CCM vs Dkt. Bashiru: Nini kinaendelea?

Mimi nilimchukia sana Bashiru enzi za mwendazake zake kwa ushenzi waliofanya,lakini nimemkubali sana juzi kwa jinsi alivyowajambisha maccm.
 
Katibu wa ccm kusema ya moyoni alikuwa ndg Kolimba (RIP) aliposema Chama kimepoteza dira.Wote tunakumbuka yaliyomsibu mara tu baada ya kuhojiwa na chama chake.Lakini nawe Bashi ungelisema nadhani viongozi tumekosa kutowashukuru wakulima na wafanyakazi kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu.Maana nawe ulikuwa huko
.
 
Bashiru ni mlafi wa madaraka, chama kinamtwanga vilivyo
SSH amefanya sana uungwana angeweza kummwaga mazima baada ya kutangaza baraza la mawaziri.

SG walijificha mwanzoni lakini wameamua kujiweka wazi kabisa kwamba wanapambana na SSH. Walimtumia Mpina bungeni kama askari wa siri lakini sasa wameinua kabisa silaha tayari kwa mapambano.
 
Bashiru alisema nini . Mimi niliona kama vile amesema Serikali ikifanya wema hakuna sababu ya kusema asante kwa vile ule ni wajibu wa Serikali.
 
Bashiru alisema nini . Mimi niliona kama vile amesema Serikali ikifanya wema hakuna sababu ya kusema asante kwa vile ule ni wajibu wa Serikali.
Ndiyo, kauli hiyo iliwakera vijana wa UVCCM
 
ccm ni ukoo wa mafisi... waliwanyonyoa makatibu wao wakuu (Makamba na Kinana) kwa nyati fulani... Wakawanyamazisha wenyeviti wao (Mwinyi, Kikwete na Mkapa)... Wakanyonyoa spika wao... Na sasa wanashughulika na Bashiru wa ccm.
 
Bushiru anajenga utamaduni wa uwajibikaji ambao hauna cha kurudisha ASANTE. Hivi nikienda ofisi ya mtendaji akanihudumia vizuri na nisimsifu kuwa wewe ni mtendaji mzuri atachukia kwa vile sikumpa sifa hiyo,sidhani huo utakuwa ni wajibu wake ametekeleza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…