mkononi mwa fikra za kiliberali za kina january makamba ndio zinaweza hata kuifanya ccm kushindwa au kulazimika kupora ushindi kitu itakua ndio mwanzo wa kuondolewa madarakani ccm. Watu wabinafsi walevi wa mali na madaraka wenye nia ya kugeuza mafanikio ya magufuli ndio adui wa ccm.
Mama hana uwezo kuongoza ingefaa asigombee 2025. Anachotaka kufanya atawarudisha mafisadi wote kuhujumu maendeleo yenye kuweka mbele maslahi ya umma.
Tuanzeni kutafuta magufuli mpya kwa mustakabali wa nchi yetu.
Viva jpm, a luta continua, vinceremos.
 
Sielewi mpaka sasa kwa nini kanda ya ziwa wanahasira na CCM!

si vijana wala wazee, wote hawataki kitu inaitwa CCM, nadhani mapimduzi mapya yataanzia huko, licha kwamba hata Chadema hawaitaki, sijui itakuweje yani,

Hata mimi nataka CCM nao waanguke bhana, tumekaa nao sana aisee
 
Mtafute Mzee mtu mzima aongee nae Kama mnaona asigombee
 
Kimsingi mama anapaswa amalizie tu hii miaka minne aliyoirithi kisha mchakato wa kutafuta mgombea mwingine ufanyike. Mama hatoshi kwenye kiti
 
Watz kama mnataka chadema iwaongoze semeni na sio kuzunguka mbuyu. Alafu Msije mkalaumu baadae, heri act wazalendo kuliko cdm
 
Kimsingi mama anapaswa amalizie tu hii miaka minne aliyoirithi kisha mchakato wa kutafuta mgombea mwingine ufanyike. Mama hatoshi kwenye kiti
Sio kweli
 
Dah ila Africa sijui nani atakuja kutupandikiza akili timamu, kiongoz msomi anafanya mambo usiyoyatarajia,

Wenzetu wanazid kufanya maendeleo kitechnolojia sisi tunapambana na wapinzani. Sijui ni lini tutapambana na ujinga.
Hata wapinzani wa wenzetu huwa wanawaza mambo ya maana si kupambana na chama dola
 
Alishasema kuwa atagombea na cha kumfanya hamna
 
Sio kumshauri asigombee, Ila CCM iruhusu demokrasia kwa wanachama kuomba ridhaa ya chama kwa ajili ya nafasi ya urais
Miaka 10 ya uongozi wake na kiongozi mwenzake JPM, mwisho 2025
Katiba inamruhusu kugombea yeye ili kuanza utawala wake mpya, na hapo apambanie hio fursa na wanachama wenzake
 
Utaambiwa wewe ni mpinzani
 
Huyu mama hawezi kugombea 2025 atakuwa na miaka 64+ ..hatujawahi kuwa na raisi mzee..full stop
 
Anatafuta kuungwa mkono na wanawake ili ashinde uchafuzi....
 
Upinzani hawana mgombea wa kumutoa mtemi Hangaya,ila siku CCM ikimeguka ndo Mtemi Hangaya aanze kuimarisha makao yake kule zenji.

Maana vipande vitakuwa Msoga gang(Hangaya) vs Sukumagang.
Sukuma gang itashinda asubuhi kabla ya chai.
Maana Msogagang ilishakataliwa na wananchi siku nyingi, Mwendazake aliokoa jahazi na Watanzania bado wanaishi kwa falsafa za Mwendazake.mfano kidogo ni juu ya chanjo na kuvaa barakoa,mtemi Hangaya amebaki kuvaa barakoa peke yake na wanaokula mezani pake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…