GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Wanabodi,Siku nne kabla ya uchaguzi ngome zetu wana CCM hasa vijijini zimechakazwa na kutikiswa na Tundu Lissu.
Wilaya ya Tunduru Ruvuma, Mambo sio mambo ni ngome yetu wana CCM lakini wananchi wa miaka mitano iliyopita sio wananchi wa mwaka huu 2020 wamebadilika na kutugeuka kabisa.
Hii wilaya ni picha au taswira tosha kuwa sasa kunakoitwa vijijini sio vijijini tena kuna werevu na waelewa wengi kuliko mtazamo wetu ndani ya chama chetu CCM.
Mkutano wa Tundu Lissu huko Tunduru leo umenifanya nibadili taswira ya chama chetu ccm kuwa lazima sasa tubadilishe mfumo mzima wa itikadi na mawazo juu ya wananchi wa vijijini.
Mosi, CCM ikishinda na tutashinda ni muda wa kuanzisha siasa za usawa ,Maeneo tuliyoyaita vijijini leo sio vijijini tena kwani yana michanganyiko ya watu kutoka mijini hivyo madhara ya mitazamo juu ya CCM imetapakaa kila kona.
Pili, Uelewa wa wananchi umeongezeka sana kutokana na teknolojia ya mawasiliano hasa simu za mikononi hivyo imepelekea watu kujua ukweli halisi wa nchi inavyoendeshwa. Haya ndio madhara ya shule za kata kwa ccm wale wanafunzi hata kama wengi walipata sifuri lakini kuna kitu waliondoka nacho kidogo shule ambacho wanawaeleza ndugu na jamaa huko vijijini.
Kuanzia mwaka 2021 kuelekea mwaka 2025 ni muda wa kuanzisha mahusiano mema kwa kila chama na kurudisha furaha kwa wananchi tena. Madhara ya chuki yameshaonekana huko vijijini kwa wananchi kuanza kukisaliti chama cha mapinduzi.
Kuanzia 2021 ni muda wa kuwa waumilivu na kuruhusu hoja mbadala, Tuache watu waongee ya moyoni, wataongea kwa hasira lakini usiku watalala, Baada ya miaka mitano hawatakuwa na kinyongo kama sasa ambapo wanakwenda kutuadhibu mpaka wilaya kama Tunduru porini huko.