Uchaguzi 2020 CCM Vijijini Tundu Lissu ametikisa ngome ni muda wa CCM kubadili itikadi na mikakati

Uchaguzi 2020 CCM Vijijini Tundu Lissu ametikisa ngome ni muda wa CCM kubadili itikadi na mikakati

Wanabodi,Siku nne kabla ya uchaguzi ngome zetu wana CCM hasa vijijini zimechakazwa na kutikiswa na Tundu Lissu.

Wilaya ya Tunduru Ruvuma, Mambo sio mambo ni ngome yetu wana CCM lakini wananchi wa miaka mitano iliyopita sio wananchi wa mwaka huu 2020 wamebadilika na kutugeuka kabisa.

Hii wilaya ni picha au taswira tosha kuwa sasa kunakoitwa vijijini sio vijijini tena kuna werevu na waelewa wengi kuliko mtazamo wetu ndani ya chama chetu CCM.

Mkutano wa Tundu Lissu huko Tunduru leo umenifanya nibadili taswira ya chama chetu ccm kuwa lazima sasa tubadilishe mfumo mzima wa itikadi na mawazo juu ya wananchi wa vijijini.

Mosi, CCM ikishinda na tutashinda ni muda wa kuanzisha siasa za usawa ,Maeneo tuliyoyaita vijijini leo sio vijijini tena kwani yana michanganyiko ya watu kutoka mijini hivyo madhara ya mitazamo juu ya CCM imetapakaa kila kona.

Pili, Uelewa wa wananchi umeongezeka sana kutokana na teknolojia ya mawasiliano hasa simu za mikononi hivyo imepelekea watu kujua ukweli halisi wa nchi inavyoendeshwa. Haya ndio madhara ya shule za kata kwa ccm wale wanafunzi hata kama wengi walipata sifuri lakini kuna kitu waliondoka nacho kidogo shule ambacho wanawaeleza ndugu na jamaa huko vijijini.

Kuanzia mwaka 2021 kuelekea mwaka 2025 ni muda wa kuanzisha mahusiano mema kwa kila chama na kurudisha furaha kwa wananchi tena. Madhara ya chuki yameshaonekana huko vijijini kwa wananchi kuanza kukisaliti chama cha mapinduzi.

Kuanzia 2021 ni muda wa kuwa waumilivu na kuruhusu hoja mbadala, Tuache watu waongee ya moyoni, wataongea kwa hasira lakini usiku watalala, Baada ya miaka mitano hawatakuwa na kinyongo kama sasa ambapo wanakwenda kutuadhibu mpaka wilaya kama Tunduru porini huko.
Korshow
 
Mkuu sidhani kama wewe ni mwana ccm

Unaleta mipasho na taarabu tu ,Kuna muda yapasa utumie kichwa chako kufikiri sio kukibeba kichwa juu ya mabega kama mzigo sawa na mizigo mingine

Mkuu hapa sio Facebook au Instagram hapa kuna wataalamu ,wabobezi na wasomi ,Ujinga wako peleka Facebook huko,Hapa ni takwimu na data zinaongea

Poroja na ujinga waachie wana ccm wa facebook huko

Sisi wana ccm wa JF ni wasomi na wataalamu wa report na tumefanya kazi duniani huko ,kwanini unaleta ushamba na ujinga ?

Waanzilishi wa chama ccm Mwalimu Nyerere alikuwa anajenga hoja na alishawishi watu tutafute uhuru

Hotuba ya kikwete akiwa Mwalimu Nyerere Memorial university alieleza kuwa Mwalimu Nyerere hakuogopa hoja na hoja hazipigwi lungu

Wewe unajiita mwana ccm huna kazi hapa JF zaidi ya kuleta ngonjera,mipasho na taarabu

Jaribu kushauri Chama nini kifanyike na wapi kunahitajika maboresho

Taarabu,Mipasho,Ngonjera ni mambo ya kiswahili na kishamba sana

Tushauri chama
Umeandika kweli tupu ccm ibadilishe propaganda na I hire watu smart wakuendana na hichi kizazi maana uelewa wa wananchi ni mkubwa hawadaganyiki mipasho haina nafasi. Ccm ishukuru kubebwa na Dola bila hvo ingeshazikwa siku nyingi na kusahaulika
 
Kupiga wananchi mabomu ni uduanzi.Manake wao ndio wapiga kura.Leo wakimsikiliza Jiwe kesho watamsiliza TL.Sasa kama watu waliokusikiliza Jana halafu leo unawapiga mabomu Bado unategemea wakupigie kura?Au ndio sikio la kufa halisikii dawa!
 
Mkuu sidhani kama wewe ni mwana ccm

Unaleta mipasho na taarabu tu ,Kuna muda yapasa utumie kichwa chako kufikiri sio kukibeba kichwa juu ya mabega kama mzigo sawa na mizigo mingine

Mkuu hapa sio Facebook au Instagram hapa kuna wataalamu ,wabobezi na wasomi ,Ujinga wako peleka Facebook huko,Hapa ni takwimu na data zinaongea

Poroja na ujinga waachie wana ccm wa facebook huko

Sisi wana ccm wa JF ni wasomi na wataalamu wa report na tumefanya kazi duniani huko ,kwanini unaleta ushamba na ujinga ?

Waanzilishi wa chama ccm Mwalimu Nyerere alikuwa anajenga hoja na alishawishi watu tutafute uhuru

Hotuba ya kikwete akiwa Mwalimu Nyerere Memorial university alieleza kuwa Mwalimu Nyerere hakuogopa hoja na hoja hazipigwi lungu

Wewe unajiita mwana ccm huna kazi hapa JF zaidi ya kuleta ngonjera,mipasho na taarabu

Jaribu kushauri Chama nini kifanyike na wapi kunahitajika maboresho

Taarabu,Mipasho,Ngonjera ni mambo ya kiswahili na kishamba sana

Tushauri chama
Mkuu hapa umeongea ukweli kama Mtanzania Mzalendo. Sijawahi ku like comments zako tangu 2014 lkn leo nimekupatia.

Tunahitaji mawazo ya kuijenga Nchi yetu kwani Tanzania ni yetu sote. Hawa wachache wanaojiona kuwa ni bora kuliko wengine leo wamejifunza kitu kutoka kwako.

Siasa siyo uadui. Siasa safi na uongozi bora hudumisha amani kwenye Nchi yetu. Tukizingatia hayo kama Nchi tutapiga hatua kiuchumi. Na uchumi huo utaonekana kwenye maisha yetu ya kila siku.
 
Back
Top Bottom