kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Usilete ulaghai katiba sio tatizo. Wala hata ukileta katiba mpya unafikiri itawasaidia vipi wapinzani?Nawasalimia kwa jina la JMT wanajukwaa.
Ndugu zangu hasa Makada wa CCM mliopo humu msinihukumu kua natumikia kundi au mlengo flani ndani ya chama. Niwe muwazi ni kwamba kwa sasa binafsi naridhika sana na utendaji wa Mama kwa miaka 5 tu aliyeachiwa na hayati JPM. Angeishia miaka hii 5 tu.
Sisemi kuwa haziwezi siasa lakini kwa hali ninayoitazama mbele ya safari inaweza kuwa ngumu zaidi, wapinzani wetu wapo kimya lakini hatujui wanawaza nini na mshindani wa Mama atakuwa nani. Kwanza CCM imeshaanza kugawanyika makundi ambayo binafsi sioni mtu wa kuyaweka pamoja kwa sasa, haya makundi kuna yapo yanayougulia maumivu makali sana na kuna yapo yanayopooza maumivu makali. Shida kubwa ni kwamba hayupo wa kuyaweka haya makundi pamoja, tofauti ya mitizamo ni kubwa mno.
Tunaweza kujifariji kwa kuzuia suala la katiba mpya itakayoondoa uwezekano wa Makada wenzetu kusimamia uchaguzi, lakini kuna wakati unaweza kufanya hujuma kubwa mpaka ukaaibika, huenda tunaweza kuelekea mahali ambapo mtu akishinda wananchi hawatakubali aporwe ushindi wake. Tusijifariji kuja kutegemea Dola itusaidie, tunaweza kuja kuaibika vibaya mno. Dola kuna wakati inachoka kutumiwa itakapobidi. Tumshauri Mama asimame kwa miaka mitano aliyorithi toka kwa JPM.
Gharama za maisha zinapanda kimya kimya, Miamala ya simu na vifurushi vya internet zinapandishwa kimya kimya, gharama mafuta ya kula,sukari, petroli,diesel,mafuta ya taa, vifaa vya ujenzi usiseme, Luku makato bila ya watu kuridhia, vurugu kwa wamachinga. Kiukweli watanzania siyo wajinga tusubiri tuadhibiwe ili tupate adabu miaka mitano watakayobeba wapinzani.
Tunaweza kufika mahali wapinzani wetu wakalazimisha katiba mpya wakatoka barabarani nchi nzima kuiomba, hivi polisi wanaweza kukamata kwa mfano wanachama wa CHADEMA million 6 nchi nzima? Watawaweka mahabusu zipi? Hata wakitoka milion 3 watawaweka wapi? Kuna mambo tunayafanyia mzaha lakini CCM mbele yetu hali ni tete.
Tungeruhusu katiba mpya tupambane kwa huo mfumo mpya badala ya mazoea na kuwapa kiki wapinzani. Hawa wapinzani tumewapa pumzi ya kua nje ya bunge miaka 5, hatujui wanarudi vipi na nguvu mpya.
Ni mawazo ya kada huru, hulazimishwa kuyachukua au kuyasoma.
Weekend njema!
Kwa ufupi wapinzani hawana nguvu kwa sasa. Ila nakubali kitu kimoja kitawapa nguvu wapinzani. Mama sio visionary na anashindwa kuelewa uungwaji mkono ccm ni kwa msimamo wake hasa chini ya magufuli wa kutetea maslahi ya umma. Kitendo chake kuingia mkenge mkononi mwa fikra za kiliberali za kina january makamba ndio zinaweza hata kuifanya ccm kushindwa au kulazimika kupora ushindi kitu itakua ndio mwanzo wa kuondolewa madarakani ccm. Watu wabinafsi walevi wa mali na madaraka wenye nia ya kugeuza mafanikio ya magufuli ndio adui wa ccm.
Mama hana uwezo kuongoza ingefaa asigombee 2025. Anachotaka kufanya atawarudisha mafisadi wote kuhujumu maendeleo yenye kuweka mbele maslahi ya umma.
Tuanzeni kutafuta magufuli mpya kwa mustakabali wa nchi yetu.
Viva jpm, a luta continua, vinceremos.