CCM: Tutamjadili kwanza Benard Membe

CCM: Tutamjadili kwanza Benard Membe

Chama cha Mapinduzi kimemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Act Wazalendo mwaka 2020 na baadae kutangaza kujitoa kwenye chama hicho, na sasa ametangaza safari ya kurudi CCM chama chake kilichomlea na baadae kumfukuza kutokana na utovu wa nidhamu kuwa kitamjadili kwanza ili wamuone kama wamkubalie kurudi CCM au la.

CCM yazungumzia kauli ya Membe

=======

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema yuko njiani kurudi mahali fulani akishamaliza kusikiliza uamuzi wa shauri lake lililopo mahakamani Oktoba 12, mwaka huu.

Licha ya Membe kutoweka wazi mahali atakaporudi lakini inaonekana atarejea Chama cha Mapinduzi (CCM) alikovuliwa uanachama Februari 28, 2020 kwa madai ya kukiuka maadaili na mwenendo usioridhisha tangu mwaka 2014

Jana akiwa kwenye mkutano wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Membe alisema anamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na yupo tayari kumpigia kampeni katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga alisema kama alivyoondoka, akiomba kurejea atajadiliwa.

“Akiomba vikao vinavyohusika vitamjadili, vinaweza kumpokea au kumkataa. Aliondoka na anataka kurudi, basi kuna taratibu na kanuni. Ataomba, atajadiliwa, akionekana ana sifa za kurudi basi atarudi. Asipofikia kiwango atakataliwa,” alisema Lubinga alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu.

Julai, 2020 Membe alijiunga na chama cha ACT Wazalendo na baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu akichuana na John Magufuli (CCM) na Tundu Lissu (Chadema) na wagombea wengine.
CCM ni chama chenye weledi.....

Alijirudi Komredi Lowassa na kupokelewa nyumbani tena.....

Haitoshindikana kwa Komredi Bernard Camilius Membe......

#SiempreJMT
 
Julai, 2020 Membe alijiunga na chama cha ACT Wazalendo na baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu akichuana na John Magufuli (CCM) na Tundu Lissu (Chadema) na wagombea wengine.
Yeye anasema hajawahi kukihama chama!
 
Chama cha Mapinduzi kimemjibu aliyekuwa mgombea urais wa Act Wazalendo mwaka 2020 na baadae kutangaza kujitoa kwenye chama hicho, na sasa ametangaza safari ya kurudi CCM chama chake kilichomlea na baadae kumfukuza kutokana na utovu wa nidhamu kuwa kitamjadili kwanza ili wamuone kama wamkubalie kurudi CCM au la.

CCM yazungumzia kauli ya Membe

=======

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema yuko njiani kurudi mahali fulani akishamaliza kusikiliza uamuzi wa shauri lake lililopo mahakamani Oktoba 12, mwaka huu.

Licha ya Membe kutoweka wazi mahali atakaporudi lakini inaonekana atarejea Chama cha Mapinduzi (CCM) alikovuliwa uanachama Februari 28, 2020 kwa madai ya kukiuka maadaili na mwenendo usioridhisha tangu mwaka 2014

Jana akiwa kwenye mkutano wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Membe alisema anamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na yupo tayari kumpigia kampeni katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga alisema kama alivyoondoka, akiomba kurejea atajadiliwa.

“Akiomba vikao vinavyohusika vitamjadili, vinaweza kumpokea au kumkataa. Aliondoka na anataka kurudi, basi kuna taratibu na kanuni. Ataomba, atajadiliwa, akionekana ana sifa za kurudi basi atarudi. Asipofikia kiwango atakataliwa,” alisema Lubinga alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu.

Julai, 2020 Membe alijiunga na chama cha ACT Wazalendo na baadaye aliteuliwa kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu akichuana na John Magufuli (CCM) na Tundu Lissu (Chadema) na wagombea wengine.
Mguse unuke?
 
All crews wa Msoga hawawezi kugomewa kujoin the team. Huo ni mkwara mee tu!
 
kwa utamamaduni wa CCM, kauli ya Mwenyekiti wa chama ni ya mwisho, vikao ni justifications tu - so far Membe kasharudi CCM tayari, kitakachosubiriwa ni vikao kubariki ujio.
Binafsi niliwahi kuwaonya the so called wapinzani, kuwa watu kama akina Membe wanapelekwa kwenye vyama hivi kwa kazi maalum. Akimaliza kazi aliyotumwa basi anajirudia NYUMBANI! Wako wengi tu wanaotumwa na kisha kurudi CCM na watazidi kutumwa tu - wewe subiri come 2025 utaona - na ukiwa na kumbukumbu ya maneno yangu haya - UTANIAMBIA!
 
Back
Top Bottom