CCM tunaenda mbele au tunarudi nyuma? Hii ya Kibajaji kuwa mchangiaji wa kwanza Bajeti nyeti ya Waziri mkuu ni kama " babeli"

Fisi kwa kawaida ni mlafi. Ikifikia wakati hawawezi kupata kitoweo ni wazi humtafuta mwenzao dhaifu (mgonjwa au mzee na kisha humtafuna).
 
HAKIKA SIAMINI MACHO YANGU KWA HII THREAD YAKO.

Nikupongeze kutoka moyoni kabisa kuwa sasa umeamua kukata minyororo uliyokuwa umefungwa.
 
Huo ubunge walipata kwa kufuata kigezo cha ujinga wao huo maana ccm inawategemea watu wa aina hiyo siyo kwa bahati mbaya.
 
Ngoja Nijikite ktk Kuwatafasilia "Kibajaji na Musukuma," Kwani Kwao Hii NGENGE ni Mtihani Mkubwa wanadhani umewasifia... "Tusidharau Wajinga Wana Nguvu Kubwa Hasa Wawapo ndani ya Kundi Kubwa".
Kwa hawa mimi nitawadharau na kamwe sitowaheshimu.
Haiwezekani wawe watu wa kutukana na kudharau elimu.

Nashindwa kujua ni kwanini profesa Ndalichako waziri wa elimu anakaaa kimya wakati anadhalilishwa?
 
Spika na ofisi yake wanaamini kibajaji, msukuma na aina zao ndio wachangiaji wenye akili kuliko wote!!
 
Hili linachangizwa na ndungai mi ningeshauri wabunge wasomi wasichangie wawaachie hao std7 walioandaliwa na spika waongoze nchi kupitia bunge.
Hilo nakubaliana na wewe kwa 100%. Ndugai kaidhalilisha mno Mhimili wa Bunge.
 
Hii akili imekuja na mwezi mtukufu au inapita tuu?
Wanaccm wangebadilika kama johnthebaptist walao kwa mwezi mmoja tuu taifa hili lingeyaona mabadiliko makubwa
 
Hawa wanaoshabikia kutengenezwa mtaala wa watoro wa shule wanawakatisha tamaa wasomi na wanaosoma sasa.Wanahakikisha Sera hazijali na kuenzi wasomi,wanafanya kazi za umma kwa ujira mdogo na mazingira magumu ya kazi.Wanakimbilia kwenye Siasa na kushindanishwa na STD VII kupigania maslahi manono wanayoyafaidi wana wa siasa chakavu.
Tusipothamini na tukiruhusu Elimu kudhihakiwa kupitia Bunge letu,tusije kujilaumu mbeleni tukigeuzwa ndondocha na hii CCM.
Katika dunia hii ya karne ya 21 tunashabikia ujinga na huku tukishangilia ni tusi kwa Uhuru wetu.Tukiwaruhusu failures kuitawala nchi na kutarajia kuwa tutaendelea itakuwa ni ndoto ya mwendawazimu kutimia.
 
Wewe umeacha lini kuwa kenge?
 

..unaweza kutanguliza darasa la saba kuchangia, baada ya hapo unatoa nafasi kwa wabunge wasomi wachangie na kufunga mjadala.

..nadhani utaratibu huo utapunguza uwezekana wa wabunge darasa la 7 kuharibu mjadala, kwa kuponda, na kupotosha, hoja za wabunge wasomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…